Ikiwa bado hata nusu mwaka wa kalenda 2024 hatujafika na Hata darasa la 7 hawajafanya mitihani. Tayari shule kadhaa binafsi zimeanza kukusanya Ada kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha 1 mwakani (2025). Hii si sawa.
Kama sio sawa, wewe acha kumpeleka mtoto wako hapo...
Elimu iko kwenye soko huru pia. It's a competition..
Kuna shule hapa hapa nchini mojowapo iko Kahama - Shinyanga ikiendeshwa na kusimamiwa na Masista wa Kanisa Katoliki (Shule ya wasichana tu Kidato cha I - IV Boarding) ifikapo mwezi Septemba kila mwaka huwa hawana nafasi za wanafunzi kidato cha I kati ya 200 wanaowahitaji kwa mwaka unaofuata wa masomo..
Kwanini?
Kwa sababu wanatoa elimu bora na usimamizi wa malezi bora na kila mzazi hupenda mtoto wake akasome hapo. Hivyo competition ya kupata nafasi hapo huwa ni kubwa sana kiasi cha kuwahiana tu..
Wao wana Entry Examinations ya kwao. Hawachukui wanafunzi kwa kigezo cha ufaulu wa mtihani wa DRS LA VII. Kila mwaka hupokea applications zaidi 2000 huku nafasi zikiwa ni 200 tu..
Kuna wazazi hupeleka wanafunzi kufanya mitihani hiyo hata kabla ya kufanya mitihani yao ya taifa DRS la VII. Mfano mtihani wa mwaka huu ni mwezi Septemba, wao tayari walishafanya Entry Exam ya kwanza. Ya pili itafanyika mara baada ya mtihani wa DRS la VII mwezi Septemba..
Pesa inayolipwa sasa ni ya English Orientation Course (au Pre Form Course) ya siku 90 (miezi mitatu) ambayo itaanza mwezi October - December. Kiwango hutofoutiana shule na shule..
Generally speaking ni kuwa, there is no problem kwa hiki kinachofanyika sasa so long as mzazi ameridhika kuwa pesa yake haitapotea na mtoto wake atakwenda kupata elimu anayoitaka..
Na kwa shule ambazo zilishajenga credibility ya utoaji elimu, wazazi hatuangalii gharama. Tunachoangalia ni kama uwekezaji wangu kwa mtoto wangu utalipa..