Shura ya Maimamu yataka Mkataba wa Bandari Uboreshwe na haki itendeke kwa Makumi ya Masheikh walioko Jela nchi nzima

"Kwa mujibu wa makubaliano hayo Serikali ya Tanzania inatao fedha (mabilion), kwaajili ya kuendeleza miradi mikubwa ya Afya na Elimu ya Makanisa. Ingawa fedha hizo ni za Watanzania wote lakini serikali haikuwahusisha Waislamu katika mjadala na wala haina mpango wa kufanya mkataba kama huo na raia Waislamu Tanzania. Kubwa zaidi mkataba huo ni wa milele hauna ukomo......."
Hi nchi buana ina mambo mengi watu wana duku duku zao
Hapa hawa waheshimiwa hawakusema ukweli. MoU ilihusu shule na hospitali zilizojengwa na taasisi za kikristu lakini zilitaifishwa na Mwalimu Nyerere. Hospitali ya Bugando ilijengwa na wakatoliki na walikuwa wakiiendesha na ya KCMC ilijengwa na walutheri ambao nao walikuwa wakiiendesha.

Baada ya serikali kuzimiliki kwa zaidi ya miaka 13, serikali ya Ali Hassan Mwinyi ikakiri kuwa haina uwezo wa kifedha na wakitaalamu wa kuzihudumia. Hapo ndipo wazo la kuzirudisha kwa waliozijenga likaja. Taasisi za makanisa zikakataa kuzipokea mpaka pawepo makubaliano rasmi kuwa serikali haitakuja kuzitaifisha tena. Hiyo MoU inatoa ahadi hiyo.

Aidha, kwa sababu serikali ilitaka ziendelee kutoa huduma kama hospitali za rufaa za taifa basi walikubaliana kuwa serikali itachangia gharama zitakazotokana na huduma hizo ambazo ni lazima zitolewe kwa bei ambayo wananchi wataweza kumudu.

Hayo ndio maudhui ya hiyo MoU ambao watu wenye nia ovu wanayapindisha ili yaendane na agenda yao. Tofauti na wanavyotaka watu waamini, hospitali hizo zilijengwa kutokana na sadaka na michango ya wakristu waliokuwa ndani na nje ya nchi. Waislamu hawakuchangia chochote katika ujenzi wake.

Mchango wanaotoa serikali kwa hospitali hizo hauendani kabisa na gharama zake. Ukitaka kulinganisha, angalia gharama za hospitali ya taasisi ya kiislamu ya Aga Khan ambayo haikuwahi kubinafsishwa na haipokei mchango kutoka serikali.

Aidha, hospitali hizo zinatoa huduma ya kufundisha madaktari wetu bila kujali dini zao na wakitoka hapo wanaenda kutoa huduma katika hospitali za serikali.

Hali hiyo inaonekana pia katika shule zilizotaifishwa halafu zikarudishwa kama Forodhani Sekondari na Mazengo Sekondari. Shule hizi zilikuwa ICU ziliporudishwa kwa waliozijenga. Ziliporudishwa kwa waliozijenga ndio kumezipa uhai mpya.

Tofauti na inavyosemwa hapa, ile MoU imewasaidia sana watanzania maana bila ile hospitali na shule hizo zingebakia maghofu tu. Tukipima kila kitu kwa kuendekeza dini hatutafika mbali.

Amandla....
 
Acha malumbano, jadili suala la msingi linalotuunganisha la bandari. Masheikh hawajapenda mkataba kama ulivyo. Hayo mengine yaliyobaki si lazima wawe na mawazo sawa na taasisi nyingine.

Nyie ndo huwa mnashindwa kutafuta common ground ya kinachowaunganisha mnakimbilia kwenye kile kinachowatenganisha!.

Au unataka masheikh wasiseme ila maaskofu peke yao ndo waseme, wewe vipi?
Kuna askofu alizungumzia mikataba iliyoingiwa na marais wakiislamu na chuo cha serikali kilichotolewa na Rais mkristu kwa waislamu? Hawa masheikh wamejikita zaidi katika kuonyesha mapungufu yaliyofanyika wakati wa utawala wa marais wakristu kuliko kuonyesha mapungufu ya IGA kati ya Dubai na Tanzania.

Amandla....
 
Bismillahir Rahmanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA
BARAZA LA IDD ADH-HA, ALKHAMISI TAREHE 29.06.2023 -1444.
“HAKI NA UKWELI VITHAMINIWE”

FALSAFA YA IBADA YA HIJJA

Awali ya yote tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema kwa kutupa fadhila nyingi. Tunamuomba Azidi kuturehemu kwa namna mbalimbali.

Aidha kwa furaha kubwa tunawapongeza Waislamu waliojipanga wakajitahidi wakaenda katika mji mtakatifu wa Makka kufanya ibada ya Hijja mwaka huu.

Juzi walikua Arafa mahala ambapo huwakutanisha mamilioni ya Waislamu kutoka kila kona ya dunia.

Dunia imejifunza kwa kuakisi mkutano kama huo mjini New Yorke Marekani ambapo mataifa mbalimbali hukuta katika kikao cha Umoja wa Mataifa UN.

Jana walichinja wanya katika kitongoji cha Jamarat kwa lengo la kushukuru na kuwafariji maskini kwa chakula chenye thamani siku ya sikukuu.

Mafundisho ya Hijja ni mengi mno na yenye faida kubwa katika maisha ya mwanadamu.

Mwisho tunajipongeza Watanzania tuliopo hapa nchini ambao tuliungana na wenzetu siku walipokutana Arafa na siku walipochinja kwaajili ya kuwafariji watu wenye kipato kidogo na maskini kabisa.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe maisha yalio bora hapa duniani na kesho akhera.

HAKI ZA BINADAMU TANZANIA

Hili ni tatizo kubwa linalo wakabili raia hasa Waislamu nchini Tanzania. Waislamu wamekuwa wakikandamizwa kama Waislamu kiasi cha kutungwa sheria zinazoashiria kuwahukumu kabla kutenda kosa.

Kwa sheria hizo hasa ile inayoitwa ya kupambana na ugaidi, wamekua wakiwekwa jela miaka mingi bila ya kuhukumiwa na wengine wakihukumiwa na kufungwa jela mpaka miaka 50. Hivi jana mjini Morogoro Waislamu 21, wamehukumiwa miaka 15, 20 na 30, baada ya kukaa jela kwa zaidi ya miaka 10.

Wengine 10, huko mkoani Tanga wamehukumiwa kunyongwa mpaka kufa.
Baadhi ya wale walioko katika gereza la Arusha wamekatwa viungo na vyombo vya dola na wengine wamepoteza maisha wakiwa mikononi mwa vyombo hivyo.

Tufupishe kwa kusema Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayopoteza sifa ya utu na haki kwa raia wake.

UCHUMI TANZANIA

Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961. Katika hatua za kuasisi misingi ya uchumi wake moja ilikuwa ni kutaifisha asasi zote kuu za uchumi za sekta binafsi na kuzifanya mali ya serikali.

Viwanda, Mashirika ya Uchumi, Mashamba makubwa na miradi mingine vikamilikiwa na serikali.

Asasi hizo ambazo zilikuwa zikiingiza mapato makubwa kwa wenyewe, vilevile zikichangia pato la serikali na kutoa huduma mbalimbali za kutosheleza mahitaji ya jamii, zilitarajiwa kuendelea na hali hiyo chini ya mmiliki mpya serikali.

Hata hivyo mashirika hayo baada ya kumilikiwa na serikali yalipoteza uwezo wa mapato, huduma bora, na kuwa tegemezi kwa serikali. Mashirika mapya yaliyoanzishwa na serikali nayo hayakuweza kutoa faida na wala huduma stahiki kwa umma.

Yapo mashirika mengi kama vile MUTEX (kiwanda cha nguo cha Musoma), toka yalipoundwa mpaka yalipokufa au kutoka mikononi mwa serikali (kwa zaidi ya miaka 20), hayakuingiza senti hata moja ya faida katika kapu lao wala kutoa gawio kwa serikali. Huduma kwa jamii pia ilikuwa sawa na hakuna.

Taarifa za ukaguzi wa hesabu za mashirika ya umma za Tanzania Audit Corporation, zilionesha ni takriban mashirika 10 tu, kati ya zaidi ya 400, ndio yaliyokuwa na ahweni kidogo na yaliosalia yalikuwa yakiendeshwa kwa hasara kubwa. Kwa muda wote huo serikali ilikuwa ikiyapa fedha (ruzuku), mashirika hayo kila mwaka na yao yakizalisha hasara.

Baadhi ya mashirika hayo likiwemo la chama tawala CCM (SUKITA), serikali iliyadhamini kwa kupewa mikopo ya mashirika ya fedha ya kimataifa na hatimaye madeni hayo yalibebwa na serikali baada ya mashirika hayo kushindwa kuyalipa. Mashirika hayo yalishindwa kurejesha gharama zao na kuingiza faida kwao na kutoa gawio kwa serikali.

Katika miaka ya 1980, mpaka 85, taarifa za viwanda, mashirika na kampuni mbalimbali za serikali kufungwa na mamia ya wafanyakazi kupewa likizo bila ya malipo, zilisikika kila kukicha Tanzania. Hata viwanda na kampuni ambazo zilikuwa hazina mpinzani wa kibiashara hazikufanya vizuri badala yake ziliingiza hasara kubwa na hatimaye kufa kabisa. Moja ya vinda hivyo ni kile cha kutengeneza matairi ya gari (General Tire). Si kwamba havikuingiza pato kwa serikali bali pia vilishindwa kutoa huduma inayoeleweka.

Aidha wakati Watanzania wakiendelea kung’ang’ania kuendesha mashirika hayo kwa hasara chini ya mfumo wa “mali yetu tuendeshe wenyewe”, mataifa ya jirani kama Kenya yalikua na mashirika kama hayo. Mashirika yao yalikuwa yakiendeshwa na sekta binafsi (kama Tanganyika ya zamani), na yalikua yakitoa faida kubwa kwa wamiliki wake, yakilipa kodi ya kutosha kwa serikali na huduma bora kwa umma.

Wakati Tanzania madukani hamna chochote zaidi ya chumvi, waya za kusugulia masufuria, majani ya chai na unga wa mhogo wenye wadudu, Kenya bidhaa zote zilikuwa zimefurika madukani na mahitaji yote ya kibinadamu kwa ujumla yalipatikana.

Tabia ya Watanzania ya kung’ang’ania kumiliki au kuendesha jambo hata kama hawaliwezi, halina faida kwao, linawaumiza, ilijengwa wakati huo.

Katika mjadala uliopo wa tuwape Kampuni ya DP World ya Dubai waendeshe Bandari ya Dar es Salaam au tusiwape, yupo kiongezi wa dini amesema tusiwape bali tuwajengee uwezo watu wetu. Bilashaka historia fupi ya uchumi wa Tanzania tuliyoitoa hapo nyuma inaweza kutusaidi katika hoja hiyo.

SERA YA UWEKEZAJI

Serikali ya awamu ya pili ilipoingia madarakani ilijaribu kufufua baadhi ya mashirika hayo lakini mafanikiao yalikuwa hafifu. Shirika la fedha duniani IMF, lilishauri serikali kutoyapa fedha (ruzuku) mashirika hayo kwa sababu hayana faida kwa taifa na hayakopesheki.

Katika muktadha huo serikali ilifanya marekebisho ya baadhi ya sheria na kutunga sheria ya ubinafsishaji inayokwenda pamoja na uwekezaji.

Serikali ya awamu ya tatu ilipoingia madarakani ilitekeleza sera hiyo mpya kwa kubinafsisha mashirika, viwanda, mabenki, mashamba, majumba, na migodi. (Haikuwa jambo la kujivunia lakini lipi bora kati ya uzalendo wa maendeleo na uzalendo wa kujiletea umaskini. Tunakiri pia katika utekelezaji kulikua na umakini mdogo na kasoro kadhaa).

Moja ya mashirika yaliyobinafsishwa ni Kiwanda cha Sukari Moshi TPC. Kiwanda hiki kama vingine kilikuwa kinaendeshwa kwa hasara kubwa kama tulivyosema huko nyuma. Wakati wa awamu ya tatu kikabinafsishwa kwa kuwapa wawekezaji Kampuni ya Wazungu ya ALTEO kutoka Mauritius. Wazungu hawa wamepewa hisa ya asilimia 75 na serikali imebaki na asilimia 25 tu. Faida yake leo hii tunaiona tunapata takriban shilingi bilioni 25, kwa mwaka na ajira zimeongezeka.

Mifano ipo mingi tutosheke na kwamba nchi yetu ina sera ya uwekezaji na wageni wamepewa miradi mikubwa mikubwa ikiwemo migodi ya dhahabu, almasi na mingine kama hiyo.

Aidha yale wanayoyafanya tunayaona kwa mfano Wazungu pale walipowekeza katika migodi yenye thamani kubwa, hawachukui madini tu balia wanachukua na vifusi vya mchanga wa ardhi hiyo na kupeleka katika mataifa yao. Ni kweli ni wajibu wetu kuzuwia kila linaloonekana kinyume na maslahi ya taifa lakini hatuwezi kusema tumewauzia nchi wazungu kwa sababu mikataba haisemi hivyo.

UWEKEZAJI BANDARINI

Tumeona hapo nyuma Tanzania ilitunga sheria na kufungua mlango kwa wawekezaji wa nje. Pia tumesema yapo mashirika mengi ya kigeni yaliyopewa dhamana ya miradi mikubwa ya kitaifa ikiwemo migodi mikubwa.

