Huu Sasa Ndio Uislam, sio ule Uhuni wa Kutangaza Amani Amani huku HAKI imefichwa.
Ni sawa tule twanafunzi, Kila kukicha "Mama asamewe" alafu tunashindwa hata kukaa na kujadili Report ya CAG.
====
Shura ya Maimamu Tanzania ikiongozwa na
Sheikh Ponda Issa Ponda imengumza kuhusu;
Kutoweka kwa Hisia za Ubinadamu
"Kutoweka kwa hisia za ubinadamu ni tatizo kubwa linaloukabili ulimwengu sasa. Hapa Tanzania, unaweza kufahamu ukubwa wa tatizo hilo ikiwa utaenda katika hospitali za serikali. Masikini anayetoka nyumbani kufuata matibabu na kurudi nyumbani hutozwa laki 2 kila siku kwa ajili ya kusafisha figo. Ikiwa hana pesa hizo, hapewi huduma hiyo pamoja na kufahamika kwamba akikosa huduma hiyo kwa muda mfupi atavimba na kupoteza maisha."
"Masikini wengi Tanzania hufariki dunia majumbani mwao kwa kushindwa gharama za matibabu. Aidha, yule aliyemudu gharama za kulazwa katika hospitali hizo kisha akaishiwa pesa na kufariki dunia, serikali huzuia mwili wake mpaka deni lilipwe."
"Serikali ya Tanzania inamdai maiti masikini mpaka shilingi milioni 50 na kuzuia mazishi yake mpaka pesa hiyo ilipwe."
Hali ya Usalama
"Matarajio ya usalama kwa jamii yoyote ni kuwa salama katika taifa lao. Hata hivyo, baadhi ya wananchi wamekuwa wakiishi kwa mashaka makubwa. Hali hiyo imeimarishwa zaidi baada ya serikali kuunda sheria inayoitwa ya
'kupambana na ugaidi'. Mswada wa sheria hiyo ulipowasilishwa bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2002, wabunge wengi walionya kwamba umetoka Marekani na utaligawa taifa kwa kuwa umelenga dini mahsusi ya Uislamu."
"Madai hayo ya wabunge yamethibitika kwa hali ya Waislamu Tanzania kuwa mbaya mno kiusalama. Wengi wameuawa na mamia wamewekwa magerezani chini ya sheria hiyo. Wamewekwa gerezani kwa zaidi ya miaka 10 bila ya kuthibitishwa tuhuma zao. Achilia mbali mamia ya waliopotezwa, wale ambao waliwekwa gerezani kwa miaka mingi, baadhi yao hufariki dunia kutokana na mateso wanayoyapata wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola."
Maisha ya Watanzania na Uongozi Bora
"Maisha yetu kama Waislamu na Watanzania yanahitaji uongozi bora ili tuishi kwa hadhi ya binadamu kama alivyokusudia Mwenyezi Mungu. Tunahitaji uongozi na serikali bora yenye misingi ya haki iliyopatikana kwa ridhaa ya wananchi na inayowajibika kwa watu wa taifa lake. Tunahitaji serikali inayoheshimu sheria, inayotambua na kuheshimu uhai na uhuru wa watu wake katika nyanja zote za maisha."
"Mwaka huu Tanzania ni mwaka wa uchaguzi. Oktoba 2025, wananchi watapiga kura kuchagua Rais, Wabunge, Madiwani, na kwa Zanzibar, Wawakilishi. Aidha, msingi wa kufaulu kwa tukio hili kubwa ni maelewano ya kijamii, kisheria, na kisiasa. Maelewano hayo huzaa msingi mwingine muhimu ambao ni amani kabla na baada ya uchaguzi."
Hali ya Kisiasa
"Hali ya kisiasa nchini inaonyesha maelewano kati ya jamii na serikali hayapo. Jamii ilitoa maoni yao ya
Katiba Mpya ya Taifa lakini serikali imeyazuia. Maelewano ya kisheria pia hayapo; mfano, Bunge lilifuta sheria inayoruhusu
TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024 na kuagiza usimamiwe na
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, lakini serikali ilifumba macho.
"Maelewano hayo pia hayapo kati ya chama tawala (CCM) na vyama vikuu vyenye watu wengi. Vyama hivyo (CHADEMA na ACT Wazalendo) vimetoa msimamo mkali unaokinzana na chama tawala na hata serikali. CHADEMA kimesema kama hakuna mabadiliko, kitazuia uchaguzi, wakati CCM kimesema uchaguzi utafanyika bila makubaliano hayo."
"ACT Wazalendo kimesisitiza kutumika kwa makubaliano hayo na kupinga kufanyika kwa uchaguzi Zanzibar kwa mfumo wa siku mbili. Kwa upande wake, serikali imeliagiza Jeshi la JWTZ kujiandaa kukabiliana na yatokanayo na upinzani huo wa kisiasa."