DOKEZO Shule ya Kibaigwa Girls imekataa kumpokea Mtoto wangu sababu sijamaliza Hela za Michango

DOKEZO Shule ya Kibaigwa Girls imekataa kumpokea Mtoto wangu sababu sijamaliza Hela za Michango

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
ndoo 1-2,000/= fangio 1-1,000/= na mopper 1-3,500/=

Inabidi utoe tu hiyo 6,500/= sasa ukikataa nani akufanyie usafi? Serekali yenyewe ndo hii kama mambo muhimu kama huduma za afya unaweza kufa kwa kukosa buku 5 unategemea vifaa vya usafi watatoa?
Msameheni aisee [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mleta uzi sikutetei ila huyo mkuu wa shule kama ni dada mmoja hivi mfupi na amehamia HAPO mwaka juzi basi inawezekana malalamiko yako yana ukweli maana ana kashfa ya upigaji hata huko alikotoka ngoja niishie hapa mamlaka zake zitafwatilia.
 
Mkuu sio fagio tu,kumpeleka mtoto advance ili apokelewe vitu walivyoorodhesha at least uwe na laki nne ndio pesa ya chini kabisa
Heb share hivo vitu vinavyofika laki nne,
Wote tumesoma siku hizi, wew peleka michango mtoto apokelewe, kwa hio unataka vyoo vya mtoto wako visafishwe kwa fagio ya nani?
 
Kwahiyo huku ndipo utapata muafaka au utamuharibia masomo mwanao?!

Wewe jamaa wa Ntwara tumia ubongo kufikiria.
 
Heb share hivo vitu vinavyofika laki nne,
Wote tumesoma siku hizi, wew peleka michango mtoto apokelewe, kwa hio unataka vyoo vya mtoto wako visafishwe kwa fagio ya nani?
Japo umeniquote kipumbavu ngoja nikujibu tu kistaarabu,mchango wa shule aufiki hata laki 1,vitu anavyotakiwa mtoto kuripoti navyo ndio gharama,vitabu tu vinakaribia laki 2,uniform,nguo za kushindia,godoro,vitendea kazi n.k,japo ni jukumu la mzazi ila uwezo watu wametofautiana sioni haja kuanza kumbully huyo mzazi ambae mwanae amekataliwa kupokelewa
 
Wazazi wa siku hizi wanashangaza,zamani mtoto alikuwa akifaulu unaweza uza mpaka shamba maana gharama zilikuwepo na michango ilikuwa mingi,sasa hivi mambo yamekuwa rahisi ila malalamiko yanazidi.
Pole kwa changamoto

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Mtoto wako alikuandikia barua umzae? Acha kusumbua waalimu. Lipa ada na michango yote unayodaiwa. Elimu ni gharama. Halafu unawezaje kutoka Mtwara hadi Dodoma huku ukijua hujakamilisha michango? Hiyo shule ni ya ukoo wenu kwamba utapokelewa? Kila siku tunalalamika kuburuzwa na watawala halafu hapohapo hatutaki kusomesha watoto...!! Mleta uzi acha upuuzi.
 
Nyie UVCCM ungeserema mwingi sana.
Unahisi watu wote wanafanana kipato au Kila siku inakuwa kama Jana?
Acheni ujuaji mwingi nyie watoto.
Kwanini kukawepo Kaya zinazohudumiwa na miradi ya TASAF?
Unafikiri huko serikalini wangewaza kama ninyi mifuko hiyo ingekuwepo?
Zamani walikuwepo wanaolipiwa na halmashauri pia sababu walijua changamoto kama hizi.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Japo umeniquote kipumbavu ngoja nikujibu tu kistaarabu,mchango wa shule aufiki hata laki 1,vitu anavyotakiwa mtoto kuripoti navyo ndio gharama,vitabu tu vinakaribia laki 2,uniform,nguo za kushindia,godoro,vitendea kazi n.k,japo ni jukumu la mzazi ila uwezo watu wametofautiana sioni haja kuanza kumbully huyo mzazi ambae mwanae amekataliwa kupokelewa
Awali naomba unisamehe kama unahisi nimekuquote kipumbavu,
Ila mkuu tukija kwenye mada,
Mzazi kama hela haitoshi basi angalia priorities, vitu vya lazima na visivyo vya lazima,
Kama hujakamilisha michango, why ulipe 50,000/- kununua chand? Au Bios? Kwa hio utaona either hakuweka priorities zake vema,
Michango ya Advance ni michache, akomae alipe, shule ziendelee
 
Nyie UVCCM ungeserema mwingi sana.
Unahisi watu wote wanafanana kipato au Kila siku inakuwa kama Jana?
Acheni ujuaji mwingi nyie watoto.
Kwanini kukawepo Kaya zinazohudumiwa na miradi ya TASAF?
Unafikiri huko serikalini wangewaza kama ninyi mifuko hiyo ingekuwepo?
Zamani walikuwepo wanaolipiwa na halmashauri pia sababu walijua changamoto kama hizi.
Nitolee upuuzi hapa. Mimi sio UVCCM na pia nilisoma wakati elimu haikuwa bure. Nimesoma shule hadi chuo kikuu cha serikali na mkopo nilipata 100% kutokana na kutoka familia ya kawaida sana. Ninachoongea nina uhakika nacho. Watu wanakwepa majukumu yao kifala. Hakuna haja ya kubembeleza.
 
Una uhakika wa nini? Uhakika kwenye kipato cha watu wengine?
You are very inconsiderate person.
 
Habari Watanzania,

Nawasalimu kwa jina la muungano..

Nina kero yangu haswa kwa shule za advance wanaopokea kidato cha tano Walimu wakuu wanachukua maamuzi ya kukataa kumpokea Mtoto ikiwa tu hajamaliza michango na vifaa vingine kama vile vya usafi ukiangalia umbali uliotoka na Mtoto ni mbali sana.

Mfano mimi mwanangu kapangiwa Kibaigwa Girls iliyopo Dodoma, Mwalimu mkuu na makamo Mkuu wa shule wamenigomea kumpokea Mtoto kisa nimelipia nusu ya pesa za michango na sijakamilisha vifaa vya usafi ukizingatia nimetokea mkoa wa Mtwara

Sijui cha kufanya, naomba waziri husika kufuatilia hili jambo, wazazi tunashindwa kuwapeleka shule mapema watoto kutokana na hizi changamoti.

Naomba kuwasilisha

🤝
Hauna connection ya Mpwayungu Village? Mtafute huyo, atakusaidia.
 
Back
Top Bottom