Shule nyingi zinazoitwa English Medium ni za kisanii tupu

Wengi wanalipa kati ya 1.5m up to 2M tena kwa installment 4 na mtoto anaenda kwa daladala bila school bus 😁 😁 😁 😁 , hata hiyo 3M wachache sana wanalipa.
 
Umeandika point tupu,

Tatizo ni umaskini wa kipato mkuu

Nataman sn wanangu wasome international

Huu mtaala wa NECTA bado sn
Unampima mtt uwezo wa kukariri na sio kuelewa concept
 
Basi kila mtu ajipimie pale anapoweza.Mimi bora nijipimie hii ya 1000 kuliko ile ya BURE.
BURE GHALI SANA
 
English medium kazi yake ni kukaririsha watoto siku nzima
Hakuna michezo
Tafuta ada ya milioni 18 kwa mwaka upeleke mwanao International School tupumuzike kelele zako humu

Hakuna asiyependa kizuri suala ni uwezo

Ukiwa na watoto wawili ada International School milioni 36 kwa mwaka minimum
Wewe mwenyewe huo uwezo unao? Au unatuletea kelele tu humu
 
Tatizo umekariri kama kuinamishwa
 
Watu wanamzodoa mtoa mada lakini ana haki ya kusikilizwa sio kubezwa ila sio vibaya mtu kutoa maoni yake

Kwa upande wangu hebu tuache kuongelea International school kwanza maana kwa upande wangu ni sawa na kujadili kumpa samaki mtihani wa kupanda juu ya mti.Au kuweka mzania kujilinganisha na mtu mwenye range rover wakati wewe una IST.

Mimi kiuhalisia nilisoma enzi za Nyerere mtaala ni mmoja nchi nzima hata watoto wa wakubwa tulikuwa tunasoma nao moja wapo,watoto wa Nyerere,watoto wa Malecela Marehemu Mwele na kaka yake Le Mutuz RIP na marehemu Mhe sana Magufuli japo alikuwa mbele yetu kidogo.Wote waliokuwa wanasoma International ni watu wa jamii ya Asia matajiri na watu wa mataifa ya nje iko shule moja st Constantine iko Arusha wanafunzi walikuwa wanadekezwa mno hata kufua walikuwa hawajui na kuchapwa ilikuwa marufuku.Field walikuwa wanakwenda Ugiriki wakati mwingine Nairobi Kenya.Hawa kwa sasa ada unaweza nunua gari la nguvu

Sasa huko tuache sio kwetu tulio wengi.Hebu turudi kwetu tulio wengi kunakonoga
Tuje hizi shule za English medium na shule mlizobatiza saint Kayumba kiukweli hata mimi nachanganyikiwa naona nchi yetu ilikosea toka mwanzo shauri ya kuweka siasa mbele ukweli ulio wazi Kingereza ndio kiswahili cha dunia Kiswahili ni lugha ya nyumbani.

Mimi sizifagilii sana hizi shule za English medium ila kinachofanya nipeleke watoto wangu English medium ni hali ilivyo sasa hivi Unakuta darasa moja wanafunzi wako 200 hadi mwalimu hajui majina ya wanafunzi wake hadi mwanafunzi amsalimie barabarani anamuambia unanifundisha.

Wanafunzi wanasomea chini hakuna madeksi.Kuna mtoto wa dada yangu siku moja nilimpa homework nyumbani cha ajabu akatoka kwenye meza akawa anajibu akiwa chini sakafuni niliumia sana nikajua kuwa ni sababu hakuzoea meza anajua meza kazi yake ni kulia chakula.
Walimu wamekata tamaa mishahara midogo hakuna ongezeko wala hakuna kitu kinaitwa muda wa ziada wa kazi alipwe yaani overtime.
Walimu ari ya kufundisha imepotea wanakopa kwenye vikoba na kufanya biashara zingine.

Mimi pamoja na kusoma enzi ya Nyerere lakini darasani deksi moja tulikuwa tunakaa wanafunzi watatu na darasa moja tulikuwa hatuzidi 25.

Kwa niliyoeleza hapo juu vihela vyangu pamoja na yote lazima nitampeleka mtoto wangu English medium kumuonea huruma asije ota kibiongo.Yuko mmoja anasema ada ya English medium ni shs 3m ukweli sawa zipo lakini mimi nalipa pungufu ya hapa chini ya hiyo kwa mwaka mzima sitashindwa kumsomesha mwanangu au kwa sasa nasema wajukuu zangu.
 
Cc: MAMA, WAZIRI WA ELIMU.
 
Nimeoba malalamiko tu toa na suruhisho kabisa.....
 
English medium kazi yake ni kukaririsha watoto siku nzima
Hakuna michezo
Kuna ka ukweli Fulani.

Lastborn wetu Alisoma hizo shule nilikuwa namtest ielewa wake aisee amekariri Kila kitu hadi nikajiona hadi Mimi enzi zangu nikiwa primary St kayumba nilikuwa kilaza tu.

Yuko standard seven analeta Pepa za maths kalamba 50/50.

Alifaulu special school Moja wapo ya wasichana kati ya zile tatu.

Huko Nako analiendeleza libeneke top ten hakosekani.

Ila hapendi michezo kabisa sio mpira w Pete Wala Nini yeye ni muziki kudance dance kama wale madancer wa marioo[emoji1]

Tukawa tumwambia utaishia kuwa dancer wa bendi za muziki[emoji1][emoji1787]
 
Umemaliza mkuu,
 
Kuna Moja inaitwa fortune IPO kinyerezi. Nilimtoa mtoto haraka sana. Watoto wamejaa, mkurugenzi anajali pesa, anadai ada on time hata ruba mnyonya damu ananafuu, walimu wakuunga UNGA cheap labor.

Watoto elfu hata shule ya kata ina afadhari. Baada ya kuona pesa amebadilika huduma duni.

Mleta hoja umeona mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…