Shule Binafsi ziheshimu likizo za watoto wetu

Ndiyo tatizo la hizi Elimu za kukariri, Walimu wanajuwa Watoto wakienda likizo yote, Watoto watasahau yale yote walio wakaririsha,kwa hiyo inabidi waendelee kuwakaririsha hata kipindi cha likizo! Na upande wa pili Walimu nao wanafaidika na hivyo vimichango vya likizo! Mimi kwenye kikao Cha shule anakosoma mwangu niliwashauri kipindi Cha likizo Watoto wasome kuanzia saa mbili hadi saa tano,masaa matatu yanatosha! Nashukuru Walimu walilifanyia kazi japokua waliongeza lii saa limoja na nusu! Watoto wanaingia saa moja na nusu asubuhi na kutoka saa sita mchana,na kwa siku wanasoma masomo mawili tu!!
 
Hizi ndo watoto wanasoma kwa raha zote za Dunia hakuna hata Homework za kijinga, kila kitu kinaishia shuleni
Hizo shule za international hazina kukariri,ni mwendo wa kusoma na kuelewa!!
 
Holiday package inatolewa kama revision ya kile kilichofundishwa na haihusiani na walimu kutokufundisha mana huwezi toa package sehem ambayo hukufundisha mwanafunzi atajaza nini?
 
Yaani likizo ya wiki 4 watoto wanaendelea kwenda shule kwa wiki 3 halafu watapumzika wiki moja ya mwisho. Unalipa ziada kwa ajili ya hiyo holiday programme halafu wanataka mtoto akakae boarding. Eti watasoma kuanzia alfajiri mpaka saa Tatu usiku ( like seriously?).Sasa basi unalazimika kununua mahitaji ya boarding kwa ajili ya wiki tatu kumbuka na likizo ikiisha unadaiwa ada. Bila kusahau kwamba ulishalipia picnic ambayo walienda siku ya kufunga shule. Jaman hata huruma hawana. Wanalazimisha kutunyang'anya watoto wakiwa bado wadogo na mazingira yenyewe ya boarding hata hayaridhishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe naongea na mtu asiyejua hata Lesson Plannig ni nini.

I am wasting my time
Alitaka umwambie lesson plan, ila hiyo lesson planning ndo kwanza anaisikia kwako. Ndo elimu zetu za madesa, tuvumiliane tu, mheshimiwa mkuu.
 
Tena usiongee kabisa kuhusu sie wa zamani,nakumbukua mimi kwa bibi yangu nilikua sina likizo,nasoma daily nikitoka shule
Huwezi kujifananisha wewe mtu mzima na mtoto ndugu,wewe huwezi sahau majukumu yako ya kazi lakini mtoto ni rahisi kusahau vitu haraka
 
Sikiliza wewe mtoto kama hana akili hana tu, hata asome Tuition hizo masaa 24 ni hana tu,

Kwani kufeli kunaanza sasa? Zamani ilikuwaje?
mkuu anzisha shule yako!

watoto wafeli uone kama utapata wateja
 
Maana za mzazi au mlezi wa mtoto ni kumlinda mtoto dhidi ya dhuluma na unyang'au wa aina yoyote ile. Watoto wa haki ya kupata mapunziko yaliyo kwisha ainishwa na wanasaikologia(na hata ya dharura kama misiba na maradhi), kwamba ni ya lazima kwa kila mtoto kwa mihula yote ya masomo.
 
Hata sisi tulisoma na wakati wa likizo tulikuwa tunacheza.

Shule zikifunguliwa week ya kwanza inakufanya urudi darasani.

Kuna sababu za kuwekwa kwa likizo.

Ila shule za sasa kama kanisa, kulazimisha kupata vipato.
 
Na hizo shule zinazolazimisha watoto waendelee kusoma ndo zinazidi kuwa za mwisho kwenye mitihani mingine.

Shule ya uhakika inakuwa na program nzuri za kueleweka na watoto wanapewa likizo.
 
Wewe ndiye unaujua ukweli.

Wababaishaji watupu hao wamejaa kwenye elimu yetu.

Na hizo shule zinazolazimisha watoto waendelee kusoma ndo zinazidi kuwa za mwisho kwenye mitihani mingine.

Shule ya uhakika inakuwa na program nzuri za kueleweka na watoto wanapewa likizo.
 
Hata sisi tulisoma na wakati wa likizo tulikuwa tunacheza.

Shule zikifunguliwa week ya kwanza inakufanya urudi darasani.

Kuna sababu za kuwekwa kwa likizo.

Ila shule za sasa kama kanisa, kulazimisha kupata vipato.
Mwisho wa siku sio lazima mtoto afanye hayo maswali,kama vipi we mwache mwanao acheze weee,arukeruke,aige vikatuni vyote,ajipikilishe,komborera hapo yani kikubwa uhai!
 
Kama wewe ni mzazi na umepleka mwanao shula na unakuja hapa kulalamika basi kuna shida mahali tena kubwa sana................. halafu wewe ni wale hamna elimu mmepata pesa mnafuata mkumbo wa kuwapeleka watoto shule sio mbaya lakini ukafuata kinachofanywa sio uwe na hisia tuu wewe lazima Elimu uako iko chini sana tuu
 
Anzisha shule yako hayo mambo usiyaweke!

Wazazi ni vichwa ngumu sana, kesho mwanao akifeli lawama kwa shule
akipewa shughuli za masomo ili afahulu vizuri napo maneno
Wwe lazima utakua Mwalimu aliyegeuza Elimu kuwa bishara!!
 
Mwambe bibi yao AJE ,shule zakata zipo wapelekee endapo unataka bibiyao awaone....
Wwe Kama ni Mwalimu pole sana, maana hujui hata kujenga hoja ya Msingi,mjibu mtu kwa hoja,Mipasho ya nini!? eti sijui amwambie Bibi yake,Sasa Bibi yake anaiingiaje hapa!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…