babayao255
JF-Expert Member
- Apr 4, 2019
- 11,632
- 29,912
Ndo maana mtu wa Mombasa hawezi sema Nishasoma anatamka na kuandika nshasomaUsafi wa Kiswahili unaupataje au unaujuaje ?
Mombasa wanaongea Kiswahili cha lahaja na si Kiswahili sanifu kwa maana kilichoteuliwa.
Ndio maana leo hii hatusemi ya kuwa "Mato" au "Kitwa" ni Kiswahili sanifu bali "Macho" na "Kichwa" ndio Kiswahili sanifu. Japokuwa "Mato" na "Kitwa" ni Kiswahili pia.
Au nakuuliza swali rahisi wewe marejeo yako ya kujua ufasaha wa Kiswahili ni wapi ?