Shule 24 zafungiwa kuwa vituo vya Mitihani kwa udanganyifu

Karibia zote kama si zote ni zile wanafunzi hupanda mabasi ya njano.Ukiangalia matokeo yao unakutana na wastani wa A nyiiingiii.Kumbe utapeli mtupu.
 
Wizi ya mitihani kwa watoto wetu tena shule za msingi. Chama tawala chaiba chaguzi mchana kweupe. Tunasimamia nini? Kama nchi tunavalueszipi? Hao watoto tunawafundisha nini?
 
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limezifungia shule 24 kuwa vituo vya mitihani ya Taifa baada ya kuthibitika kupanga kufanya udanganyifu katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.

Shule hizo ambazo ni sawa na asilimia 0.13 ya vituo vyote vya mitihani nchini, ndani yake zipo shule maarufu ikiwemo ya Musabe ya jijini Mwanza na St Anne Marie ya jijini Dar es Salaam na shule ya Rweikiza ya mkoani Kagera.

Hayo yameleezwa leo Desemba Mosi na Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amasi wakati akitangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2022.

Akizitaja shule hizo ni Kadama shule ya msingi iliyopo Chato- Geita, Rweikiza (Bukoba), Kilimanjaro shule ya msingi (Arusha) Sahare (Tanga), Ukerewe (Mwanza), Peaceland (Mwanza), Karume (Kagera), Al-hikma (Dar es Salaam)

Nyingine ni Kazoba (Kagera), Mugini (Mwanza), Busara (Mwanza), Jamia (kagera), Winners (Mwanza), Musabe (Mwanza), Elisabene (Songwe), High Challenge (Arusha), Tumaini (Mwanza), Olele (Mwanza), Mustlead (Pwani).

Pia zipo shule za Moregas (Mara), Leaders (Mara), Kivulini (Mwanza) na St Severine (Kagera).

“Vituo hivi vimefungiwa kwa mujibu wa kifungu 4(8) cha kanuni za mitihani mwaka 2016 hadi hapo Baraza litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa mitihani ya kitaifa,” amesema.

Mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi ulihusisha watahiniwa zaidi ya 1.38 milioni nchi nzima.
Matokeo yao lini hawa
 
Kanda ya ziwa imetia Fora. Wajifunze kwanini Kilimanjaro kuna Quality education...huu upuuzi hawa untertain na nakumbukuka kipindi hicho walimu na wasimamizi walikua wakali kama Mbogo.

Ila sishangai maana ma Role model wao ni PHD holder Darasa la Saba B kingi Msukuma.
 
Back
Top Bottom