Shule ya uongozi ya Hamphrey Polepole (Kataa Wahuni) inatufungua kwa mengi sana

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,866
Reaction score
4,264
Tangu Polepole ameanza series yake kali kabisa ya kataa wahuni, kuna mengi sana nimejifunza na ninaendelea kujifunza. Hakika ni kama jambo la heri sana kwa bwana huyu kutokea na kuendeleza ile shule yake kipindi cha Magufuli. Ni kama vile roho ya Magufuli imemwingia na sasa imentuma kuzungumza yote kwa uhalisia wake.

Huyu si Polepole wa kawaida bali asiye wa kawaida. Pengine itapita miaka kumi na atakuja kushangaa imekuwaje aliongea hayo na bila woga. si yeye bali ni roho iliyowekwa ndani yake kuzungumza haya. Ni sala za watanzania zikiendelea kufanya kazi. Ni vilio vyao pia hasa pale ambapo msaada mwingine haupo isipokuwa ni kwa Mungu pekee. Na Mungu hufanya kazi kupitia watu.

Anamzungumzia Magufuli kwa namna ambayo wengi hatukuwa na picha nayo. Tulimwona Magufuli kama jitu fulani katili kupindukia. Ni kweli alikuwa na ukatili wake na mabaya yake ila kwa sasa tuyaone mazuri yake kupitia Polepole. Ushahidi upo wazi kila sehemu kuwa watu wanasema NYUMBA HAINA MWENYEWE. Mwenye nyumba angekuwepo haya yote yasingetokea.

Katika maisha yangu ni mara mbili nimewahi kutoa machozi bila kupenda japo nilitamani sana kujizuia. Mara ya kwanza ni kifo cha mzee wangu. SIkuwahi kuishi nae na sikuwahi kuona nafasi yake katika maisha yangu ila niliposikia taarifa ya kifo chake, nikiwa peke yangu chumbani nimekaa kitandani (miguu chini), machozi yalitoka yenyewe kwa dk moja hivi. baada ya hapo uchungu uliondoka. RIP

Mara ya pili niliposikia kifo cha Magufuli asubuhi. Nikiwa tena nimekaa kitandani, ila sikuwa mwenyewe. Tena nilikuta nalia kwa dk 2 hivi. Nashukuru mwenzangu hakuniona. Magufuli sikuwa namkubali. Pengine niliaminishwa na propaganda nisimkubali. Aendelee kupumzika kwa amani.

Back to Polepole. Baada ya kuendelea kusikiliza shule yake na yanayoendelea kwenye siasa zetu na za kimataifa kwa ujumla, nimebaini kwa uchache yafuatayo;

1. Raisi awe mbaya vipi au awe mzuri vipi; kazi ya uraisi sio rahisi
2. Nimegundua licha ya Rais kwa na almost absolute power, bado kuna watu wenye power zaidi yake
3. Maamuzi ya mkuu wa nchi, ya aina yoyote ile tuyahoji ila si kwa mihemko. Hatujui ni lipi limempelekea kufanya maamuzi hayo
4. Kama alivyowahi kusema mzee Nyerere kuwa upinzani wa kweli utaanzia CCM, itabaki hivyo. Maono yake ikifika wakati yatatimia. Kina Lissu kazi yao ni kukoleza.
5. Watanzania tunapenda kusikiliza na kusikitika ila nusu saa baadaye tunasahau hadi tukumbushwe tena lilelile.
6. Ukiwa na wadhifa mkubwa kwenye serikali, kuwa makini sana na simama sana na Mungu. Hoji, chunguza, chukua tahadhari
7. Ukitaka kuendesha urais kwa angalau amani kiasi, imarisha taasisi. Toa mamlaka kwa mihimili. usiwe mlafi.
8. Kiongozi wa nchi unaweza kuja na falsafa zako, tena njema tu ila wahuni wakazichukua na kuziweka kando kisha wakakupa zao. Kwa kupenda au kutopenda. Kwa uwazi au kificho (indirect).

Na mengine mengi
#designated survivor

Ni imani yangu kuwa vyombo mbalimbali vya mamlaka vinaendelea kufuatilia shule hii ya uongozi na kwa mamlaka yao wapate nguvu na hekima ya kuchukua hatua stahiki
 
Hata wamuue tayari keshasema ukweli wake wote na watanzania tumejua na uzuri mda si mwingi Tanzanai mpya yaja
 
Aendelee kuwepo ili tuendelee kupata madini haya, japo kweli kasema yenye kutosha kabisa
 
Polepole is the designated survivor. Tumpe support afunguke zaidi nchi yetu ipone. Wenye viapo vya kulinda katiba wamepewa assignment na polepole, waifanyie kazi vinginevyo nao ni waguni tu.
 
Ile series ulishawahi kuitazama? Pale pia nimekula shule ya kutosha kuhusiana na madaraka makubwa. Mle kuna wahuni pia, ila wale wabaya zaidi 🙂
 
Ni zaidi ya Shule, na inaonekana wanavyomjibu ndivyo anavyofukunyua details
 
Wing ya kushoto Mange kulia Polepole
Katikakati anasimam Gwajima. Formation ni 4:3:3 ni kushambulia tu kwa kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom