MJADALA WA BANDARI KATI YA WANANCHI NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI (G.Msigwa)
01 Julai, 2023
SEHEMU YA KWANZA (01).
G. MSIGWA: Kumekuwa na Upotoshaji juu ya Makubaliano haya, Leo Mtajua mbivu na Mbichi Kuhusu Mkataba wa Bandari.
WANANCHI: Aaaahh! Kwani Kati ya Ninyi watu wa Serikali na Wananchi nani Mpotoshaji?😒
G. MSIGWA: Maswali yenu yote yatajibiwa na Wakili wetu Msomi Ndugu Mohamed.
WANANCHI: Sawa, Tunaweza Kuanza?
MSIGWA: Karibuni
(Maswali ya Mwana CHAMA Wa CHADEMA STUDENTS' ORGANIZATION (CHASO))
MWANA CHASO: Katiba kama Sheria mama ya Nchi, inasema Bandari zote zipo chini ya Serikali ya Muungano, Kwanini Mkataba Huu Unaziweka Bandari za Tanganyika peke yake chini ya Serikali ya Dubai kupitia Kwa DPW?
MSIGWA: Zanzibar Wanajitegemea kupitia mamlaka zao za Bandari Kwa mujibu wa sheria😟
MWANA CHASO: Kaka Ulisema Maswali ya Kisheria atajibu Wakili Mudi. Hebu Mwache Ajibu🤒
MSIGWA: Sikiliza, huu Mkataba ni kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai, chini ya Mamlaka ya bandari za Tanzania TPA na DP World. huelewi Nini hapo?
MWANA CHASO: 😒 Tufanye nimeelewa. Hebu nipatie kirefu Cha TPA Ndugu Msemaji.
MSIGWA: Ni Tanzania Port Authority. Ikiwa na maana Mamlaka ya Bandari Tanzania.
MWN. CHASO: Asante Kwa jibu zuri. Kama nakuelewa, Ukisema TANZANIA Unamaanisha Kote, yaani Bara na visiwani. Sasa turudi kwenye Swali langu, Ni kwanini Mkataba haujumuishi na Bandari za Zanzibar?😎
MSIGWA: Eeem. Aaaam la. la. Lakini, Hebu Wakili Mohammed Mweleweshe huyu.
WANANCHI WOTE: Vicheko 😂😂😂😂😂😂
WAKILI MUDI: Kutokana na Makubaliano ya Kimataifa, Miaka ya 1980 hadi 1990 Zanzibar ilianzisha Sheria zilizoipatia Mamlaka ya Kuendesha Bandari zake. Hivyo, ndiyo maana Haija jumuishwa katika Mkataba Huu.
MWN. CHASO: Wakili, nataka kufahamu kati ya Kifungu Cha Sheria, na Ibara ya Katiba, ni kipi Chenye Mamlaka zaidi ya Kingine?
WAKILI MUDI: Kwa kawaida, Katiba ndiyo yenye Mamlaka.
MWN CHASO: Sasa nataka kufahamu, kati ya Katiba inayosema Bandari zote zipo chini ya Serikali ya Muungano, na Hizo Sheria zinazosema Zanzibar iendeshe Bandari zake, ni ipi inapaswa kuheshimika na Kufuatwa?😒
WAKILI MUDI: 😥Ki. ki. kiukweli hapo Kuna Madhaifu, lakini...
MWN. CHASO: Hamna Cha lakini, Tuambie Kati ya Katiba, na hizo Sheri zinazokinzana na Katiba ni kipi kinastahili kufuatwa!?😎
MSIGWA: Tusikilizane, twende Taratibu. Wewe Ulishawahi kuona wapi TPA imesimamia Bandari za Zanzibar?🥵
MWN. CHASO: Kaka Msigwa, Mimi ni Mwanafunzi wa Sheria, Namuuliza Mwanasheria Mwenzangu Ili anijibu Kisheria. ila kama na wewe ni Mwanasheria, Tafadhali tujibu Kisheria🤒
MSIGWA: Wewe unaelezwa vizuri hutaki Kuelewa, Inatosha Kaa chini na wengine waulize Maswali😡
WANANCHI WOTE: Aaaahh hakunaa Ajibiwe.!!!! Ajibiwe.!!!
Maelewano yakakosekana na Swali halikijibiwa. Wengine Wakapewa Nafasi ya Kuuliza Maswali. Kuutetea uovu ni Kazi NGUMU Sana😂😂
"CHASO - Chanzo Cha Fikra Bora ✊🏼✌🏼"
Dedan Chacha Wangwe
Mwanafunzi wa Sheria.
Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na
👆🏾Akili kubwa sana. Msigwa na vibaraka wake wajitafakari. Wakubali ushauri wa Professor Issa Shivji warudi bungeni warudie matapiko yao.