KERO Shule ya Bungo Mlimani ni changamoto, wanafunzi wanachelewa kutoka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Kuna shule ipo Morogoro mjini inaitwa shule ya msingi Bungo Mlimani.

Hii shule ni kipengele sana yaani mtoto wa darasa la pili anatoka nyumbani saa kumi na mbili asubuhi anarudi nyumbani saa kumi na Moja jioni, akiwahi sana ni saa kumi jioni. Hapa mtoto anateseka sana kuanzia njaa plus uchovu, pia Kuna risky kubwa ya watoto kupotea maana wanarudi muda umeenda sana wakati mwingine mvua kubwa zinanyesha.

Ratiba ya mtoto wa darasa la pili kutoka darasani kurudi nyumbani kachelewa sana saa saba na nusu.

Kwa wenye taaluma hii mje hapa msaidie jamvi, je hii ni sawa? Na taratibu gani itumike kisheria kumdhibiti mwalimu huyu anayewatesa watoto kiafya.

Nasubiria ushauri ulio thabiti.
Najua wenye sekta hii mpo humu ndaniπŸ™πŸ½
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…