Mkuu simpo tu kama una chuki nao na unaona hamstahili kupokezana nao uongozi si uwahamishe kama vipi. Au waueni mbaki wenyewe. Ukishajiona wew bora kuliko mwenzio kwa perceptions za utofauti wa dini, wew unakua mpuuzi kuliko yeye.
Nina hakika wew mwenye chuki ya kiasi hiki na Waislamu/Uislamu, ungezaliwa Zanzibar au maeneo hayo unayotaja na wew ungekua Muislamu pia. Ndio maana mijadala wa tofauti za imani wa ipi bora ni relative na haitakuwa hata siku moja watu wakaamini sawa.
Utofauti wa kila kitu duniani ndio umeleta maana halisi ya maisha. Wewe unaowatukana Waislamu, unafanya hivyo kwa vile umezaliwa jamii tofauti. Watu wachache sana wanaamua imani zao baada ya kuwa watu wazima, wengi hurithi toka kwa wazazi.
Acha kashfa mana haitawaondoa hao usiowependa na pia na wao wana haki ya kuongoza taifa hili kama nyie wenye akili!
Mungu akusaidie kubaini utofauti wetu wa kila hali ndio unakamlisha maana ya maisha. Lakin pia hamna namna yoyote Muislamu/Mkristo anaweza mfuta mwenzie katika nchi hii. We will always co-exist, na hamna atakaeshinda akimbagua mwenzie.