KERO Shule ya Bungo Mlimani ni changamoto, wanafunzi wanachelewa kutoka

KERO Shule ya Bungo Mlimani ni changamoto, wanafunzi wanachelewa kutoka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Aise ata kama wee unaishi mbinguni lakini sio kwa kutukosea hivyo wanamorogoro.
Wee hapa tuna vyuo, sgr inakatiza hapa, king of the road mwenyewe yupo na tuna nyumbani lounge totoz zote unapata pale hadi wale wagawa visoda wakiume.
Moro ndio home wewe
Hahahah nisameheni wakuu
 
Kuna shule ipo Morogoro mjini inaitwa shule ya msingi Bungo Mlimani.

Hii shule ni kipengele sana yaani mtoto wa darasa la pili anatoka nyumbani saa kumi na mbili asubuhi anarudi nyumbani saa kumi na Moja jioni, akiwahi sana ni saa kumi jioni. Hapa mtoto anateseka sana kuanzia njaa plus uchovu, pia Kuna risky kubwa ya watoto kupotea maana wanarudi muda umeenda sana wakati mwingine mvua kubwa zinanyesha.

Ratiba ya mtoto wa darasa la pili kutoka darasani kurudi nyumbani kachelewa sana saa saba na nusu.

Kwa wenye taaluma hii mje hapa msaidie jamvi, je hii ni sawa? Na taratibu gani itumike kisheria kumdhibiti mwalimu huyu anayewatesa watoto kiafya.

Nasubiria ushauri ulio thabiti.
Najua wenye sekta hii mpo humu ndani🙏🏽
Mkuu,nenda hapo ofisini onana na mwalimu,unakwama wapi?
Wahi kabla watoto hawajapata shida zaidi
 
Mkuu,nenda hapo ofisini onana na mwalimu,unakwama wapi?
Wahi kabla watoto hawajapata shida zaidi
Uyu mwalimu n wazaz wamemchoka nataka Kuonana na mwalimu wake mkuu alafu niskie atajibuje Kisha nione atua ya kuchukua
 
Wewe sasa ndio umekurupuka 😂😂😂 uyu mwalimu ana jifanya ni kichwa kibovu hamsikilizi ata mkuu wake wa shule ambae ndio boss wake je atamsikiliza mzazi?,pili kuusu no apo Umepuyanga mkuu😂😂 Nina no za viongozi wote wa mkoa morogoro mjini Kwa vijijini ila kabla ya Yote nimeomba ushauri apa pia najua Kuna watu wa sekta iyo wapo umu (wizara ya elimu) ivyo kama mada haikuusu pita kushoto mkuu🙏🏽
Sasa kama una namba za viongozi, kwa nini usiwapigie ukatoa malalamiko yako?
 
Ngoja waje st kayumba wajadili vizuri kupinga ems huku wakisahau mateso ya watoto wao na ratiba ngumu
 
He
Acha wasome ili watoe ujinga na wasiwe kama wale wajinga wasiotofautisha L na R waliojaa ugali kichwani kiasi cha kuandika "wai" badala ya "wahi".hela wanaandika ela,jiuzulu waandika jiuzulu,kuna mmoja yuko Arusha,kura anatamka kula.
 
Kuna shule ipo Morogoro mjini inaitwa shule ya msingi Bungo Mlimani.

Hii shule ni kipengele sana yaani mtoto wa darasa la pili anatoka nyumbani saa kumi na mbili asubuhi anarudi nyumbani saa kumi na Moja jioni, akiwahi sana ni saa kumi jioni. Hapa mtoto anateseka sana kuanzia njaa plus uchovu, pia Kuna risky kubwa ya watoto kupotea maana wanarudi muda umeenda sana wakati mwingine mvua kubwa zinanyesha.

Ratiba ya mtoto wa darasa la pili kutoka darasani kurudi nyumbani kachelewa sana saa saba na nusu.

Kwa wenye taaluma hii mje hapa msaidie jamvi, je hii ni sawa? Na taratibu gani itumike kisheria kumdhibiti mwalimu huyu anayewatesa watoto kiafya.

Nasubiria ushauri ulio thabiti.
Najua wenye sekta hii mpo humu ndani🙏🏽

Usikose kuja kuwasilisha hoja yako kwenye kikao kijacho cha wazazi.
 
Shule za vijijini huwa wanarudi huo mda, ila shule wanaenda saa 5, wanapishana na drs la 1.

Hata mimi, kijijini tulikuwa tuna swap. Tunaingia saa 2 tunatoka 5 wengine wakiingia muda huo, wanatoka saa 8
 
Kuna wengine wameibuka wanaongeza h mbele mfano:-
Ameamka=hameamka
Anakuja=hanakuja
Amenipa=hamenipa
Hawa wenzetu sijui wameishia darasa la ngapi?

Hao ni wahaya. Hata kabila lao wanaloita wa'aya. Wanashindwa kitamka ha.
 
Uyu mwalimu n wazaz wamemchoka nataka Kuonana na mwalimu wake mkuu alafu niskie atajibuje Kisha nione atua ya kuchukua

Hudhurieni vikao vya wazazi ni muhimu. Mambo yote kama haya, huishia huko
 
Back
Top Bottom