Shule ya Mafunzo ya Uongozi isitumie jina la Mwalimu Nyerere, bali itambulike kama Shule ya Uongozi (SUT)

Jina la Mwalimu Nyerere limetumika sana katika mambo mengi mpaka barabara mikoani. Inatosha kwa sasa kuliitaita kwenye miradi liitwe kwenye mambo mengine ambayo hayajazoeleka
 
Hicho Ni chuo Cha CCM. Siyo chuo Cha serikali.

Naona hujaelewa hicho kitu.

Kwahiyo kwa CCM kulipa Hilo jina chama Chao, hakuna tatizo lolote.

Maana huwezi kumtenganisha Nyerere na CCM.
Sawa sawa
 
Ilibakia kidogo tu useme kiitwe mbowe academy international.

Ila ndio hivyo tena nyerere ndio alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa chama hivyo ana haki hiyo.

Hujui kuwa Mbowe ni mtoto wa Nyerere.!
 
nadhani hujui branding

Kuna brand Tanzania inayoweza kuuzika kama JK Nyerere katika pande za Dunia ?

Uongozi ni nini ?
Na Nyerere aliongoza Mangapi ?
Ukishajibu hayo na kuelewa Brand awareness nadhani utabadilika....

Kikiitwa Shule ya Uongozi pekee na vikija vingine vya uongozi huku na kule tuviite nini ? Majina ya Mtaa au Miji ?

Sisemi kiitwe Nyerere lakini naona umuhimu na manufaa ya kukiita hivyo hususan this day and age ambapo viongozi ni wabinafsi, wezi, hawana uzalendo wala vision
 
Sasa matusi ya nn! Mambo ya chama huhudhuliwa na mwenyekiti! Mambo ya kitaifa Ndipo Kofia ya URAIS hutumika!

Huwezi muita RAIS kwenda kuzindua tawi la BAVICHA, AU UVCCM
Tatizo la watanzania wengi lipo kwenye kutenganisha Urais na uenyekiti wa Chama. Kama Rais anaweza kualikwa kufungua chichote katika nchi.
 
Kinafunguliwa na Mheshimiwa 23rd February,

Lami imeishia pale pale chuo wakati hiyo ndo njia ya kwenda steshen reli ya mwendokasi.

Maji huku jirani na chuo hakuna ni wiki tatu sasa raia hatuna maji.

Hapa tuko kuandika mabango hatujui yataondoka na nani.
 
Penye Nyaya andika Nyayo...
Majengo hayo si ya kukaribia... utafundishwa uzezeta wa ccm
 
Poleni sana asee.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ni kwa mtazamo tu ila sioni kama kuna tstizo maana lile jina tu ambalo halijabeba chochote kitu, chukulia mfano familia zetu ili kizazi kisisahsulike kinaenziwa kwa kulidhishana majina hata ukienda kwenye mandiko matakatifu ni hivohivo kwa maana hiyo kwangu naona haileti shida maana we pale umefuata mafunzo sio jina la shule au taasisi.
 
Penye Nyaya andika Nyayo...
Majengo hayo si ya kukaribia... utafundishwa uzezeta wa ccm
Hapo hakuna tofauti kati ya nyayo na nyaya kwa sababu obviously neno letu limetoka India au neno like la India limetoka hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…