Katika muktadha huo ndio mwaka huu pamekua na mchakato wa uwekezaji katika sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam.

Baada ya serikali kukamilisha hatua zake za ndani ilipeleke mswada husika bungeni ili wawakilishi wa wananchi waujadili. Mswada huo ulikuwa na sehemu mbili kubwa. Kwanza ulitambulisha kampuni ya DP World ya Dubai kwamba ndiyo mbia anayetarajiwa kuendesha sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam. Pili ni sehemu ya rasimu ya mkataba unaotarajiwa kufungwa kati ya kampuni hiyo na serikali (Inter Government Agreement - IGA).

Wabunge wengi walijadili kwa namna tofauti lakini hatimaye wengi wao waliunga mkono makubaliano hayo ya awali (IGA). Kwa hali hiyo sehemu ya awali ya mkataba imepitishwa na bunge.

BAADA YA BUNGE KUPITISHA IGA

Wananchi walioona mjadala wa bunge waliona kama tulivyoeleza kwa ufupi hapo nyuma.
Kwa wale ambao hawakuona moja kwa moja bungeni, walipata taarifa ya jambo hilo kupitia wasemaji mbalimbaliu katika vyombo vya habari. Na hawa waliopata taarifa kwa njia hio ndio wengi zaidi.

Wasemaji hao walikua wamefanya mapitio ya mchakato wa zabuni na mkataba na hatimaye kwa uelewa wao waliona mambo kadhaa yakiwemo sita:

1. Mkataba una mapungufu ambayo hayawezi kurekebishika.

2. Mchakato wa zabuni umefanywa kwa kificho na makampuni mengine
hayakupewa fursa kama waliyopewa DP World.

3. Mchakato unatia mashaka kwa sababu baadhi ya viongozi akiwemo Rais,
Waziri wa Uchukuzi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, wanatoka upande wa pili
wa Muunga wa Tanzania (Zanzibar).

4. Mchakato huo haukuwa na nia njema kwa Tanganyika ndio maana
haukuhusisha bandari za Zanzibar wanakotoka viongozi hao.

5. Kupitia mkataba huo upo uwezekano wa bandari kutumiwa na magaidi kuingiza silaha na kuhatarisha amani ya taifa.

6. Baadhi yao walihitimisha kwa kusema kwa hali hiyo, bandari imeuzwa na wauzaji hawakua na nia njema kwa Tanganyika.

Hoja hizi zilipata nafasi kubwa katika vyombo vya habari na kupelekea baadhi ya jamii kujadili uwekezaji wa bandari ya Dar es Salaam kwa mwelekeo huo.

HALI ILIOPO SASA

Wabunge wengi wamefurahia kurejeshewa uhuru wao wa kujadili na kupitisha mambo muhimu ya taifa kwa niaba ya watu wao. Raia pia mtaani wamefurahia kutoa maoni kisha wakabaki salama.

Hata hivyo katika suala hili (mtaani) Watanzania wamekosa muundo mzuri unao wawezesha kujadili kama wamoja, kutafakari kwa kina na hatimaye kuona maslahi makubwa au hatari kwa taifa lao. Kwa upungufu huo watu wamegawika katika makundi makubwa matatu:

• Wako wanaosema mkataba wa serikali na DP World haufai kabisa uondolewe.

• Wako wanaosema mkataba huo ni mzuri upite kama ulivyo.
• Na wako wanaosema Mkataba unamapungufu yanayorekebishika.

Hiyo ndio taswira tuliyoiona katika jamii ingawa inabadilika kama tutakavyoona huko mbele.

MTAZAMO WETU

Kwa hakika hoja za Uarabu, Uislamu na Ukristo zilizotolewa katika suala hil, ni hoja binafsi ambazo hazina mashiko katika suala la uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam. Pia Uzanzibari, Utanganyika na Ugaidi ni hoja binafsi.

Mwka 1992, Serikali ya Tanzania iliingia mkataba na Kanisa uitwao, Memorandum of Understanding between Christian Council of Tanzania and Tanzania Episcopal Conference and the United Republic of Tanzania (MoU).

Kwa mujibu wa makubaliano hayo Serikali ya Tanzania inatao fedha (mabilion), kwaajili ya kuendeleza miradi mikubwa ya Afya na Elimu ya Makanisa. Ingawa fedha hizo ni za Watanzania wote lakini serikali haikuwahusisha Waislamu katika mjadala na wala haina mpango wa kufanya mkataba kama huo na raia Waislamu Tanzania. Kubwa zaidi mkataba huo ni wa milele hauna ukomo.

Pamoja na kwamba suala la MoU kati ya serikali na makanisa ni mkataba, na uwekezaji wa DP World na serikali ni mkataba, lakini abadan hatuwezi kuhusisha suala hilo na suala la Bandari. Kwa hoja au dhana tu (Interpretation), au kulinganiasha. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeliingiza jambo mahala si pake.

Tofauti za uhakika katika suala la bandari ni tofauti za mtazamo wa kiuchumi zaidi na si vinginevyo.

Kwamfano ukisema bandari ikiendeshwa na Waarabu upo uwezekano wa magaidi kupenya itakuwa ni sawa na kusema, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam unatumika kuingiza magaidi kwa kuwa unaendeshwa na Wazungu wa “Swissport” jambo ambalo si kweli.

Aidha katika uchunguzi wetu kadiri mjadala unavyokomaa watu wanaelekea katika hatua nzuri. Hivi karibuni tumesoma waraka wa Wakili Msomi Boniface A. Mwambukusi ulio sheheni mambo mengi na katika aya za mwishoni amesema:

“Uboreshaji wa (Inter Government Agreement) IGA”.
1. Ukomo wa mawanda ya mradi na utekelezwaji wa shughuli zote zilizokubaliwa katika mradi husika.
2. Kuweka kifungu cha kuongoza uvunjaji wa Mkataba.
3. Kuondoa vifungu vinavyoashiria umilele.
4. Kuondoa vifungu ambavyo moja kwa moja au kwa matokeo yake vinaondoa
haki ya nchi ya umiliki wa rasilimali (Sovereignty), haki ya nchi kufanya ushindani na fursa ya nchi kuruhusu wawekezaji wengine katika eneo la uwekezaji wa bandari.
5. Kuhakikisha uzingatiwaji wa sheria zingine za nchi na kuhakikisha kwamba mkataba huu hauwi juu ya katiba ya nchi, sheria za ardhi na sheria zinazolinda rasilimali asili za nchi.

