Shule Binafsi ziheshimu likizo za watoto wetu

Shule Binafsi ziheshimu likizo za watoto wetu

Acha uvivu mwalimu,
Tumia muda wako shuleni kumfundisha mtoto, umeajiriwa na kulipwa kwa muda huo.

Wewe ndiye hujui Scheme of work pamoja na Lesson Planning.

Pambaffffff.
Lesson Planning ndio nini? Mambo ya watu usiyoyajua wayakimbilia ya nini?
 
Mwambe bibi yao AJE ,shule zakata zipo wapelekee endapo unataka bibiyao awaone....
 
Imekuwa ni kawaida kwa watoto wanasoma Shule za Binafsi kuwabebesha watoto mafurushi ya kazi za kufanya wakiwa likizo almaarufu Kama HOLIDAY PACKAGES na wakati mwingine watoto wanaendelea kwenda shuleni wakati wa likizo kwa kile kinachoitwa HOLIDAY COACHING. Sasa hizi ni likizo?

Likizo zingeachwa huru ili watoto wawe huru kuwasaidia wazazi wao kazi za nyumbani au kusafiri kwenda kuwasalimia bibi zao huko vijijini ili wafahamu asili yao na pia kujumuika na ndugu zao wengine.

Tungeomba Serikali ilitazame hili jambo na ikiwezekana itoe mwongozo kuhusiana na jili jambo. Tusiwafanye watoto wetu kuwa kama ndondocha, kuna maarifa mengine ambayo watoto wanayahitaji zaidi ya hesabu, fizikia na jiorafia.

Naomba kuwasilisha.
Hiyo shule anayosoma mwanao huwa hamna vikao vya wazazi??

Kama mnavyo huwa mnajadili nini kuhusiana na taaluma za wanenu??
 
Nilipita kwa ccsta nikakuta ametoka kuchukua matokeo ya mwanaye wastani mzuri tu wa A ila ndiyo wamefungana haswa sijui ndiyo mbinu zao ila wameandika eti akasome tuition gharama kilo na upuuzi

Nikamwambia achana na tuition muache mjomba likizo aruke viunzi akili iwe fresh atasoma tu mtoto drs la kwanza tuition ya nini si wizi huo muda wa drsni aliokaa hayo ndiyo mavuno yake sasa likizo ya wiki mbili itasaidia nini nashukuru ameelewa. Muda wa likizo ndiyo muda wa mtoto kucheza aachane na mambo ya shule akili iwaze vitu vingine apige michezo yake ya kukimbizana, kutengeneza magari, kuwinda ndege nk akirudi shule akili safi kbs
 
Ni za lazima kwa kila mtoto au ni hiari kumruhusu mwanao?
 
Yaani unasaidiwa kumfanya mwanao asipoteze content alizojifunza unalalamika Tena?
 
Utampeleka wapi kila kona ni hivyohivyo, hizo shule zinabore sana, ni ujinga mtupu et mtoto wa shule ya msingi asiende likizo ya maana ati ni masomo ya ziada.
unataka kuniambia hujui wapi unataka mwanao awepo????...sio zote mkuu...kwanza elewa shule binafsi ni biashara (service business), so wewe ujivike ualimu,, mwanangu ni lazima awepo likizo nyumbani......mtake msitake.............watakuelewa....
 
Yaani unasaidiwa kumfanya mwanao asipoteze content alizojifunza unalalamika Tena?
Ndo unavyo jidanganya? Kwa hio wali tengeneza mfumo wa Likizo walikuwa mazuzu sana hao walimu ndo wana akili?
 
Nilipita kwa ccsta nikakuta ametoka kuchukua matokeo ya mwanaye wastani mzuri tu wa A ila ndiyo wamefungana haswa sijui ndiyo mbinu zao ila wameandika eti akasome tuition gharama kilo na upuuzi

Nikamwambia achana na tuition muache mjomba likizo aruke viunzi akili iwe fresh atasoma tu mtoto drs la kwanza tuition ya nini si wizi huo muda wa drsni aliokaa hayo ndiyo mavuno yake sasa likizo ya wiki mbili itasaidia nini nashukuru ameelewa. Muda wa likizo ndiyo muda wa mtoto kucheza aachane na mambo ya shule akili iwaze vitu vingine apige michezo yake ya kukimbizana, kutengeneza magari, kuwinda ndege nk akirudi shule akili safi kbs
Nailaumu sana Wizara ya Elimu kuto kuingilia kati huu upuuzi, fikiria unakuta hadi watoto wa Chekechea wanaenda Tuiotion
 
Ndio mkuu, ka kwangu kamesoma tuition mwezi mmoja, teacher alisuggest apate remedial classes
Too sad, mtoto mdogo Tiotion ya nini? Na mzazi unakubali kweli kweli kwamba acha akasome Tuiotion? Aisee labda sio mimi,
 
Unajaribu kushawishi,kwani wakifanya hizo Holiday Packages zinawadhuru nini mkuu?maisha hayajawahi kuwa rahisi hata siku moja...
 
Anzisha shule yako hayo mambo usiyaweke!

Wazazi ni vichwa ngumu sana, kesho mwanao akifeli lawama kwa shule
akipewa shughuli za masomo ili afahulu vizuri napo maneno
Sikiliza wewe mtoto kama hana akili hana tu, hata asome Tuition hizo masaa 24 ni hana tu,

Kwani kufeli kunaanza sasa? Zamani ilikuwaje?
 
Watoto wa shule za serikali wapo wana round tu kwenda shule likizo labda zamu ya usafi😂😂
 
Too sad, mtoto mdogo Tiotion ya nini? Na mzazi unakubali kweli kweli kwamba acha akasome Tuiotion? Aisee labda sio mimi,
Mwenzangu aliona ni sahihi sikutaka kubisha. Ninae mwingine anaingia form five hajawahi kwenda tuition tangu ameanza shule na yupo vzr kupita maelezo. Na bahati nzuri shule alizosoma zilikuwa zinadiscourage tuition, zinasema kabisa hawashauri tuition kwa mtoto ila holiday packages walikuwa wanapewa za kutosha.
 
Hii ni kwa faida ya mwanao
Mtoto sio kama wewe,akiwa nyumbani mchezo ukikolea+vikatuni anasahau kila kitu cha shuleni kiasi kwamba akifika shule inahitaji juhudi za ziada ili aweze kucatch up na ndo mana unapewa hiyo package ili mtoto asisahau sana ya shuleni
It's simple kama hutaki acha chukua hiyo package choma moto as sio kwamba atatakiwa apeleke isahishwe irekodiwe kwenye ripoti yake!
 
Hakuna faida yoyote mkuu, mtoto anatakiwa ku-refresh akili kwa kufanya mambo mengine tofauti na ABC za huko shuleni. Imagine kama wewe unapata likizo then boss anasema uje kazini kila siku, kisa kuna pending issues hakukupa wakati ukiwa ofisini.

Kwani zamani tulisoma vipi, mbona watu walifaulu tu!!
 
Back
Top Bottom