Shule nyingi zinazoitwa English Medium ni za kisanii tupu

Vipaji vinaibukia huko
Ahahah ni kwel nilikua namzingua tu huyo HIMARS .. kwa mtoto michezo ni crucial.wengi tulikua tunapenda shule kipaumbele ni vile kucheza cheza kisha masomo yanafuata namba 2.So kadiri unakua ndio priorities zina shift sasa elimu inakua namba moja na wengine wanaendeleza vipaji..
 
Lkn mkuu shule ada 2Mil watoto 1000. Kwa mwaka ninoesa ndg?
 
kuna english medium zipo watoto wanafundishwa hadi ufugaji, nidhamu n.k, wazazi tumekuwa wapumbavu kupindukia, hatufanyi utafiti, hatufatilii, tumejikita kutafuta pesa tu masaa 24 na kuwaachia walimu watulelee watoto. Pumbavu kabisa.
 
Kweli na ndo tunapokosea
 
Nadhani kuanzia mil 20 hiv ila kama ist inaenda mpaka milioni 70
Asante!!! I was just being sarcastic maana mtoa mada anataka huduma za gharama ya juu zitolewe sawasawa na huduma za gharama ya kati/chini.
 
Tutoe ushamba mkuu,namna gani ya kutambua shule bora,yenye standards bora na yenye walimu mahiri?
 
Ndugu BLACK MOVEMENT ni kweli international school inatoa elimu bora ila umechemsha kushindwa kutofautisha gharama za international schools na hizo English medium schools. Elewa hizo English medium schools zinafuata mitaala ya NECTA ambapo lugha tu ndo zinazitofautisha na hizi St Kayumba. Kwangu mimi bora English medium schools kuliko St Kayumba. Mtoto kujua kiingereza vizuri kabla ya kumaliza la saba ni ushindi mkubwa. Iwe hata kwa kukariri cha muhimu ni kuwa anatema yai. Hizi St Kayumba ni majanga matupu sema tu hali ya kiuchumi ni ngumu ila wengi wangepeleka watoto English medium schools kuliko Kayumba. Ungekuwa na hela ungempeleka mtoto Ngarenaro Primary School au St Patrick School?
 
Ni usanii kweli kuwaridhisha wazazi wajinga na wazungu.Kiswahili ndio lugha inayotawala kila sehemu hapa kwetu.
 
Tatizo ada za International ni kubwa
Ni kweli mfano International School of Tanganyika ada ya chekechea kwa mwaka mmoja ni shilingi milioni 31 kwa mwaka

Ada hizo hapo

Finances: For the 2022-2023 school year, the annual tuition fees are as follows: early childhood 1-2: $16,100; kindergarten-grade 5: $23,500; grades 6-8: $27,300; grades 9-10: $28,900; and grades 11-12: $33,300. There is also a $1,000 annual capital
fee per child.

Ukiambiwa Tanzania ni.mojawapo ya nchi.maskini sio utani.Watanzania wangapi waweza mudu hizo ada?
 
Ana hoja huyu asikilizwe vzr hapa mwishoni.
Kimsingi huyu hoja hana, yeye ni kama Lema mwenye kutoa mifano ya Kanada na Marekani akisahau kuwa yuko Tanzania.
Kwanza ajue kwanini shule iitwe International na nyingine iitwe English medium. Hoja yake ianze hapo.
Akirudi, hoja yangu nitaiendeleza.
 
Nakupa 5. Hapo umeingia katika hoja nzuri. Yule muandika Thread aje atuambie mfuko wake upoje? Ni watanzania wangapi wataweza kulipa ada hiyo. Ndugu zanguni msiwe akina Lema mnaofikiri tunaishi Kanada na Marekani.
 
Ni usanii kweli kuwaridhisha wazazi wajinga na wazungu.Kiswahili ndio lugha inayotawala kila sehemu hapa kwetu.
Hizi akili zijuathiri wewe tu jitahidi zisije muharibia mtoto wako pia unajua matumizi ya kiingereza kwenye interview na kazini wejamaa.