Mawazo ya uboresha wa mkataba kama hayo sasa yanatolewa na wengi yakiwemo yale ya kuundwa kampuni ya uendeshaji yenye umiliki wa asilimia 50-50, kati ya DP World na kampuni ya umma itakayokuwa na hisa nyingi zaidi. Mengine yanasema:

1. Suala la muda wa mkataba utakaoingiwa kwa ajili ya uwekezaji liwe wazi pamoja na vipindi vya kufanya marejeo (Contracts reviews).
2. Suala la aina ya uwekezaji liwe wazi kwamba itakuwa Concession Agreement- CA. (Yaani uwekezaji usiwe ni kukodisha bandari au kubinafsisha bali iwe Ubia). CA hii iwe na muda maalum kwa mfano miaka 25, na kila miaka 5, kuwe na mapitio ya kuona kama malengo yamefikiwa.
3. Suala la kuvunjwa kwa Mkataba pale pande mbili zikishindana liwe wazi kwenye IGA.
4. Suala la eneo lipi bandari ya Dar es Salaam litaendeshwa na kampuni binafsi na bandari zipi zitakuwa sehemu ya uwekezaji huo liwe wazi kuondoa sintofahamu ya bandari zote za Tanzania kuwa chini ya DP World.
5. Suala la “exclusivity” ya kampuni binafsi itakayoendesha bandari kwamba nchi pia iwe na “exclusivity” dhidi ya kampuni hii kuwa na mikataba na bandari shindani na Tanzania. (Yaani kama ambavyo DP World imetaka serikali isiingie makubaliano na kampuni nyingine kuendesha bandari na wao wapewe sharti wasiwekeze kwa bandari shindani za jirani ya Tanzania).

Mapendekezo haya na mengine kama haya yanawatoa watanzania katika mawazo ya mapokeo waliyo yapata katika vyombo vya habari na kuwarejesha katika mjadala wenye maslahi kwa taifa.

MAPENDEKEZO YETU

Mjadala wetu ujikite kwenye kuongeza ufanisi wa bandari yetu ili kuongeza mapato ya serikali, na fedha za kigeni.

Wachumi wanatuambia bandari pekee inaweza kulipa mishahara ya watumishi wote wa Umma na kuhudumia (kulipa), deni la taifa ikiwa itatumika ipasavyo.

Moja ya tafiti inaonesha shehena kubwa ya mzigo, ikiwemo shaba na chuma ipo katika taifa la Congo DRC. Pia mataifa jirani kama Uganda na Rwanda yana shehena kubwa.

Shehena hizo kubwa na endelevu hukusanywa katika bandari kavu iliyopo Rwanda na kusafirishwa kupitia bandari ya Daban Afrika ya Kusini (ambayo iko mbali ukilinganisha na Dar es Salaam Tanzania).

Tunaelezwa mradi wa reli ya kisasa Tatanzania (SGR), ulilenga kunufaika na shehena hiyo kubwa na endelevu kutoka mataifa hayo ya magharibi.

Wawekezaji wa Bandari Kavu ya Rwanda inayokusanya shehena hiyo ni DP World ya Dubai. Kama tulivyosema huko nyuma, mjadala wetu ujikite zaidi kwenye kuongeza ufanisi wa bandari yetu ili kuongeza mapato ya serikali na fedha za kigeni.

Tuungane na Wanzania wanaosema tuboreshe mkataba wa bandari tusonge mbele kwa maslahi ya taifa letu.

SALAM ZA IDD

1. Tunawapongeza Watanzania kwa kuwezeshwa na Mwenyezi Mungu kudiriki Sikukuu tukufu ya Idd ya kuchinja mnyama mwaka huu.

La pili tunawapongeza kwa kujitokeza kujadili na kutoa maoni yao katika jambo muhimu la mkataa wa uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam. Katika Serikali ya Awamu ya Tano wananchi hawakujitokeza kujadili na kuhoji mambo muhimu kama hivisasa. Bila shaka ni kwa hofu ya kutokewa na yale yaliyowakuta akina Ben Saanane, Sheikh Khatbu Yunus, Simon Kanguye, Athumani Ali Kisinga na wengine wengi ambao walipotezwa baada ya kuhoji mambo muhimu kuhusu utawala.

Aidha tunawapongeza kwa kubadili mwelekeo na kuanza kujadili kiuchumi zaidi suala Bandari ya Dar es Salaam na uwekezaji wake.

2. Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita katika suala hili nyeti la mkataba wake na Kampuni ya DP World ya Dubai kwa kuupeleka mkataba huo bungeni ukajadiliwa na wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi.

Katika hili ili tusirudie makosa ya nyuma, tujikumbushe jinsi katiba ya nchi ilivyovunjwa mara kadhaa na serikali kwa kuingia mikataba mikubwa na wawekezaji hasa wazungu bila kuipeleka bungeni ikajadiliwe kama sheria inavyoagiza.

Baadhi ya mikataba ambayo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya hayati Dk. John Pombe Magufuli aliyoingia na wawekezaji bila kuipeleka bungeni:

Mkataba kati ya Tanzania na Barick Gold Corporation ya Canada.

Mikataba hii ni tisa iliyofungwa kati ya Tanzania na Barick (baada ya mgogoro wa kodi kati ya Tanzania na Kampuni ya Acacia ambayo baba yake ni Barick).

Mkataba Huu ulisainiwa Januari 24, 2020 Ikulu. (Katika hatua za utekelezaji iliundwa kampuni ya pamoja ya Twiga ambayo serikali iliachiwa asilimia 16, tu ya hisa.

Hawa Barick wanaendesha migodi mikubwa ya dhahabu ya Buzwagi, North Mara na Bulyanhulu. Ni kampuni kubwa ya dhahabu duniani).

Rais Magufuli hakuona umuhimu wa mkataba huo mkubwa na nyeti kwenye rasilimali kubwa ya taifa kupelekwa kwa wawakilishi wa wananchi bungeni ukajadiliwe. (Tunaelezwa Tanzania ni nchi ya nne kwa uzalishaji wa dhahabu Afrika).

Mkataba kati ya Tanzania na ZL Nickel ya Uingereza

Mkataba huu ulisainiwa Januari 19, 2021, kati ya Tanzania na Kampuni ya ZL Nickel ili kuendeleza mradi wa madini ya Nickel kule Kabanga mkoani Kagera. (Nickel ni madini muhimu kwenye kutengeneza betri ya magari yanayotumia umeme). Kwakua mchakato wake haukupelekwa bungeni na ukafanywa kwa maslahi binafsi, ulisababisha mgogoro ulioigharim sana serikali.

Mradi huu ulikuwa chini ya makampuni mawili ya Barick (ya Canada) na Glencore (ya Uingereza), kabla ya Rais Magufuli kusitisha leseni zao na kuwapa ZL Nickel ya Uingereza.

Katika sintofahamu hiyo, ZL Nickel siku chache tu ilibadilisha jina na kuwa Kabanga Nickel ikiwa na mali za bilioni 16 tu, (sawa na dola za Marekani, milioni 8, wakati mradi umefanyiwa upembuzi yakinifu (Feasibility Study), kwa gharana kuwa ya pesa yetu Tanzania takriban dola milioni 250, (bilioni 500). Kwa hiyo ni sawa na kusema wamepewa bure, na huo pia ulikua mgogoro mkubwa.

