Shule zenye ubora ni gharama lakini muhimu sana

Shule zenye ubora ni gharama lakini muhimu sana

T14 Armata

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2017
Posts
12,362
Reaction score
41,886
Bila kupoteza muda leo natoa mawazo yangu yanayotokana na uzoefu niliokutana nao mwenyewe.
Kuna mkanganyiko unatokea kwenye suala la elimu na shule hasa za msingi, sekondari na Advanced level. Kuna kundi la wazazi wavivu, sizitaki mbichi hizi na wazembe wa majukumu hasa wakiongozwa na chairman wao humu ana username ya chama tawala cha Israel.

Hawa jamaa wamekuwa wakisimanga uwepo wa shule za binafsi wakihamasisha wazazi wengine wategemee tu shule za serikali, ama wawe na uwezo mkubwa sana ndipo wafikirie international schools. Hawataki kabisa kukubali mchango wa shule binafsi za ada labda 2-4M kwa mwaka, wanaona bora shule ya kata eti kisa wanafunzi ni walewale watakutana chuo, mara ungefanya investment nyingine kwa mwanao.

Nitaeleza matukio ya kweli yakihusisha shule, familia, crew ya hao classmates, background na baadae nitasema kwanini nimepita mbali uko mpaka kuja kwenye hitimidlsho la kwanini mzazi hakikisha mwanao anasoma shule ya maana. Maelezo yangu ni ukweli 100% kasoro majina ya wahusika nimeyabadilisha kidogo.

Binafsi nimesoma shule ya kawaida kabisa ya serikali na nilikuwa na rafiki zangu Salehe, Joshua, Michael, Francis na wengine. Kwenye NECTA form II marafiki zangu wote walifeli, walikuwa vilaza kiasi fulani na walinifundisha utoro ila pia walifeli sababu ya mazingira ya shule na mwamko wa wazazi wao. Hata mrembo wangu wa Form II alifeli (huyu baba yake kafungwa miezi sijui mingapi, nasikia alimpiga mjumbe wa CCM kwenye pombe akamfanyia figisu uko, pia mama yake ni mlevi). Sasa hivi huyu binti yuko Goba ana mtoto mmoja na ana mimba kwa mwanaume huyohuyo age ni 40+. Uzuri wake wote umeisha, kanyoa sahivi hata hasuki hana hela.

Mwaka huo 2015 kabla Magufuli hajafuta ada, shuleni kwetu kulikuwa na genge la wanafunzi waliokuwa wanajificha vichakani na kwenye mapagale wakipika na kulewa pombe uko. Mwasisi wao aliitwa Anfrey walimpa cheo cha jenerali alafu crew yao wanaita International School. Mdogo kuliko wote pale alikuwa Form One, sasa nimeambiwa alikuwa bodaboda akaoa binti mdogo ameacha shule. Alitoroka kwao baada ya kuoa, akakosa marejesho ya chombo akapokonywa na akakosa kodi ya chumba akarudi kwa bibi yake na mkewe akiwa mjamzito.

Hao marafiki zangu huyo Michael alikuwa jobless amejinyonga mwaka huu, alikuwa na ugonjwa wa kifafa na aliishi na shangazi yake nasikia wazazi wake waligombana ndani na mama alimuua baba kwa kumvuta kende. Ilikuwa early 2000s baada ya msiba mama naye hakukaa sana naye akakutwa amefariki ndani. Michael akabaki yatima na hajaacha ndugu ila nahisi aliacha mtoto.

Huyo Salehe alikuwa rafiki yangu zaidi, alipofeli akafanya kazi na Wachina kuna interviews nilikuwa namsaidia. Nikamaliza Form 6 akaniunganisha kibarua "connection" yangu ya kwanza, kwenye hao jamaa niliofanya nao kazi mwenye elimu kubwa form 6 kafeli ndio kiongozi wao, anayefuatia form 6 kafeli naye kiongozi msaidizi. Hawa jamaa wakawa na wasiwasi na mimi maana story za mpira sijui, za Diamond sijui, mimi ni rejea ya facts pale wakidanganyana kwenye vitu vya msingi. (Baada ya chuo nilienda Morogoro nako wakanihisi ni usalama wakanitenga kwa sababu hizihizi, sasa hivi hata kama mpira sijui nikienda sehemu ya watu wenye inferiority complex lazima niseme mfano "yule Mzize mbovu hamna kitu anacheza" ili nionekane kawaida kisha niwaache wadandie mada wabishane).

