DOKEZO Shule ya Kibaigwa Girls imekataa kumpokea Mtoto wangu sababu sijamaliza Hela za Michango

DOKEZO Shule ya Kibaigwa Girls imekataa kumpokea Mtoto wangu sababu sijamaliza Hela za Michango

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nyie UVCCM ungeserema mwingi sana.
Unahisi watu wote wanafanana kipato au Kila siku inakuwa kama Jana?
Acheni ujuaji mwingi nyie watoto.
Kwanini kukawepo Kaya zinazohudumiwa na miradi ya TASAF?
Unafikiri huko serikalini wangewaza kama ninyi mifuko hiyo ingekuwepo?
Zamani walikuwepo wanaolipiwa na halmashauri pia sababu walijua changamoto kama hizi.
Sasa kama hana hela si aombe msaada serikalini au kwingineko sio kulaumu shule haijapokea mwanae, shule ina haki ya kutopokea mwanafunzi ambaye hajakidhi vigezo
 
Nadhani kinacholeta mtanziko hapa ni serikali kuhubiri elimu bure mpaka form 6 halafu pia jamani kuna watanzania bado ni maskini lazima hii hoja ya mkuu ipewe mashiko
Wewe umasikini wako unaihusu vipi utaratibu wa shule? Sort kwanza tatizo la hiyo michango ndio umpeleke shule
Ama kila mtu atakuwa anasingizia umaskini
 
Uongozi wa shule umeshindwa kuweka utaratibu wa malipo kufanyika kwa awamu? Kwa nini wanakataa kumpokea mwanafunzi?
Miaka tunasoma unapokwenda likizo utaandikiwa mahitaji unayotakiwa kuja nayo...mfano matibabu kila mtu 10000,ukirudi shule bila hiyo elfu 10,hata kama kwenu umbali ni km 1400,utarudishwa ulete hiyo pesa,hata kama umelipa ada...huyu mzazi alipata Joining letter ambayo imeorozeshwa kila hitaji...mtoto unampeleka hujakamilisha unataka huruma humu,...yunatengeneza kizazi kizembe kisichopenda kuwajibika...na ndio maana tunasema Elimu shule za serikali ni duni kwa sababu wazazi hawataki kuwajibika,unataka serikali ikufanyie kila kitu...tumepita kwenye michakato ya Elimu na tunajua kama unataka kupata kilicho bora lazima mzazi+mwanafunzi mpambane...nina mifano mingi ya vijana leo wako kwenye position kubwa,lkn wametoka kwenye hali duni mno,...wazazi na wanafunzi walipambana....huyu mzazi aache kulia lia,somesha mwanao aje akushukuru baadae.
 
Unajua nchi zilizoendelea na zenye elimu bora inayoendesha hii dunia, wanafunzi hawafuti hata vumbi katika viti vyako, wachilia kuleta fagio? Elimu (rahisi sana) ni nini kwa mtazamo wako?
Huko wananchi wake wanafanya kazi na kulipa kodi, Tz hata kodi hawataki kulipa wanadai ni wanyonge
 
Habari Watanzania,

Nawasalimu kwa jina la muungano..

Nina kero yangu haswa kwa shule za advance wanaopokea kidato cha tano Walimu wakuu wanachukua maamuzi ya kukataa kumpokea Mtoto ikiwa tu hajamaliza michango na vifaa vingine kama vile vya usafi ukiangalia umbali uliotoka na Mtoto ni mbali sana.

Mfano mimi mwanangu kapangiwa Kibaigwa Girls iliyopo Dodoma, Mwalimu mkuu na makamo Mkuu wa shule wamenigomea kumpokea Mtoto kisa nimelipia nusu ya pesa za michango na sijakamilisha vifaa vya usafi ukizingatia nimetokea mkoa wa Mtwara

Sijui cha kufanya, naomba waziri husika kufuatilia hili jambo, wazazi tunashindwa kuwapeleka shule mapema watoto kutokana na hizi changamoti.

Naomba kuwasilisha

🤝
Sasa si umalize tu michango .....?
 
Na muda unamsubiri yeye tu au huoni changamoto licha ya kueleza bayana umbali anakotoka hivyo kuna gharama nyingi tu mpaka afike shuleni? Kwa uchumi gani wa MTz wa kawaida?
Umeelewa hata nilichoandika?
 
Serikali inawadekeza sana nyie wazazi hili nalo ni la kuomba msaada kutoka kwa waziri
 
Umeelewa hata nilichoandika?
Kwamba ' kwa nini asingeomba uongozi wa shule, akamilishe Ada halafu ndio aende shule'. Wakati huo wenzake hawafundishwi wanamsubiri yeye ama?
 
Kwanza imekuaje Mwanao Kapangwa Dodoma na ametoka Mtwara?

