Shura ya Maimamu yataka Mkataba wa Bandari Uboreshwe na haki itendeke kwa Makumi ya Masheikh walioko Jela nchi nzima

Tena ulipaswa kushukuru izo hospital za kanisa ukienda unapatiwa matibabu ya viwango.Hospital za serikali unazoenda umeona huduma zilivyo mbovu .
 
Umesema ukweli sana humu ndani congrats mkuu
 
Kweli akili ni muhimu sana we unaona serikali ikivunja mkataba na kanisa kwenye utoaji huduma za afya na elimu watakaoumia ni rai wakristo peke yao?
 
Hizi hoja za uislamu na ukristo tungeziacha tujadili mustakabari wetu kama taifa kwanza mwishi wa siku wote tunahitaji huduma nzuri za afya ,elimu barabara,umeme n.k
 
Kweli akili ni muhimu sana we unaona serikali ikivunja mkataba na kanisa kwenye utoaji huduma za afya na elimu watakaoumia ni rai wakristo peke yao?
Sio uvunjwe upitiwe upya na uwekewe kikomo kwanini uwe wa milele? Hapo kuna unyonyaji kwa raia
 
Hata wakijenga hospital zao swala la usimamizi zikaleta kwa wananchi ni issue nyingine aisee acheni tu makanisa yatupatie huduma tuache chuki.
Kati ya hospital za kanisa na serikali zipi zinatibu wengi!?..na Kwa nini serikali itie ruzuku kwenye biashara za kanisa!?
 
Tena ulipaswa kushukuru izo hospital za kanisa ukienda unapatiwa matibabu ya viwango.Hospital za serikali unazoenda umeona huduma zilivyo mbovu .
Kwa hiyo kwa kuwa saint Mary's sec schools zinafanya vizuri basi serikali itie ruzuku!?
 
FaizaFoxy tumia ule muda wa kuwasengenya majirani kusoma haya madini kutoka kwa masheikh.
Halafu ingekua vizuri Kama ungefuata dini moja wapo kuliko kuabudu binadamu wenzio.
 
Kumekucha

Sasa Mkataba wa Bomba la Mafuta tuliambiwa na Katibu Mkuu wa Chadema mh John Mnyika kwamba Shujaa Magufuli aliupeleka bungeni mwaka 2017 na ulijadiliwa na kuridhiwa

Naomba ufafanuzi hapo alhaj FF wa Jf!
Ni kweli ulijadiliwa. Ngoja nipekue kmbukumbu za bunge
 
Mimi napenda mikataba yote kama huo wakanisa ijadiliwe tuone mapungufu yake kwanini aina kikomo, mpaka lini serikali isaidiwe na kanisa......mwizi ni mwizi awe wa ndani au wa nje ila wa ndani ni hatare zaidi.
Mimi napenda waisilamu nao waingie mkataba usio na ukomo kihudumia jamii kama ilivyo kwa wakristu
 
Punguza chuki zenye chembechembe za udini ili tuunganishe nguvu tunusuru bandari yetu. Tukishakomboa bandari unaweza kuendelea na chuki zako kwa kadri utakavyoweza

Hao sura ya imamu asilimia 80 ya hoja zao zimejikita kuhoji mikataba ya kanisa na serikali pia urasimishaji uliofanyika katika serikali za awamu ya 4,kimsingi wamejificha kwenye kichaka cha kuhararisha mkataba wa dpw indirect.
 

Hii ndio dhamira yenu kuu kupotosha na kuleta hoja za kipuuzi,hakuna anayekataa muwekezaji ila mikataba hii imekua ya kipuuzi na kisenge mbona hamuongelei mkataba na vipengele vyake mkaa kusema mara ukristo mara uslamu,mpuuzi wewe.
 
Hao sura ya imamu asilimia 80 ya hoja zao zimejikita kuhoji mikataba ya kanisa na serikali pia urasimishaji uliofanyika katika serikali za awamu ya 4,kimsingi wamejificha kwenye kichaka cha kuhararisha mkataba wa dpw indirect.
Soma vizuri sana hilo andiko, wamesema wazi kuwa wanaungana na Watanzania wanaotaka mkataba huu wa bandari urekebishwe.

Hayo mengine waachie wenyewe. Tuungane katika linalotuunganisha.
 
MJADALA WA BANDARI KATI YA WANANCHI NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI (G.Msigwa)

01 Julai, 2023

SEHEMU YA KWANZA (01).