Pamoja na ukubwa wa mradi na utata wote huo lakini mradi huo haukupelekwa bungeni kama sheria ya madini ya mwaka 2017, inavyoagiza.

Mkataba mwengine ni wa ujenzi wa bomba la mafuta kati ya Tanzania na Uganda wenye dhamana ya dola bilioni 3.55.

Mradi na mkataba huo chini ya Rais Magufuli na Rais Museveni wa Uganda, haukuwahi kupita bungeni toka mwanzo mpaka ulipokamilika.

Kwa ufupi Rais Magufuli aliingia mikataba mingi ikiwemo mikubwa ya sekta ya madini bila ya kuipeleka bungeni japo sheria ya madini ya 2017 ilimtaka aipeleke Bungeni.

Mifano hii mitatu inatosha kuonyesha ni kiasi gani bunge lilivyodharauliwa na Katiba ya Nchi kuvunjwa huko nyuma.

Ndio maana kwa hili la kulirejeshea uhai na heshma bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaipa kongole serikali kwa hilo.

3. Wananchi wamekuwa na mchango mwingi wa mapendekezo kuhusu Mkataba wa DP World na serikali. Vuguvugu lilikuwa kubwa na wengi walikuwa hawajui hatma ya mawazo yao.

Tarehe 19.06.2023, katika kongamano la kitaifa lililofanyika jijini Dar es Salaam kuhusu suala hilo, mbunge wa Jamhuri ya Muungano Profesa Kitila Mkumbo alifafanuzi kuhusu msimamo wa bunge.

Alisema bunge limejipanga kuzingatia mawazo ya wananchi katika rasimu na hatimaye mkataba halisi.

Wito wetu, tunalishauri bunge lisipuuze mawazo mapya ya wananchi, liyapokee na kuyafanyia kazi.

4. Tunawatakia Watanzania na wengine kote duniani, Sikukuu njema ya Idd ya kuchinja (Adh-ha).

AMIRI SHAABAN IBRAHIM - 0748144720
Ukweli mm mkristo lakini waraka huu umeandikwa kwa weredi
 
Kuna askofu alizungumzia mikataba iliyoingiwa na marais wakiislamu na chuo cha serikali kilichotolewa na Rais mkristu kwa waislamu? Hawa masheikh wamejikita zaidi katika kuonyesha mapungufu yaliyofanyika wakati wa utawala wa marais wakristu kuliko kuonyesha mapungufu ya IGA kati ya Dubai na Tanzania.

Amandla....
Sawa, hata maaskofu nao wakizungumza hisia zao siyo mbaya, Kusema ni kuchagua cha kisema. Kwa sasa tuunganishe nguvu ya pamoja kwenye hili tunalokubaliana. Hayo mengine yanajadilika!. Hebu hisia za "Ngoja nitetee dini yangu kwanza" tuziache kwa sasa tubaki kwenye common ground.
 
Pumba tupu zimejaa humu.
 
Mwaipopo yule aliyepinda kiuno ni bendera fuata upepo anapinga tu wala hana maslahi yoyote zaidi ya Uislamu wa Samia.
 
Sawa, hata maaskofu nao wakizungumza hisia zao siyo mbaya, Kusema ni kuchagua cha kisema. Kwa sasa tuunganishe nguvu ya pamoja kwenye hili tunalokubaliana. Hayo mengine yanajadilika!. Hebu hisia za "Ngoja nitetee dini yangu kwanza" tuziache kwa sasa tubaki kwenye common ground.
Nakubaliana na sentensi yako ya mwisho. Lakini sio vizuri hawa viongozi wa dini wanapozungumzia hisia zao badala ya facts. Maaskofu wakianza kuzungumzia hadharani vitu kama teuzi za waislamu ( wakisahau kuwa wakristu wameteuliwa sana katika nchi hii) watakuwa wanachochea mpasuko katika jamii kuliko kuiunganisha. Kwa bahati mbaya kuna baadhi ya masheikh ambao wanaona kama ni wajibu kila wakati wa kuonyesha kile wanachodai ni dhulma na uonevu unaofanywa dhidi ya waislamu na serikali bila kujali ukweli wa suala husika. Hiyo MoU kati ya serikali ya Rais Muislamu na taasisi za kikristu inatumika sana kujenga chuki katika jamii ya kiislamu dhidi ya wakristu hasa wakatoliki.

Tunatakiwa tuungane katika kuishauri na kuikosoa serikali pale tunapoona bila kujali dini zetu au dini za viongozi wa serikali. Tukiendekeza udini hatutapata mafanikio yeyote.

Amandla...
 
Nawapongeza sana hii shura. Ktk huu mkataba hawajapepesa macho. Hii ndiyo maana ya usomi wa dini. Huwezi kusoma dini halafu uegemee upande usio na tija ktk jamii hasa ktk suala kama la bandari. Naioongeza sana Shura.
WACHATUSEME NA.2

TANZANIA NI YETU SOTE SIO MALI YA WAKRISTO

Hivi karibuni kumezuka mjadala mkali kuhusu Serikali kuingia kwenye makubaliano ya kuendesha Bandari za Tanzania na kampuni ya DP World. Mjadala huu ulianza na sura ya kisiasa wakati Mwenyekiti wa Chadema Bwana Freeman Mbowe alipotoa shutuma kali kuwa Bandari za Tanganyika zinauzwa na Wazanzibari yaani Waziri wa Ujenzi, Mhe Makame Mbarawa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Lakini ghafla mjadala ukahama kwenye Siasa na ukatawaliwa na hisia kali za kidini. Sote tumeshuhudia namna viongozi wa dini ya Kikristo hasa wakatoliki wakiongozwa na Kadinali Pengo walivyokuwa wakilipigia kelele suala la Bandari.

Hoja zinazotawala mjadala huu ni mbili. Hoja ya kwanza ni kwamba mkataba ule umesainiwa na Waziri Mzanzibari na Rais Mzanzibari na kwamba Wanzanzibari hawa wawili wanauza mali za Tanganyika. Hoja yao ya pili inadai kuwa mkataba hauna ukomo wa muda, yaani ni mkataba wa milele. Hii hoja hii ya pili inashabikiwa sana na viongozi wa Kanisa.

Jambo la kushangaza ni kuwa mpaka sasa hakuna hata msemaji mmoja, awe mwanasiasa au kiongozi wa Kanisa aliyetoa hoja za kiuchumi na utendaji za kupinga makubaliano hayo.

Badala yake, viongozi wengine kama vile mama Anna Tibaijuka anadiriki kusema uwongo kuhusu sababu za DP World kukataliwa kuendesha Bandari za Marekani. Mama Tibaijuka anajua vyema lakini hakutaka kusema kuwa sababu ya kukataliwa kuongoza Bandari za New York na New Jersey ni Uwarabu wao na wala si utendaji wao.

