Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Kinondoni Shamba amesema alipoongea na wanafunzi wamesema chanzo ni umeme lakini bado haijathibitishwa rasmi. Amesema moto unaendelea kusambaa kwa sababu baada ya kutoa taarifa limefika gari moja lakini wanaomba magari mawili kwa sababu shule ina mabweni makubwa na gari limeshaishiwa maji na moto unazidi kupamba kusambaa hivyo wanaomba msaada wa magari mengine ili msikiti mpya wa Bakwata usije nao ukaungua.
Amesema anashukuru Mungu wameokoa wanafunzi wote na wapo wawili wamewapeleka hospitali hivyo wanafunzi wote wako salama. Amesema kama wananchi wamejitahidi kuokoa vifaa kama computer na vinginevyo lakini juhudi zao zimegonga mwamba hivyo vilivyobaki wamewaachia Jeshi la zimamoto.
Shule ya secondari ya Kinondoni Muslim inateketea moto muda huu, ambapo chanzo chake hakijafahamika mara moja. Endelea kuwa nasi ili kufahamu kwa kina.
Hizi shule 2 za secondary zimeteketea kwa moto kwa asilimia 75%+ nini kiko nyuma ya hii mioto. Turudi nyuma kwa nini hizi shule zilianzishwa? (Vision and mission of these schools) Je, wapi wamiliki wa hizi shule?
History ya walimu wa madrasa wa hizi shule zikoje? Kwa nini fire wanashindwa kufika katika eneo la tukio zaidi ya masaa 3? Na mwisho zinakuja Gari za zimamoto zaidi ya 2?
moto ni kitu hatari sana kwatuliowahi kupata ajali ya moto haswa nyumba tunajua taharuki yake.....moshi ongeza na moto na joto kali na kuchanganyikiwa.....Mungu awasaidie