Shule za Serikali kufanya vizuri kuliko za Binafsi: Je, ni mkakati wa kuzifuta shule binafsi, kama walivyokuwa upinzani?

Shule za Serikali kufanya vizuri kuliko za Binafsi: Je, ni mkakati wa kuzifuta shule binafsi, kama walivyokuwa upinzani?

wajingawatu

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2013
Posts
2,046
Reaction score
2,453
Sioni sababu ya shule za Sekondari za Serikali kufanya vizuri kuliko za watu au mashirika binafsi. Ila naamini kuna mkakati wa kuzifuta shule za binafsi kwa njia ile ile iliyotumika kuvidhoofisha vyama vya upinzani. Wenye povu au hoja tofauti mnakaribishwa.
 
Mkuu siyo kweli hapo jua pia kuwa shule binafsi mnawapikia wanafunzi bora wanaowachukuwa kwenda form five hivyo utakuta cleam nyingi zilienda shule za Serikali lazima ufaulu uwe mkubwa na ukakuta bianfsi walichukuwa randomly hawakuqangalizi ufaulu lazima matokeo yawe chini hayo ni mawazo yangu
 
Shule nyingi advance wanaoenda secondary huwa wanachaguliwa vipimgi na vichwa haswa, tofauti na private ambao huiiba mithinani ili wafaulu. Nimesoma government mojaaapo ya shule kongwa hapa nchi darasa Zima tulifaulu kwa division one Hadi three na hapo tulikuwa tunafundishwa kawaida tu Tena tulipata wanafunzi walioingia kumi Bora kitaifa kwa miaka miwili mfululizo. Government School kwa advance level huwa nzuri kuliko huko private loh
 
Mkuu nashukuru kwa uzi mzuri.. kuna shule zipo huko Arusha wanafunzi hata kiswahili hawajui vizur lakini ipo Top ten..

Kuna uwezekkano mkubwa sana kwamba
1.Shule za serikali wanaleta Mark's za upendeleo.. let's say 30+x=××%
2 Shule za binafsi matokeo halisi.

Impact ni miaka kadhaa ijayo hatuwezi ona sasaivi .. kuwa na smart on paper with empty brain.. yale yale ya quack Drs and Engeneers
Siasa za kipumbavu sana yani.
 
Walimu wanafundisha siku hizi. Sio miaka yetu ile upo advance lakini hujawahi kumuona mwalimu wa kemia na bios hadi unamaliza kidato cha sita. Alafu mwalimu anapokea mshahara lakini anaenda kufundisha private. Sasa hivi subutu huo ujinga utashangaa barua inakuhusu.
 
Sioni sababu ya shule za sekondari za serikali kufanya vizuri kuliko za watu au mashirika binafsi. Ila naamini kuna mkakati wa kuzifuta shule za binafsi kwa njia ile ile iliyotumika kuvidhoofisha vyama vya upinzani. Wenye povu au hoja tofauti mnakaribishwa.

Naunga mkono hoja. Tusubiri mwakani na wanaomaliza form 4.

Kwamba hata seminari nazo zimedolora?

Pumzika huko huko tutaonana baadaye.
 
Kwa advance shule za serikal zitabaki kuwa juu,
Mizigo ya advance ada haiamui ufaulu ila kichwa chenyewe cha mwanafunzi na kujituma kwake

Ila o-level lazima wawaachie wawekezaji, mfano ulio hai
Keko secondary form 1 kuna watoto zaidi ya 300
Mwalimu wa somo husika n mmoja wakizid basi wawil. Hilo darasa ata akifundisha malaika atagonga mwamba tu
 
Walimu wanamaliza topic mapema Sana. Walimu wanafundisha jinsi yakujibu mitihani ili ufaulu. Enzi zetu ilikua sifa mapindi mitaani tunajua mambo mengi ila mbinu zakujibu pepa hatuna. Sikuhizi wanasahisha uelewa wa mwanafunzi zamani walikua wanataka jibu sahihi. Hahaha lazima utage
 
Ila kujivunia ufaulu ni upuuzi mtupu ikiwa hiyo elimu haimfanyi mhitimu kujitambua
 
Shule nyingi advance wanaoenda secondary huwa wanachaguliwa vipimgi na vichwa haswa, tofauti na private ambao huiiba mithinani ili wafaulu. Nimesoma government mojaaapo ya shule kongwa hapa nchi darasa Zima tulifaulu kwa division one Hadi three na hapo tulikuwa tunafundishwa kawaida tu Tena tulipata wanafunzi walioingia kumi Bora kitaifa kwa miaka miwili mfululizo. Government School kwa advance level huwa nzuri kuliko huko private loh
Nakuunga mkono Private ni wazuri o-level

Ila Advance ni serikali miaka yote toka Uhuru iko hivyo.

Private school nyingi hazina investment na resources kwenye elimu ya form five na six
 
Ila kujivunia ufaulu ni upuuzi mtupu ikiwa hiyo elimu haimfanyi mhitimu kujitambua

Fact
tuna uzao unaosifia ufaulu usio na ujuzi kwa mwanafunzi.
Hatimaye watoto wanahangaika mtaani kwa kukosa ajira.
 
Kwann ? Maana A level shule nyingi za serikali hasa za science hazina waalimu na vitendea kazi
Wanafunzi hujitambua na Mara nyingi hufundishana wao kwa wao hawategemei sana walimu, mi nimesoma kisimiri kulikuwa na walimu wawili tu ila tulikuwa tunafundishana wenyewe
 
Nakuunga mkono Private ni wazuri o-level

Ila Advance ni serikali miaka yote toka Uhuru iko hivyo.

Private school nyingi hazina investment na resources kwenye elimu ya form five na six
Na Tena wengi waliopata division three mwaka wetu walitoka shule za st Francis ya mbeya na Marian wakati wao ndo walikuja na one ya nane kutoka huko kwao private walivo kuja government wakawa wanakuwa wa mwisho. Waliotoka government hujitaftia kufaulu na kukiwa na walimu wazuri ni lazima mfaulu wote.
I agree with you private wako vizuri olevel na kuiba mitihani ili waongoze ufaulu wapate wateja wengi.
 
Wanafunzi hujitambua na Mara nyingi hufundishana wao kwa wao hawategemei sana walimu, mi nimesoma kisimiri kulikuwa na walimu wawili tu ila tulikuwa tunafundishana wenyewe
Wengi hawajui Hilo kwa government wengi huwa wamepiga tuition na kufundishana wenyewe kwa wenyewe. Kwa advance level na wengi hupelekwa waliofaulu vizuri wamezoea kujisomea tofauti na private too much spoon feeding
 
Kwa advance secondary education shule za serikali ziko vizuri.

Kwanza wanapelekwa wenye uwezo wa kiakili naturally. Mtu katoka Namanyere huko na ana Div 1 ya point 14 akipelekwa advance Kisimiri au Tabora unafikiri huyo mtu ni wa kawaida!?
Pia madogo wanajipigia shule wenyewe na kufundishana kutwa kucha.
Wanaishi kama ndugu wa baba mmoja maana wanajua hawana mtetezi zaidi ya kukata msuli.

Si mchezo hata kidogo.
Na hata wakifika vyuoni huko huwa wako fit.
 
Back
Top Bottom