Ni kweli Bunge la Marekani lilikataa DP World wasipewe Bandari hizo lakini walisema wazi kuwa Marekani haiwezi kuwapa Waarabu kuendesha Bandari zao kwa sababu za kiusalama. Hakuna asiejua msimamo wa Marekani kuhusu Waarabu na Waislamu.

Kwa makusudi kabisa, mama huyu anapotosha watu kwa kufananisha suala la Bandari za Marekani na Bandari za Dar es Salaam. Kwenye suala la Dar es Salaam, DP World haikutaka kununua TPA. Inachopendeza ni kuendesha na si kununua Bandari ya Dar es Salaam.

Suala hili la kuendesha si geni Tanzania. Kampuni ya TICTS imeendesha Bandari ya Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 20. Kampuni ya “Swissport” inaendesha Kiwanja cha Ndege cha Dar es Salaam kwa muda mrefu. Mbona hizi kelele hatukuzisikia?

Wakati wa utawala wa Donald Trump Marekani ilifika hatua ya kupiga marufuku baadhi ya Mataifa ya Arabuni kwa maana Waislamu kuingia Marekani. Kwa hiyo mama Tibaijuka hakutaka kuwa mkweli kuhusu suala hili.

Ametumia kivuli chake cha kuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwa wakati ule kuwaaminisha Watanzania kuwa yeye anafahamu zaidi kuhusu ubaya wa DP World.

Mama Tibaijuka amekosa uadilifu (moral authority) wa kuweza kukemea kile alichokiita mkataba mbovu kwa sababu wakati kampuni ya TICTS iliyokuwa inaendesha Bandari ya DSM kwa utendaji wa hovyo huyu mama alikaa kimya hata pale ambapo TICTS walipopewa nyongeza ya mkataba wa miaka 15 bila kufuata sheria za manunuzi.

Lakini jambo la pili, nani asiyejua kuwa mama Anna Tibaijuka alikiri hadharani kuwa alipokea shs 1.6 bilioni ya fedha za rushwa za ESCROW? Huyu mama ambaye alisema kwa majigambo kuwa shs 1.6 bilioni ni pesa ya mboga ana uchungu gani wa kuwatetea Watanzania masikini?

Bado tunarejea kusema tena kwa kinywa kipana, mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja aliyesema kwa kuonesha ushahidi kuwa DP World hawana uwezo kifedha au utendaji wao ni mbovu. Hakuna aliyesema kuwa hizo fedha ambazo tunaahidiwa ni ahadi hewa kwa sababu DP World hawana uwezo wa kuvutia mizigo kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa kuwa mjadala umetawaliwa na CHUKI za kidini na wasemaji wakubwa wamekuwa viongozi wa Kanisa. Tukumbuke kuwa ni Wakristo hao hao ambao mmoja kati ya viongozi wao waliosema kuwa Rais Samia anafanana na muuza vitumbua! Makanisa hawakukemea kauli hii ya kumkosea adabu Rais.

Kwa kuwa mjadala wa Bandari una chuki za udini, naomba tujikumbushe nafasi ya Makanisa katika nchi hii.

TUKUMBUKE MWAKA 1992

Mwaka 1992, Serikali iliingia Mkataba na Makanisa kupitia Taasisi zao za TEC na CCT. Chini ya Makubaliano yale, hospitali za Makanisa zitatumika kwa wananchi wote pale ambapo Serikali haina hospitali.

Kwa kufanya hivyo, Serikali itakuwa na wajibu wa kuyapa Makanisa fedha za kuendesha hospitali hizo ingawa umiliki wa hospitali utabaki kuwa wa Makanisa.

Ifahamike kuwa fedha hizo zinatokana na kodI za Watanzania wote; Waislamu, Wakristo, Mabaniani, Magoha, Makadiani, na hata wale wasio na dini.

Nini athari za Mkataba huu ? Mkataba huu wa kibaguzi una athari nyingi. Kwanza:

Serikali inatumia kodi za wananchi kuyapa Makanisa kuendesha shughuli zake za kuimarisha Ukristo.

Tunasema hivyo kwa sababu utaratibu unaotumika ni kuwa Serikali inatoa fedha kwa Makanisa ambayo wao ndio wanapanga matumizi ya fedha zile na sio Serikali.

Pili, kwenye Jamii, Makanisa yanaonekana ndio yanatoa huduma za Jamii na hivyo kujenga saikolojia kwa wananchi kuwa Ukristo ndio unajali wananchi.

Athari ya tatu ni kuwa Makanisa yananyonya wananchi kwa sababu pamoja ya kuwa hospitali zile zinapata fedha kutoka Serikalini, bado wananchi wanalipia huduma.

Nne, Mkataba hauna ukomo, yaani ni wa milele. (Wakristo wataendelea kupewa hayo mabilioni na Waislamu watanyimwa milele).

Kwa tafsiri nyingine ni kuwa Serikali imejivua kwenye wajibu wa kutoa huduma za Jamii na kuchagua Makanisa kuwa ndio wakala wake.

Tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa wakati Mkataba huo unasainiwa aliyesaini Mkataba ni Bwana Edward Lowassa aliyekuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu. Huyu ni Mkristo

Kwa utaratibu wa Serikali, Lowassa alikuwa Waziri wa Nchi, hivyo basi Waziri mwenye dhamana ni yule mwenye ofisi yake kwa maana ni Waziri Mkuu.

Wakati unatiwa saini Mkataba, huo Waziri Mkuu alikuwa John Samwel Malecela ambaye ni Mkristo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndie aliyeishauri Serikali isaini Mkataba ule ambao kwanza hauna ukomo (mkataba wa maisha) na pili unatumia kodi za wananchi kuimarisha Ukristo alikuwa Damian Lubuva ambaye ni Mkristo.

Kwa upande wa Kanisa mwanasheria wao alikuwa Prof Balozi Costa Mahalu, Mkristo.
Kwa maana hiyo, upande wa Serikali, Mkataba ule umeasisiwa na kusimamimwa na Wakristo watupu. Waziri wa Nchi Mkristo, Waziri Mkuu Mkristo, Mwanasheria Mkuu Mkristo.

Ni Wakristo! Wakristo! Wakristo!

Kama kwenye hoja ya makubaliano ya Bandari ni Wazanzibari wawili (ambao ni Waislamu) wamesaini makubaliano ya kuiuza Tanganyika, Mbona Waislamu hawakulalamika pale Wakristo 3 wazito Serikalini walipobuni mbinu za kutumia kodi za wananchi kuimarisha dini yao Ukristo Tanzania?

Kama hoja ni ukomo wa mkataba, mbona Mkataba huu wa Serikali na Makanisa hauna ukomo? Ni mkataba wa milele na ndio maana mpaka leo (miaka 30 sasa) bado unaendelea kutumika.

