Licha ya eneo hilo kuzungukwa na viwanda vingi, shule hiyo haina samani za kutosha kwa wanafunzi wala walimu. Ukifika shuleni hapo, hali iliyopo inasikitisha.
Je, Mkurugenzi na Meya wa Manispaa ya Kibaha wameshindwa kabisa kuhamasisha wadau na viwanda vilivyopo eneo hilo kuchangia kuboresha mazingira ya shule?
Diwani wa Kata ya Misugusugu naye anaonekana kutofanya jitihada za kutosha katika kushughulikia changamoto hiyo.
Je, viongozi husika wanafahamu kikamilifu mahitaji na utekelezaji wa mtaala mpya? Afisa Elimu wa Kata yupo na anafuatilia hali ya shule hiyo?