Shule 24 zafungiwa kuwa vituo vya Mitihani kwa udanganyifu

Shule 24 zafungiwa kuwa vituo vya Mitihani kwa udanganyifu

OLYMPIO NAYO naona wameandika * W* wanafunzi wote. naona matokeo yamezuiliwa
 
Utakuta wengine watoto hadi sasa wanasoma "PRE-FORM ONE" alafu unatokea ujinga Kama huo. Tatizo ni tamaa ya kuongoza kitaifa na kusifiwa ilishule ada ipande.
 
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limezifungia shule 24 kuwa vituo vya mitihani ya Taifa baada ya kuthibitika kupanga kufanya udanganyifu katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.

Shule hizo ambazo ni sawa na asilimia 0.13 ya vituo vyote vya mitihani nchini, ndani yake zipo shule maarufu ikiwemo ya Musabe ya jijini Mwanza na St Anne Marie ya jijini Dar es Salaam na shule ya Rweikiza ya mkoani Kagera.

Hayo yameleezwa leo Desemba Mosi na Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amasi wakati akitangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2022.

Akizitaja shule hizo ni Kadama shule ya msingi iliyopo Chato- Geita, Rweikiza (Bukoba), Kilimanjaro shule ya msingi (Arusha) Sahare (Tanga), Ukerewe (Mwanza), Peaceland (Mwanza), Karume (Kagera), Al-hikma (Dar es Salaam)

Nyingine ni Kazoba (Kagera), Mugini (Mwanza), Busara (Mwanza), Jamia (kagera), Winners (Mwanza), Musabe (Mwanza), Elisabene (Songwe), High Challenge (Arusha), Tumaini (Mwanza), Olele (Mwanza), Mustlead (Pwani).

Pia zipo shule za Moregas (Mara), Leaders (Mara), Kivulini (Mwanza) na St Severine (Kagera).

“Vituo hivi vimefungiwa kwa mujibu wa kifungu 4(8) cha kanuni za mitihani mwaka 2016 hadi hapo Baraza litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa mitihani ya kitaifa,” amesema.

Mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi ulihusisha watahiniwa zaidi ya 1.38 milioni nchi nzima.
Mbona nyingi ni za ukanda mmoja...?
 
Kwa hiyo Mkuu ulionyeshwa paper.

Huoni dhambi inawahusu nyote nyie watu wangedhibiti hii hali watoto wa watu Leo wasingewekwa kwenye sintofahamu. Mtoto siku zote Hali yake kubwa ni kuongozwa na kuendelezwa. Hii ni sahihi kweli
Una majibu yako tayari Mana naona unakimbilia kujudge.
Half told story isikukimbize puta.
Wangekuwa wanapewa mitihani kila mwaka wangeongoza
 
Achilia mbali mbweni hata madarasa ya o level hadi a level ni Kama mabanda ya kufugia nguruwe

USSR
Hahahah nimetoroka sana kwenda mbezi angalia mpira....
 
Mwisho wa siku mzazi ndo anaumia zaidi kwa huu ujinga unaofanywa na hizo baadhi ya shule.

Sababu kiukweli Std VII inakuwaga na mahitaji 100 kidogo kwa ajili ya kumuandaa mtoto kumbe nyuma ya pazia walimu wana mbinu zao za hovyo kabisa.
 
Kama unawalazimisha walimu wakuletee matokeo ya A zote unategemea nn

USSR
Rweikiza Mimi nilimwambia,kufaulu kwa magumashi kutamcost akakataa.Sasa najua ananikumbuka.Magumashi Sana,eti mkuu wa shule ni form six leaver tu,unategemea nini?
 
Back
Top Bottom