Bado Serikali inaendelea kutekeleza Mkataba wa kibaguzi ambapo inatumia kodi za wananchi wote kuimarisha shughuli za Kanisa.

USHAHIDI

Tarehe 23 Januari 2019, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa dini zote IKULU. Kwenye Mkutano ule Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tanga Bwana Maimo Mndolwa alilalamika kwa Rais Magufuli kuwa Serikali inavunja Mkataba kwa kujenga hospitali kwenye maeneo ambayo Kanisa imeachiwa kuwa na hosptali ambazo zinapewa fedha na Serikali.
Amelalamika hivyo kwa sababu Mkataba wa Makanisa na Serikali hauna ukomo. Kila penye hospitali ya Kanisa, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali yake. Badala yake, Serikali inatakiwa kuendelea kutoa fedha za kodi kuwapa Makanisa ili ziendeshe hospitali zao na kuimarisha Ukristo kwa kutumia jasho la Watanzania.

Katika kusisitiza madai yake, Askofu Mkuu alitoa ushahidi wa hospitali zilizojengwa na Serikali katika Wilaya ya Ifakara, Ngara na Muheza ambazo kwa mujibu wa Mkataba wa 1993, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali hizo za Wilaya.

Kitendo cha Serikali kujenga hospitali hizo kinatafsiriwa na Kanisa kuwa Serikali imevunja Mkataba kwa sababu sasa inatoa huduma hiyo muhumu kwa wananchi.

Askofu Mkuu alifafanua kua matatizo haya yapo kwenye ngazi ya Wilaya kwa sababu kwenye ngazi za juu, hakuna tatizo kwa kuwa kuna Msimamizi anaesimamia Mkataba huo.

Hapa Askofu Mkuu alikuwa ana maana kuwa hospitali za KCMC ya Moshi, Bugando ya Mwanza na CCBRT ya Dar es Salaam ambazo zote ni mali ya Kanisa bado zinaendelea kupata fedha za kodi huku zikiendelea kuwalipisha wananchi kwa huduma wanazopewa kwenye hospitali hizo.

Rais Samia Suluhu Hassan alifanya Mkutano na Baraza la Maaskofu la Kanisa Katoliki Tanzania uliofanyika Kurasini tarehe 25 Juni 2021. Katika risala yao, Baraza la Maaskofu limeilaumu Serikali kwa kujenga hospitali zake kinyume cha Mkataba wa 1992, na Makanisa.

Kwenye risala hiyo, Baraza la Maaskofu limeshangaa kuona Serikali inajenga hospitali kwenye Wilaya ambazo Makanisa tayari yana hospitali zao. Wamehoji kwa nini kuwepo na ushindani wa kutoa huduma hizo?

Kwa maana nyepesi, kwa nini Makanisa yasiachiwe kuendesha hospitali maisha (milele) na kuendelea kupewa ruzuku zinazotokana na kodi za wananchi?

Risala hiyo ni ya chombo cha juu kabisa katika Kanisa Katoliki ambao leo viongozi hao hao wanaohoji na kulalamika kuhusu makubaliano ya Serikali na DP World kuwa hayana ukomo!

Kanisa hilo hilo ambalo linapiga kelele kuhusu mkataba wa Serikali na DP World, ndilo ambalo kiongozi wake Askofu Method Kilaini alipewa shs. 80.9 milioni, Askofu Eusebius Nzigirwa alipewa shs. 40.4 milioni na Mchungaji Alphonce Twimanye Simon alipewa shs 40.4 milioni fedha za Rushwa zilizotokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta ESCROW.

Hadi leo Kanisa halijatangaza hadharani hatua za kinidhamu iliyowachukulia viongozi hao. Ukimya huu tuutafsiri vipi? Kwa ukimya huu, Kanisa linapata wapi “moral authority” ya kupinga mkataba wa DP World.

Watanzania hawajasau wakati wa utawala wa Magufuli wameshuhudia mauwaji kule Kibiti na Rufiji ambayo ni Wilaya zenye Waislamu wengi. Watanzania bado wanakumbuka viroba vyenye miili ya watu vilivyokuwa vinaokotwa Coco Beach kila uchao.

Kanisa lilikuwa wapi wakati Magufuli anatoa roho za watu wasio na hatia? Masheikh wangapi wamepotea ambao mpaka leo hawajulikani walipo wakati wa utawala wa Magufuli?

Hao waliobahatika wametoka jela wakiwa vilema kama alivyo Sheikh Abdallah Maginga Wambura ambaye kakatwa mguu kutokana na vipigo vya Polisi?

Yuko wapi mwanasiasa Ben Saanane ambaye “kosa” lake ni kuandika kuwa PhD ya Magufuli ni feki? Yuko wapi Mwandishi Azory Gwanda ambaye “kosa” lake lilikuwa kuandika ukweli kuhusu mauwaji ya Kibiti?

Wakati wa utawala wa Magufuli, Mbunge wa Kilwa Kusini Mhe Selemani Bungara maarfu “Bwege” aliwahi kusema Bungeni kuwa raia wake walichukuliwa na askari msikitini na wamepotea mpaka leo hawajulikani walipo. Kanisa halikuyaona haya?

Kama Kanisa ilifumbia macho udhalimu na ukatili huu, leo wanapata wapi mdomo wa kukemea hicho wanachokiita mkataba usio na maslahi kwa wananchi?

Ni wananchi gani hao ambao leo Kanisa linajifanya kuwatetea?

Saa Watanzania wanakumbuka kuwa pamoja na ukatili wote wa Magufuli, ni viongozi hao hao wa Kanisa waliokuwa wakimkaribisha kila Jumapili kwenye Makanisa yao na kumpa nafasi ya kuzungumza. Leo Kanisa linataka kuwadanganya Watanzania kuwa lina maslahi na wananchi?

Kuna kitu kikubwa zaidi ya uhai? Wakati watu wanatolewa roho zao na Magufuli Kanisa lilikuwa wapi?

KWANINI WAKRISTO WANAPINGA MKATABA WA BANDARI

Mpaka sasa si Makanisa wala Wanasiasa ambao wametoa hoja ya kiuchumi. Tofauti na Wamarekani ambao walisema hadharani kuwa hawawezi kuwapa Waarabu kuendesha Bandari zao, hapa Tanzania sababu haswa ya kupinga Mkataba haisemwi hadharani.

Vinatafutwa visingizio tu. Ukweli ni kuwa Mkataba wa Bandari unapingwa na kuwepo kwa fikra potofu za Kanisa kuwa:

Iwapo DP World watapewa zabuni ya kuendesha Bandari, uwepo wao Tanzania utawanufaisha Waislam kwa namna moja au nyingine.

Kuna wanaohofia kuwa iwapo Bandari itafanikiwa, na endapo itatokea fursa ya miradi mingine mikubwa ya kiuchumi, Dubai watakuwa na nafasi nzuri ya kupewa miradi hiyo. Kwa hiyo kuwepo kwao kutaimarisha Uislamu.

