Shura ya Maimamu Tanzania: Mlinzi Mwanamume wa Rais kuvaa Hijabu na kuingia Msikitini

Kwanza tujue hiyo shura ya maimamu ni kikundi au mamlaka rasmi iliyokua na usajili au ni hivi vikundi vya kiislam vinazukaga kama uyoga na kujipa uwezo mbele ya jamii huku havipo kisheria. Tukimaliza hapo tuangalie hili jambo.
Kwa maoni yangu sio sahihi kabisa ulinzi wa rais kumuingiza mwanamume sehemu ya wanawake kwenye msikiti kwa hivyo yeyote aliyefanya hivyo inabidi achukuliwe hatua. Japo binafsi sio muislaam najua namna na desturi za waislaam kuheshimu ibada na kuna kitu wanaita udhu nadhani usafi. Kama kulikua na udharura inabidi kuomba radhi na hata kama ni dharura naona ingebidi walinzi wabaki nje ya msikiti au rais asishiriki kabisa ibada.
 
Okay. Vipi mwanaume akiingia tu kawaida msikitini akaenda upande wa wanawake. Je ibada itasitishwa? Je kuna kifungu ambacho wata refer to?
 
Mihemko tu. Rais alindwe.
Sahihi alindwe, ila sema wewe hii siyo dini yako hivyo hujui UTARATIBU na MIIKO yake. Na kitu usichokijua siyo vizuri kukishangilia maana utazidi kupotosha na wengine.

Hapa watu hawaangalii nafasi ya mtu ktk serikali, wanaangalia UTARATIBU na MIIKO ya dini husika inasemaj. Km wangekuwa wanaangalia nafasi ya mtu basi Rais huyo angeingia msikitini na mabunduki yamemzunguka km anapokuwa kwenye mazingira mengine ya kawaida.

Km ingekuwa inaangaliwa nafasi aliyonayo basi asingevua viatu nje na kuingia peku msikitini na wasaidizi wake.

Km ingekuwa inaangaliwa nafasi aliyonayo asingefuata maagizo ya IMAMU wakati wa kuswali. Imam akielekeza kuwa "sasa ni muda wa swala kila mtu azime SIMU yake lazima azime". Unajua ni kwa nini.

Tusipende kudakia na kushadadia mambo tusiyoyafahamu. Madaraka ya duniani mwisho ni mlangoni mwa mlango wa nyumba ya ibada. Nyie ndo mnakuwa viongozi tayari unachukuwa na nafasi ya Mungu, unaanza kudharau watu, kuwatusi, na kuwatisha ili wakunyenyekee.

Kumbuka wanaoona km jambo lilofanyika halikuwa sawa ni ndugu zake wenyewe (WAISLAM WENZAKE). Sasa wewe wa upande wa pili unapata wapi nguvu ya kusema alikuwa sahihi lazima alindwe. Km kulikuwa na tishio la usalama asingetoka hata kwake. "Ulinzi pekee wa uhakika unatoka kwa Mungu, Unaweza kuwa na mabunduki yako na mapanga lakini ukauwawa na MANATI."
 
Picha iko wapi
 
Manati ya Daudi 😂😂😂😂
 
Okay. Vipi mwanaume akiingia tu kawaida msikitini akaenda upande wa wanawake. Je ibada itasitishwa? Je kuna kifungu ambacho wata refer to?
Ahaa!!

Hilo swali lako ujumla wake ndiyo inatakiwa ijulikane kama ni mapokeo tu ama surah/aya inayokataza wanawake kuchanganyika na wanaume wakati wa kuswali ipo.

Maana wakatoliki wanapiga alama ya msalaba kabla ya kusali wakati wakristo wengine hawafanyi hivyo. Kwa ivo kupiga alama ya msalaba ni mapokeo tu ila yanayoheshimiwa.

Kwa ivo inawezekana pia kutochangamana wanawake na wanaume wakati wa kuswali inawezekana isiwe sharia ya kiislam ila ikawa ni mapokeo yanayoheshimiwa.

Siyo dhambi kuheshimu mapokeo(Sunnah).
 
Umesema Sana mkuu. Hapo umekua mtu na nusu. Hakuna mamlaka yazidiyo ukuu wa Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…