Ile naanza chuo Salehe akaoa, akafanya bodaboda mpya ya mkataba akapakia abiria usiku akiwa mitaa ya Yombo kidogo wamuue ila akakimbia akaibiwa TVS. Mwaka juzi mwishoni alifariki kwa ajari uko Mbagala, kaacha watoto wawili mmoja hakuwa hata na mwezi.

Hao wengine wana maisha ya kawaida fundi furniture, mwingine alibahatika kupata certificate ya umeme yuko Tanesco.

Nina classmates wengi sana saidia fundi, deiwaka, jobless, vibarua, walevi na wametelekeza watoto. Mwanzoni nilikuwa naona sio shida zangu mpaka nilipoanzisha kibiashara. Baadae nikamfundisha jamaa mmoja kazi nikamleta ofisini nisikae peke yangu nikitoka isifungwe. Sasa ajabu yeye kwenye mizigo ya delivery isiyotokana na ads akaanza kuuza kunizidi, akaanza kutembelewa na wateja marafiki zake. Kumbe bwana yeye shule alikuwa mchache sana kichwani ila alisoma shule ya maana kaishia sekondari, ana classmates wamesoma, wana biashara, wana exposure na vitu vingi mpaka wamekuwa msaada kwangu na ni wateja.

Yeye ni livivu lizembe ila anabebwa na watu wanaomzunguka. Mimi sijawahi uzia classmate wa O level maana siuzi necessity products, wao mpaka mtu awe na njaa ndio anunue chakula, mpaka nguo ichakae ndio anunue nyingine. Nina jamaa wanakula sana hela zangu kwenye michango yao wanatarajia nijitoe sana ila wao sifaidiki nao kwenye utafutaji.

Hapo ikanipa taa nyekundu kichwani, ikabidi nitazame rafiki zangu wa chuo na partners kwenye biashara. Hapo ndio nikaja kuona umuhimu wa kusoma shule zinazoeleweka. Kumbe bwana nina watu wachache sana wa kuunga mkono kazi yangu. Nimekuta marafiki zangu waliosoma shule za mabasi ya njano wana marafiki wenye tabia zifuatazo:

• Wana exposure sio washamba, wamesafiri nje, wana passport, wajanja kujua fursa ziko wapi. Mimi saidia fundi wangu na bodaboda hawanisaidii kabisa alafu wabishi kama nini wana visingizio sana hata uwashauri jambo la maana.

• Wanasaidiana misaada mikubwa hawajakurupuka kuoa kisa nyege kwahiyo hawashindani kuchangia harusi wao wana vikundi vya kukopeshana na kuweka. Wengi kwenye mid 20s hakuna mwenye haraka ya kuoa na hata wakifika muda nina imani hawatachangiana mabakuri na harusini kumimina bia kwenye madumu kama wafanyavyo hawa wa kwangu.

• Hawana njaa, wana purchasing power kubwa wengi hawajatokea familia duni wanasaidiwa hata mawazo na familia zao, mikopo, wanapewa mitaji, fursa. Huyu wa hivi anaweza kuja dukani kwako ukamshawishi kumuuzia kitu akaamua kulipia kidogo hata kama bidhaa yenyewe alikuwa haijui ila ndugu zangu wale ni waulizaji sana ila kununua hawana hela.