Ikiwa DP World watapata tenda ya Bandari, nchi itapata mafanikio makubwa ya kiuchumi ambayo kwa fikra zao potofu yatakuwa yameletwa na Rais Mwislamu. Kwa maana hiyo, Waislamu wanaweza kuongoza nchi kwa ufanisi. Tayari kuna watu wanaosema kuwa Samia awe Rais wa mwisho Mwislamu Tanzania

Kuna wanaosema Bandari ikipata mafanikio itaonekana kuwa kumbe Wanawake wanaweza kuongoza nchi vizuri
Kuna wasemao kuwa Bandari ikifanikiwa itaonekana Wanzanzibari nao wana uwezo sawa na wa Bara katika kuliongoza taifa letu.

Hoja zote hizo ni za kipuuzi. Mafanikio yakiletwa na Rais Mwislamu au mwanamke au Mzanzibari wataonufaika ni wananchi wote.

Fedha za Bandari zitawanufaisha WOTE kwani anaepanga matumizi ya fedha ni Bunge letu ambalo lina Wabunge Waislamu, Wakristo na wasiokuwa na dini.

MWISHO

Nchi hii Waislamu wamekuwa wakidai kuwa Tanzania ni NCHI YETU SOTE

Waislamu wamekuwa wakidai kuwa idadi yao ni kubwa

Waislamu wanajigamba kuwa wamesoma lakini hawapewi fursa sawa

Kinachoshangaza ni kuwa tokea Mjadala wa Bandari uanze na hata mijadala mingine inayohusu UDINI huwasikii Waislamu kusema lolote. Wao ni kimyaaaaaaaaaa.

Mjadala wa Bandari umetawaliwa na viongozi wa dini ya Kikristo, Wasomi Wakristo, Taasisi za Kikristo na hata wanasheria waliofungua kesi Mahakamani ni Wakristo.

Kwenye mjadala wa Bandari kuna mafunzo kwa Waislamu.

MWENYEZIMUNGU ASHUHUDIE TUMEFIKISHA
 
U nailed it
 
Mnaoleta udini katika hili suala la bandari mmepotea njia.

Ishu ya MoU ya Taasisi za Kanisa na serikali kwenye mambo ya Afya ni tofauti sana na ishu ya bandari.

Kwanza Makanisa ya Tanzania ni watanzania sisi kwa sisi kwa hiyo tutakabana mashati sisi kwa sisi kama amvavyo imekuwa siku zote ktk hii ishu. Ila hawa DP World ni wageni, Hatuwezi kukubali nchi yetu igawiwe kwa wageni!

Mkataba una matobo mengi, ya kisheria na hata kiuchumi masna hauweki wazi hata share zetu katika faida ya kuendesha hiyo bandari ni sh ngapi.

Sasa mnapoleta habari za MoU kati ya serikali na Kanisa, kwenyejadala huu mmepotea njia.
 
What do you want to justify? Kwamba pesa za ummah ziendelee kuimbia na kanisa kwasbb ni watanzania wenzetu? Ungejua kwamba kanisa ina utii na upendo kwa Vatican kuliko Raisi wa hamhuri usinge sema hayo. Wizi mbaya na hatari ni wandani.........kanisa inaibia na inaendelea kuibia serikali kwa kujificha kwenye mgongo wa kutoa huduma bure wakati huduma zao sio za bure.
 
Ni yepi maoni yako, Je unakubaliana na hoja za TLS, Shura ya Maimamu, Profesa Shivji, Jaji Warioba kuwa mkataba wa Bandari una matatizo urekebishwe?
 
Wasiishie kwenye huo mkataba wa bandari tu kuna mikataba mingi inayo tuingizia hasara na aina kikomo kabisa, na hamna anae taka kuileta hadharani........kwanini serikali iendelee kupoteza pesa wakati huo mkataba wanaweza kubadilishwa sasa muaka zaidi ya 30 kanisa inaendelee kuxhukua pesa ya ummah, hao watu wakanisa hawana moral authority kuongelea mkataba wa bandari wote ni wezi
 
Umeeleza mengi lakini hujazungumzia content za mkataba na kile kinacholalamikiwa.Sanasana andiko lako limetawaliwa na hisia na mapenzi ya dini na blah blah za kila siku za waisalamu
 
Wasiishie kwenye huo mkataba wa bandari tu kuna mikataba mingi inayo tuingizia hasara na aina kikomo kabisa, na hamna anae taka kuileta hadharani........kwanini serikali iendelee kupoteza pesa wakati huo mkataba wanaweza kubadilishwa sasa muaka zaidi ya 30 kanisa inaendelee kuxhukua pesa ya ummah, hao watu wakanisa hawana moral authority kuongelea mkataba wa bandari wote ni wezi
Kama unaunga mkono mkataba wa bandari urekebishwe basi tuko pamoja.

Hayo ya MoU ya kanisa na serikali sisi wenyewe tutakabana mashati humuhumu kwa namna itakavyokuwa LAKINI hili la bandari kupewa mgeni kwa terms zile, tuungane kulikataa. Tusikubali kugawanywa!
 
Mimi napenda mikataba yote kama huo wakanisa ijadiliwe tuone mapungufu yake kwanini aina kikomo, mpaka lini serikali isaidiwe na kanisa......mwizi ni mwizi awe wa ndani au wa nje ila wa ndani ni hatare zaidi.
 
Kwenye hili la serikali kutoa ruzuku kwa hospitali zinazomilikiwa na Kanisa, mbona siyo tatizo. Ifahamike kuwa wala halikuwa ombi la Kanisa kuwa na hiyo memorandum.

Hilo lilikuja pale Serikali ilipotaka hospitali za Kanisa zitumike kama hospitali za rufaa. Kwa hiyo kwenye hospitali hizo ambazo hazikuhitaji kuwa hospitali za rufaa, zikabebeshwa mzigo wa kubeba majukumu ya Serikali.

Na haikuwa maamuzi ya Kanisa, bali wataalam wa afya ndio waliopendekeza ni hospitali zipi zimefikia viwango vya kuwa hospitali za rufaa. Na ninaamini kama kungekuwa na hospitali yoyote inayoendeshwa na BAKWATA iliyokuwa imefikia viwango vilivyokuwa vinatakiwa, ingejumuishwa.

Tena hayo yalifanyika wakati Rais akiwa muislam. Na sahizi Rais ni muislam. Kama waislam wana duku duku kwenye hili, mbona wanaweza kuivunja hizo MoU, na hospitali zikarudi kwenye mfumo wake wa zamani. Tena hapo zamani, kabla ya Serikali kujiingiza humo, huduma zilikuwa bora zaidi, na hata msongamano wa wagonjwa haukuwa mkubwa kama ulivyo sasa.
Well said
 
Back
Top Bottom