Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Ujenzi wa Shule Mpya ya Makulo, iliyopo katika Kijiji cha Makulo, Kata ya Nkinto, Wilaya ya Mkalama, yenye thamani ya TSh milioni 300.2, umeleta matumaini mapya kwa wananchi wa eneo hilo na unatarajiwa kuondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu.
Awali, wanafunzi wa Kijiji cha Makulo walilazimika kutembea zaidi ya kilomita 10 kufuata elimu katika shule zilizopo maeneo ya mbali, hali iliyokuwa changamoto kubwa kwa wanafunzi hao na wazazi wao.
Kukamilika kwa shule hiyo kumekuwa mkombozi kwa wananchi wa Makulo, kwa kuwawezesha watoto kupata elimu karibu na makazi yao katika mazingira bora, hatua inayofuta.