• Hawana wivu wa kijinga na roho mbaya. Wale ambao hawajakulia kwenye shida chuki wanajifunzia ukubwani, hawakai na hasira hovyo, hawana kijicho na roho mbaya. Na wako tayari kumfundisha mtu hata kama ni maskini kaingia kwenye kundi lao kwa bahati. Tofauti yake sasa hao wengine ikitokea mmojawapo kafanikiwa kukwepa cycle of poverty tiyari anachukiwa kwa chinichini. Akikosea matamshi kidogo wanakurupuka kusema anajisikia na anaringa, kuna jina tunaitwa na tuliosoma nao tunaitwa "akina Armata". Tulifaulu wachache sana sitaki kusema idadi hivyo tunaonekana kama tumesaliti waliofeli na vile tulitumiwa kama mifano "unasema shule walimu hawafundishi mbona fulani kafaulu" basi sisi ni alliens. Wakati shule za maana kufaulu sio ajabu, hakuna kundi special la waliofaulu. Umpeleke mwanao Yombo Sekondari afaulu vizuri si anatupiwa majini huyo.

• Wengi hawajatelekezwa na wazazi wao (kama kwangu kina Michael na Salehe). Haijalishi kama wanaishi nao au ni separated families ila wazazi wao wanawajibika na kugharamika. Hawa jamaa wanaoshinda wanapinga shule za kulipia ada ndio watelekezaji wakubwa. Wanategemea wafyatue tu serikali ilipie gharama eti kisa wao watachangia uji tu. Matokeo yake unamuweka mwanao kwenye mzunguko wa watu duni wenye tija kidogo kwake.

Kuna outliers zinatokea ila bado shule nzuri inarahisisha maisha baadae kwa wengi, wachache wanaoharibikiwa kutokana na private schools wanashikiwa bango na kuonekana ni kielelezo cha kutokuwepo umuhimu wa shule hizo kumbe ujanja tu wa kukwepa majukumu. Kuna jamaa MM tulisoma nae A level kwao uwezo mdogo sana, akafaulu vizuri akakosa mkopo chuo. Kumbe alilipiwa ada na mjomba wake aliyetumbuliwa na Magufuli, kukosa mkopo tu akaghairi chuo. Ila ukouko O level alikotokea kuna rafiki yake kaka yake ana hardwares kubwa akamuunganisha nae maana MM ni mwaminifu. Akafanya kazi miaka miwili akajikusanya na sasa yuko mwaka wa pili chuo. Sasa angesoma na sisi nani angempa kazi labda kuuza gongo.

Namaliza kwa kusema hivi, hapo nimetaja makundi mawili sasa wewe chagua lililo jema kama una uwezo. Kama huna sawa ila usitafute visingizio na kujifariji.

Anayebisha muache dunia huru hii, matokeo utaanza kuyashuhudia kwenye harusi ya kijana wako marafiki zake ukumbi utajaza vishandu kama kijiweni. Mzee wangu siwezi msamehe kanipeleka lishule libovu kweli hata nisiposoma nakuwa wa kwanza sasa shule gani hiyo. Shule wanafunzi wanatoroka kufanya deiwaka, mara ni wacheza shoo harusini na sasa hivi walevi wa visungura.
 
Sijasoma kabisa ulichoandika (marefu sana) ila itoshe kusema ukitaka mtoto wako awe vizuri ki elimu na kimaadili basi chekechea hadi la Saba kufa kupona asome hizi English medium na kama Kuna zile za wakatoriki jirani basi peleka huko ukiweza peleka na sec kabisa
 
Sijasoma kabisa ulichoandika (marefu sana) ila itoshe kusema ukitaka mtoto wako awe vizuri ki elimu na kimaadili basi chekechea hadi la Saba kufa kupona asome hizi English medium na kama Kuna zile za wakatoriki jirani basi peleka huko ukiweza peleka na sec kabisa
Mkuu naweza kaa miaka miwili bila kuandika thread ni mpaka jambo liniguse sana ndio naandika. Na siandiki kivivu.

Mtoto hata akisoma hizi zinaitwa English medium kisha akaenda sekondari anakuwa hata kujiamini ni tofauti na huku wanakobeba madumu ya maji.
 