G. MSIGWA: Kumekuwa na Upotoshaji juu ya Makubaliano haya, Leo Mtajua mbivu na Mbichi Kuhusu Mkataba wa Bandari.

WANANCHI: Aaaahh! Kwani Kati ya Ninyi watu wa Serikali na Wananchi nani Mpotoshaji?😒

G. MSIGWA: Maswali yenu yote yatajibiwa na Wakili wetu Msomi Ndugu Mohamed.

WANANCHI: Sawa, Tunaweza Kuanza?
MSIGWA: Karibuni

(Maswali ya Mwana CHAMA Wa CHADEMA STUDENTS' ORGANIZATION (CHASO))

MWANA CHASO: Katiba kama Sheria mama ya Nchi, inasema Bandari zote zipo chini ya Serikali ya Muungano, Kwanini Mkataba Huu Unaziweka Bandari za Tanganyika peke yake chini ya Serikali ya Dubai kupitia Kwa DPW?

MSIGWA: Zanzibar Wanajitegemea kupitia mamlaka zao za Bandari Kwa mujibu wa sheria😟

MWANA CHASO: Kaka Ulisema Maswali ya Kisheria atajibu Wakili Mudi. Hebu Mwache Ajibu🤒

MSIGWA: Sikiliza, huu Mkataba ni kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai, chini ya Mamlaka ya bandari za Tanzania TPA na DP World. huelewi Nini hapo?

MWANA CHASO: 😒 Tufanye nimeelewa. Hebu nipatie kirefu Cha TPA Ndugu Msemaji.

MSIGWA: Ni Tanzania Port Authority. Ikiwa na maana Mamlaka ya Bandari Tanzania.

MWN. CHASO: Asante Kwa jibu zuri. Kama nakuelewa, Ukisema TANZANIA Unamaanisha Kote, yaani Bara na visiwani. Sasa turudi kwenye Swali langu, Ni kwanini Mkataba haujumuishi na Bandari za Zanzibar?😎

MSIGWA: Eeem. Aaaam la. la. Lakini, Hebu Wakili Mohammed Mweleweshe huyu.

WANANCHI WOTE: Vicheko 😂😂😂😂😂😂

WAKILI MUDI: Kutokana na Makubaliano ya Kimataifa, Miaka ya 1980 hadi 1990 Zanzibar ilianzisha Sheria zilizoipatia Mamlaka ya Kuendesha Bandari zake. Hivyo, ndiyo maana Haija jumuishwa katika Mkataba Huu.

MWN. CHASO: Wakili, nataka kufahamu kati ya Kifungu Cha Sheria, na Ibara ya Katiba, ni kipi Chenye Mamlaka zaidi ya Kingine?

WAKILI MUDI: Kwa kawaida, Katiba ndiyo yenye Mamlaka.

MWN CHASO: Sasa nataka kufahamu, kati ya Katiba inayosema Bandari zote zipo chini ya Serikali ya Muungano, na Hizo Sheria zinazosema Zanzibar iendeshe Bandari zake, ni ipi inapaswa kuheshimika na Kufuatwa?😒

WAKILI MUDI: 😥Ki. ki. kiukweli hapo Kuna Madhaifu, lakini...

MWN. CHASO: Hamna Cha lakini, Tuambie Kati ya Katiba, na hizo Sheri zinazokinzana na Katiba ni kipi kinastahili kufuatwa!?😎

MSIGWA: Tusikilizane, twende Taratibu. Wewe Ulishawahi kuona wapi TPA imesimamia Bandari za Zanzibar?🥵

MWN. CHASO: Kaka Msigwa, Mimi ni Mwanafunzi wa Sheria, Namuuliza Mwanasheria Mwenzangu Ili anijibu Kisheria. ila kama na wewe ni Mwanasheria, Tafadhali tujibu Kisheria🤒

MSIGWA: Wewe unaelezwa vizuri hutaki Kuelewa, Inatosha Kaa chini na wengine waulize Maswali😡

WANANCHI WOTE: Aaaahh hakunaa Ajibiwe.!!!! Ajibiwe.!!!

Maelewano yakakosekana na Swali halikijibiwa. Wengine Wakapewa Nafasi ya Kuuliza Maswali. Kuutetea uovu ni Kazi NGUMU Sana😂😂

"CHASO - Chanzo Cha Fikra Bora ✊🏼✌🏼"


Dedan Chacha Wangwe
Mwanafunzi wa Sheria.
Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na
MRATIBU CHASO-DSM.

👆🏾Akili kubwa sana. Msigwa na vibaraka wake wajitafakari. Wakubali ushauri wa Professor Issa Shivji warudi bungeni warudie matapiko yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…