Shule binafsi zaanza kukusanya Ada Kidato cha Kwanza 2025

Shule binafsi zaanza kukusanya Ada Kidato cha Kwanza 2025

Kwenda secondary Sio lazima mtoto awe kamaliza darasa la saba Kwa shule za secondary za private
Nimesoma uliandika ukafuta. Kama kwenda secondary sio lazima mwanafunzi apitie la saba, Je Kuna umuhimu gani wa NECTA kutunga mitihani ya darasa la saba (PSLE) kwenda sekondari
 
Ikiwa bado hata nusu mwaka wa kalenda 2024 hatujafika na Hata darasa la 7 hawajafanya mitihani. Tayari shule kadhaa binafsi zimeanza kukusanya Ada kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha 1 mwakani (2025). Hii si sawa.

Kama sio sawa, wewe acha kumpeleka mtoto wako hapo...

Elimu iko kwenye soko huru pia. It's a competition..

Kuna shule hapa hapa nchini mojowapo iko Kahama - Shinyanga ikiendeshwa na kusimamiwa na Masista wa Kanisa Katoliki (Shule ya wasichana tu Kidato cha I - IV Boarding) ifikapo mwezi Septemba kila mwaka huwa hawana nafasi za wanafunzi kidato cha I kati ya 200 wanaowahitaji kwa mwaka unaofuata wa masomo..

Kwanini?

Kwa sababu wanatoa elimu bora na usimamizi wa malezi bora na kila mzazi hupenda mtoto wake akasome hapo. Hivyo competition ya kupata nafasi hapo huwa ni kubwa sana kiasi cha kuwahiana tu..

Wao wana Entry Examinations ya kwao. Hawachukui wanafunzi kwa kigezo cha ufaulu wa mtihani wa DRS LA VII. Kila mwaka hupokea applications zaidi 2000 huku nafasi zikiwa ni 200 tu..

Kuna wazazi hupeleka wanafunzi kufanya mitihani hiyo hata kabla ya kufanya mitihani yao ya taifa DRS la VII. Mfano mtihani wa mwaka huu ni mwezi Septemba, wao tayari walishafanya Entry Exam ya kwanza. Ya pili itafanyika mara baada ya mtihani wa DRS la VII mwezi Septemba..

Pesa inayolipwa sasa ni ya English Orientation Course (au Pre Form Course) ya siku 90 (miezi mitatu) ambayo itaanza mwezi October - December. Kiwango hutofoutiana shule na shule..

Generally speaking ni kuwa, there is no problem kwa hiki kinachofanyika sasa so long as mzazi ameridhika kuwa pesa yake haitapotea na mtoto wake atakwenda kupata elimu anayoitaka..

Na kwa shule ambazo zilishajenga credibility ya utoaji elimu, wazazi hatuangalii gharama. Tunachoangalia ni kama uwekezaji wangu kwa mtoto wangu utalipa..
 
Nimesoma uliandika ukafuta. Kama kwenda secondary sio lazima mwanafunzi apitie la saba, Je Kuna umuhimu gani wa NECTA kutunga mitihani ya darasa la saba (PSLE) kwenda sekondari
Hiyo ni.kwa ajili ya kupima wanafunzi wake wanaosoma shule za serikali ndio maana shule ya secondary za private Huwa na mitihani Yao ya mwanafunzi kujiunga kidato Cha kwanza hawategemei hiyo ya kumaliza msingi ya NECTA
Wana iamini ya kwao zaidi

Mtoto hata akiwa darasa la Tano aweza fanya mitihani ya kujiunga kidato Cha kwanza private akifaulu wanamchukua
 
Nimesoma uliandika ukafuta. Kama kwenda secondary sio lazima mwanafunzi apitie la saba, Je Kuna umuhimu gani wa NECTA kutunga mitihani ya darasa la saba (PSLE) kwenda sekondari
Siku hizi ni lazima sababu ya prem number,,but kama mzazi ni mjanja mjanja wa mjini mtoto anaweza akaishia la sita then akaenda sekondari!
 
Hiyo ni.kwa ajili ya kupima wanafunzi wake wanaosoma shule za serikali ndio maana shule ya secondary za private Huwa na mitihani Yao ya mwanafunzi kujiunga kidato Cha kwanza hawategemei hiyo ya kumaliza msingi ya NECTA
Wana iamini ya kwao zaidi

Mtoto hata akiwa darasa la Tano aweza fanya mitihani ya kujiunga kidato Cha kwanza private akifaulu wanamchukua
Sawa mkuu
 
Ikiwa bado hata nusu mwaka wa kalenda 2024 hatujafika na Hata darasa la 7 hawajafanya mitihani. Tayari shule kadhaa binafsi zimeanza kukusanya Ada kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha 1 mwakani (2025). Hii si sawa.
Sasa wewe kama mzazi kwa nini ulipe?
 
Hizo shule zinamilikiwa na watu njaa ambao wanazitegemea hizo shule kuendesha maisha yao, kulipa mikopo ya benki, kula bata, kutunza ndugu na jamaa nk.

Shule zinazomilikiwa na watu wenye uchumi imara haziwezi kutoza ada hivyo.

Fanya utafiti, huwezi kukuta shule ya taasis za kidini zinatoza ada kwa mtindo huo!
 
Ikiwa bado hata nusu mwaka wa kalenda 2024 hatujafika na Hata darasa la 7 hawajafanya mitihani. Tayari shule kadhaa binafsi zimeanza kukusanya Ada kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha 1 mwakani (2025). Hii si sawa.
Simmesema mnatoa darasa la saba inabaki lasita peke
 
Back
Top Bottom