Nijuavyo kuanzia mwaka huu, ili kuepuka usumbufu serikali inampanga mwanafunzi kwenye kanda aliyosomea O-level na hilo limefanyika kweli...

Kuna kanda Ya ziwa, Kanda ya kati, kusini, kaskazini Pwani n.k,
Labda uniambie mwanao Kasomea Maeneo ya karibu ila Kwa sasa ndio mmetokea mtwara..
 
Sasa wewe ukitetewa huoni na Wazazi wengine watapuuzia suala la kukamilisha ada wakitegemea kutetewa? Shule itaendeshwaje?

Kwanini hukuomba ukamilishe ada na kununua vifaa ndio uende?

Hukuwa na mawasiliano ya Mkuu wa shule na makamu wake?
Waziri alishatoa maagizo kwamba isitokee mwanafunzi akakataliwa kupokelewa kisa hajamaliza michango.

Mtoto aendelee kupata elimu wakati mzazi anaendelea na taratibu zingine za kutafuta fedha inayohitajika.

Mtoto hatafuti wala hana vyanzo vya mapato kwahiyo kumzuia kuendelea na masomo kisa michango ambayo yeye hahusiki ni uvunjaji wa haki ya kupata elimu.
 
Sasa kama hana hela si aombe msaada serikalini au kwingineko sio kulaumu shule haijapokea mwanae, shule ina haki ya kutopokea mwanafunzi ambaye hajakidhi vigezo
Haya ndiyo majibu ya grown up people. Siyo Yale majibu ya kitoto.
 
Habari Watanzania,

Nawasalimu kwa jina la muungano..

Nina kero yangu haswa kwa shule za advance wanaopokea kidato cha tano Walimu wakuu wanachukua maamuzi ya kukataa kumpokea Mtoto ikiwa tu hajamaliza michango na vifaa vingine kama vile vya usafi ukiangalia umbali uliotoka na Mtoto ni mbali sana.

Mfano mimi mwanangu kapangiwa Kibaigwa Girls iliyopo Dodoma, Mwalimu mkuu na makamo Mkuu wa shule wamenigomea kumpokea Mtoto kisa nimelipia nusu ya pesa za michango na sijakamilisha vifaa vya usafi ukizingatia nimetokea mkoa wa Mtwara

Sijui cha kufanya, naomba waziri husika kufuatilia hili jambo, wazazi tunashindwa kuwapeleka shule mapema watoto kutokana na hizi changamoti.

Naomba kuwasilisha

🤝
Unapata wapi mda wa kupiga siasa uchwara jukwaani wakati huna hela ya kulea Watoto wako mwenyewe?

Wewe ulitaka nani akulelee hao Watoto wako?

Serikali shikilia hapo hapo wajinga kama Hawa ndio wanadhani Kuna vya Bure.
 
Elimu ya TZ ni rahisi sana, yani unaambiwa fagio tu nalo hutaki kupeleka unalalamika.Tuache ujinga
Hata Mimi namshangaa
Rim paper
Fagio
Jembe
Ndio
Fyekeo
Uniform
Vifaa vya masomo

Basi hivyo vitu havifiki hata 300k eti baba mzima kashindwa anakuja kulalamika.

Serikali irudishe ada Ili kukomesha huu uzembe uzembe usio na Tija.
 
Mkuu sio fagio tu,kumpeleka mtoto advance ili apokelewe vitu walivyoorodhesha at least uwe na laki nne ndio pesa ya chini kabisa
Sasa Laki 4 ni hela ya kulalamika kweli? Tanzania Ina watu wazemne sana,basi akashitaki Chadema Ili wampost Twitter,stupid father
 
Ifike hatua tuzae idadi ya watoto tunaoweza kuwahudumia.
 
Habari Watanzania,

Nawasalimu kwa jina la muungano..

Nina kero yangu haswa kwa shule za advance wanaopokea kidato cha tano Walimu wakuu wanachukua maamuzi ya kukataa kumpokea Mtoto ikiwa tu hajamaliza michango na vifaa vingine kama vile vya usafi ukiangalia umbali uliotoka na Mtoto ni mbali sana.

Mfano mimi mwanangu kapangiwa Kibaigwa Girls iliyopo Dodoma, Mwalimu mkuu na makamo Mkuu wa shule wamenigomea kumpokea Mtoto kisa nimelipia nusu ya pesa za michango na sijakamilisha vifaa vya usafi ukizingatia nimetokea mkoa wa Mtwara

Sijui cha kufanya, naomba waziri husika kufuatilia hili jambo, wazazi tunashindwa kuwapeleka shule mapema watoto kutokana na hizi changamoti.

Naomba kuwasilisha

🤝
Peleka michango,acha kulialia kwenye mambo ya msingi huku ukichangia sherehe bila kilio.
 
Back
Top Bottom