Kafanye utafiti upya...
Haina haja ya utafiti mpya. Kuna vitu vipo wazi, wewe siku utakapoona watoto wa wanasiasa wanasoma shule za serikali ujue mambo yako sawa.
Hata hao watoto wa matajiri ambao hawakusoma, nao wanasoma shule zq gharama. Kisa Sauli kaishia la saba usingekuta wanae wanasoma shule mbovu. Au kwani Super Feo wanae kawapeleka shule za bure kisa alisomea kwenye shida akaishia la saba.
 
Sio kila mtanzania ana uwezo wa kumpeleka mwanae shule za gharama ila kwa wale wenye uwezo huo wafanye hivyo. Shule za kata zina msaada mkubwa sana kwa wazazi walio na kipato kidogo na ndio zilizobeba idadi kubwa ya wanafunzi.
Jambo la msingi ni sisi wazazi tushirikiane na walimu kuwasimamia watoto wetu wasome kwa bidii. Jitihada zikifanyika kwa pamoja vijana watafanya vizuri katika mitihani yao.
 
Haina haja ya utafiti mpya. Kuna vitu vipo wazi, wewe siku utakapoona watoto wa wanasiasa wanasoma shule za serikali ujue mambo yako sawa.
Hata hao watoto wa matajiri ambao hawakusoma, nao wanasoma shule zq gharama. Kisa Sauli kaishia la saba usingekuta wanae wanasoma shule mbovu. Au kwani Super Feo wanae kawapeleka shule za bure kisa alisomea kwenye shida akaishia la saba.
Swala sio shule anazosoma mtoto ndo apate exposure, the matter is uchumi wa familia
 
Swala sio shule anazosoma mtoto ndo apate exposure, the matter is uchumi wa familia
Sasa si uchumi unaamua hata shule ya kusoma mkuu. Ndio hapo nashauri wenye uwezo wahakikishe hizo shule zenye ubora wanazifikia
 
Shule ya kwanza ni Familia, izo nyengine ni ziada. Ukitaka kutoa products nzuri za watoto jenga Familia bora.

Hata akisoma shule ya kidumu na mfagio, 80% atakuwa mtu bora kwenye jamii.
Ndio ndio watoto wanakuwa average kwenye jamii. Vigumu sana kufanya maajabu, sasa mtu anahitimu chuo hata lugha ya kigeni hajui unategemea ashindane kwenye soko la ajira kimataifa.
 
1724531176408.png
 
Sijasoma kabisa ulichoandika (marefu sana) ila itoshe kusema ukitaka mtoto wako awe vizuri ki elimu na kimaadili basi chekechea hadi la Saba kufa kupona asome hizi English medium na kama Kuna zile za wakatoriki jirani basi peleka huko ukiweza peleka na sec kabisa

Wewe ulisoma hizo shule? Kwa hiyo umepungukiwa nini?
 
Sasa hivi huyu binti yuko Goba ana mtoto mmoja na ana mimba kwa mwanaume huyohuyo age ni 40+. Uzuri wake wote umeisha, kanyoa sahivi hata hasuki hana hela.
Mbona imekaa kikuda Sana hii,kwani lengo kuu la uzi ulitaka liwe Nini?
 
Mbona imekaa kikuda Sana hii,kwani lengo kuu la uzi ulitaka liwe Nini?
Lengo la uzi liko kwenye uzi wenyewe. Unaweza iona imekaa kikuda huo ni mtazamo wako, ila huyo binti kafeli shule kidato cha pili kutokana na shule aliyosoma na maisha ya nyumbani kwao. Mwishowe ameingia kwenye cycle ileile ya umaskini uleule.
Angesoma shule nzuri kidogo tu asingefeli, angekaa shule muda mrefu zaidi akakomaa akili, asingetoroka kwao kuishi kwa mwanaume kisa maisha yamemshinda. Hata angeweza pata marafiki wa maana shule nzuri na hata angeelimika zaidi akaajiriwa au kujiajiri au kuwa jobless ila sio desperate hivi, na angezaa watoto wake anavyojisikia yeye. Sasa yuko kwa mwanaume anateswa kisa hana shule, kazi wala yeyote wa kumsaidia.
 
Back
Top Bottom