KERO Shule ya Bungo Mlimani ni changamoto, wanafunzi wanachelewa kutoka

KERO Shule ya Bungo Mlimani ni changamoto, wanafunzi wanachelewa kutoka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mkuu mtoto wa la 2 atoke nyumbani ahsubuhi arudi sa 11 jioni ikiwa hata wa darasa la sita anarudi saa kumi upo serious?
Nilijikita kumrekebisha mtoa taarifa badala ya kujibu hoja kwani alikuwa ameandika vitu vya kuumiza kichwa. Karekebisha tayari na taarifa imekaa vizuri.

Kwa tatizo hilo ni vyema wakaongea na uongozi wa shule hiyo kwa ufumbuzi wa tatizo.
 
Turudi kwenye mada kwanza hii shule inaitwa Mlimani primary, kwanini usiwapeleke Towelo shule ya msingi km kwako ni mbali na hapo Mlimani. Enzi zetu sisi tulisoma na watu wengi wa Milimani kule pale Mjimkuu primary. Magical power
 
Kuna shule ipo Morogoro mjini inaitwa shule ya msingi Bungo Mlimani.

Hii shule ni kipengele sana yaani mtoto wa darasa la pili anatoka nyumbani saa kumi na mbili asubuhi anarudi nyumbani saa kumi na Moja jioni, akiwahi sana ni saa kumi jioni. Hapa mtoto anateseka sana kuanzia njaa plus uchovu, pia Kuna risky kubwa ya watoto kupotea maana wanarudi muda umeenda sana wakati mwingine mvua kubwa zinanyesha.

Ratiba ya mtoto wa darasa la pili kutoka darasani kurudi nyumbani kachelewa sana saa saba na nusu.

Kwa wenye taaluma hii mje hapa msaidie jamvi, je hii ni sawa? Na taratibu gani itumike kisheria kumdhibiti mwalimu huyu anayewatesa watoto kiafya.

Nasubiria ushauri ulio thabiti.
Najua wenye sekta hii mpo humu ndani🙏🏽
Oya nipe tender ya kumpeleka na kumrudisha mwanao....
 
Morogoro sio sehemu ya kuishi hiyo ni Parking ya Abood
Aise ata kama wee unaishi mbinguni lakini sio kwa kutukosea hivyo wanamorogoro.
Wee hapa tuna vyuo, sgr inakatiza hapa, king of the road mwenyewe yupo na tuna nyumbani lounge totoz zote unapata pale hadi wale wagawa visoda wakiume.
Moro ndio home wewe
 
Bungo bila shaka ipo kando ya ile barabara ya kwenda flat za kingaru au shule ya forest nadhani kuna nyingine jirani sijui inaitwa mchikichini
 
Bungo bila shaka ipo kando ya ile barabara ya kwenda flat za kingaru au shule ya forest nadhani kuna nyingine jirani sijui inaitwa mchikichini
Mchikini ipi chini pamoja na bungo,ila bungo primary ipo shule ya forest secondary Kwa juu kidogo
 
Kuna shule ipo Morogoro mjini inaitwa shule ya msingi Bungo Mlimani.

Hii shule ni kipengele sana yaani mtoto wa darasa la pili anatoka nyumbani saa kumi na mbili asubuhi anarudi nyumbani saa kumi na Moja jioni, akiwahi sana ni saa kumi jioni. Hapa mtoto anateseka sana kuanzia njaa plus uchovu, pia Kuna risky kubwa ya watoto kupotea maana wanarudi muda umeenda sana wakati mwingine mvua kubwa zinanyesha.

Ratiba ya mtoto wa darasa la pili kutoka darasani kurudi nyumbani kachelewa sana saa saba na nusu.

Kwa wenye taaluma hii mje hapa msaidie jamvi, je hii ni sawa? Na taratibu gani itumike kisheria kumdhibiti mwalimu huyu anayewatesa watoto kiafya.

Nasubiria ushauri ulio thabiti.
Najua wenye sekta hii mpo humu ndani🙏🏽
Tatizo hilo hata Dar. lipo.
 
Dar ndio kuna maajabu nilishawahi kusubiri bus saa 2 usiku na watoto wa shule pale stendi mnazi.mmoja
 
Unachokifanya hapa ndiyo sababu ya elimu kuzorota kila siku.

Suala la elimu ni pembetatu; mzazi, mwanafunzi, mwalimu.

Wewe kama mzazi wa mwanafunzi, unatakiwa kuwa na mawasiliano na mwalimu wake. Muulize akujuze sababu. Na pia, hudhuria kwenye vikao vya walimu na wanafunzi ili upeleke malalamiko yako huko mjadili pamoja na wazazi wenzako.

Unakurupukia huku. Inaonesha huna hata namba ya mwalimu wa darasa analosoma mwanao.
 
Wewe sasa ndio umekurupuka 😂😂😂 uyu mwalimu ana jifanya ni kichwa kibovu hamsikilizi ata mkuu wake wa shule ambae ndio boss wake je atamsikiliza mzazi?,pili kuusu no apo Umepuyanga mkuu😂😂 Nina no za viongozi wote wa mkoa morogoro mjini Kwa vijijini ila kabla ya Yote nimeomba ushauri apa pia najua Kuna watu wa sekta iyo wapo umu (wizara ya elimu) ivyo kama mada haikuusu pita kushoto mkuu🙏🏽
 
Back
Top Bottom