KERO Shule ya Sekondari Zogowale, Kata ya Misugusugu Kibaha Walimu hawana ofice wapo zaidi ya 50 viti havizidi 15

KERO Shule ya Sekondari Zogowale, Kata ya Misugusugu Kibaha Walimu hawana ofice wapo zaidi ya 50 viti havizidi 15

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

idiomer

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2012
Posts
289
Reaction score
342
Licha ya eneo hilo kuzungukwa na viwanda vingi, shule hiyo haina samani za kutosha kwa wanafunzi wala walimu. Ukifika shuleni hapo, hali iliyopo inasikitisha.

Je, Mkurugenzi na Meya wa Manispaa ya Kibaha wameshindwa kabisa kuhamasisha wadau na viwanda vilivyopo eneo hilo kuchangia kuboresha mazingira ya shule?

Diwani wa Kata ya Misugusugu naye anaonekana kutofanya jitihada za kutosha katika kushughulikia changamoto hiyo.

Je, viongozi husika wanafahamu kikamilifu mahitaji na utekelezaji wa mtaala mpya? Afisa Elimu wa Kata yupo na anafuatilia hali ya shule hiyo?
 
  • Thanks
Reactions: Lax
wapeleke taarifa kwa muajiri wao na wizara hiyo ya elimu, maana siku hizi zinajengwa shule hadi za maghorofa
 
Wanakua wanajua ...hii jamii forum akiiweka tuu chapu viti na ofisi zinajengwaa
 
Kwa hiyo kila siku mnafanyia kazi zenu chini ya mwembe/mnazi huku mmekalia matofali ?
 
Back
Top Bottom