Kila tangazo la Ajira lina kipengere uww Fluent in English
 
Ok. Waziri wa elimu aichukue hii na kuifanyia kazi. Tunataka mwaka kesho shule zote za Tanzania ziwe international. Na huo mtaala wenu mpya wa elimu feki pelekeni kule zanzibar, sisi tunaka mtalaa wa Cambridge
Angalia kwanza mfuko wako kabla hujaamua ni hoteli gani ukale Lunch. Vizuri tunavipenda wote, lakini vizuri na bei zake ziko vizuri. Unachangia hoja kwa namna hiyo wakati utakuta mwanao hata shule ya kata umeshindwa kumlipia.
Waziri wa elimu atacheka tu akisoma ushauri wako. Soma nukuu hapa chini!

Nukuu toka kwa YEHODAYA "Ada hizo hapo
Finances: For the 2022-2023 school year, the annual tuition fees are as follows: early childhood 1-2: $16,100; kindergarten-grade 5: $23,500; grades 6-8: $27,300; grades 9-10: $28,900; and grades 11-12: $33,300. There is also a $1,000 annual capital
fee per child"
 
Umemaliza kila kitu,shida sio kwamba hatuzijui hizo shulee shida ni kwamba mifuko yetu wazazi imeishia English Medium, lakini pesa ilivyo ingekuwepo hata hiyo Tanganyika School tusingepeleka watoto zetu.

Kuna shule nyingi kali hizi international za hapa Bongo zinasubiri nyuma,shida ni 1 tu Tunajikuna mkono unapofikia mambo mengine tunapambana hata kama sisi tumeshindwa wasomesha watoto zetu international schools

basi wao wasije kuwa kama sisi,yani watoto wetu waweze wasomesha watoto zao (wajukuu zetu) hizo international schools.

ila kudananyana internatinal school ni ADA tu,ni uongo kule watoto hawaendi TRIP serengeti,wanaweza pelekwa TRIP U.K huko,sasa mimi naweza jikakamua mwanangu akapata ADA hizo unseen cost za hapa na pale zikija ntaziweza?

Hubu tuachwe kidogo,Acha akaririshwe english mengine ntakuja mfundisha nyumbani kwanza elimu anaitoa mzazi mashuleni wanaenda kuondoa Ujinga tu na kuwekwa katika utaratbu wa dunia.

isingekua mambo ya ELIMU,VYETI,nk mwanangu ningemtafutia mwalimu private wa kila somo Ajue kusoma,kuandika kuhesabu,Maarifa mengine yote ntajua namuwekeaje..maana kuna ma elimu mengine yanapatkana mashuleni ni useless useless.
 
Basi mkuu peleka st. Kayumba ama IST and the other international schools
 
Ukifuatilia sera ya shule inatakiwa iwe na kiwanja.
Vipindi vya michezo lazima.

Mfano tuliosoma Loyola Kila Ijumaa mkitoka class ilikuwa michezo hadi jioni

Siku hizi shule zaanzishwa ila hakuna viwanja kabisa

Shule za International, unawakuta wanaenda ogelea, music club, computer club, running, football.
 
Niache nunua GARI,niache kujenga Niende kutoa mihela yote hiyo kisa elimu kwa level niliyonayo ni uongo!

ninachoweza ni kuandaa mazingira ya wajukuu zangu kuweza kusoma hizo shule,maana income ya mzazi anaesomesha mtoto hizo shule si chini ya 100m per month, ni mtu anae ingiza sio chini ya 5m kama Faida per day.

Ameshakula
Amesha spend
Ameshatoa matumizi yote

kwa siku anaweka akiba ya 5m bank,huyo ndio anaeweza afford hizo shule,ila sio sisi wa 5m tunaitafuta mwezi mzima,hizo hazitufai tuna afford English Medium (kayumba zilizochangamka)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…