Si ajabu tunawazika kwa heshima wale walio machukizo mbele za Mungu

Si ajabu tunawazika kwa heshima wale walio machukizo mbele za Mungu

Kama kitu kipo na ukawa na uhakika basi hutakua na sababu ya kuamini kua kipo kwasababu ushajua kwa uhakika na unaweza kuthibitisha pasi na shaka uwepo wa hicho kitu
Mkuu wewe una uhakika gani kwamba hicho kitu kwamba hakipo?
Kwaiyo kutuambia kitu flani kipo eti kwasababu imani yako imekushawishi uamini hivyo, hiyo haitoi mwanya kufikia hitimisho juu ya madai yako kua ni kweli.

Kwasababu ni jambo ambalo huwezi kulithibitisha kwa uhakika. Na kama huwezi kulithibitisha bila kuacha shaka tutakubsliana vipi kua kitu hicho ni kweli kipo na sio kwamba ni invention uliyoitengeneza kichwani mwako tu
Una vithibitisho vyovyote vvyenye uhakika na visivyo na shaka ambavyo vinasema kitu hicho hakipo? (mungu)
 
Mkuu wewe una uhakika gani kwamba hicho kitu kwamba hakipo?

Una vithibitisho vyovyote vvyenye uhakika na visivyo na shaka ambavyo vinasema kitu hicho hakipo? (mungu)
Hayupo kwasababu ni dhana tu ya kufikirika ambayo haithibitishiki kihalisia nje ya masimulizi yake

Kama unapingana na hoja yangu basi thibitisha huyo Mungu yupo tuone
 
Neno fikirishi. Asante. Lakini huko RC siku hizi kulewa ni dhambi. Mimi nijuavyo kunywa pombe inaruhusiwa RC.
Mama mmoja alikuwa na mume mlevi sana. Kila siku mwanaume huyo alienda kilabuni kunywa pombe na kurudi nyumbani usiku. Kwa vile mama huyo alikuwa Mcha Mungu, hakuweza kumkimbia mumewe; bali kila siku alimuombea kwa Mungu ili abadilike na kuwa mcha Mungu kama yeye
 
Hayupo kwasababu ni dhana tu ya kufikirika ambayo haithibitishiki kihalisia nje ya masimulizi yake

Kama unapingana na hoja yangu basi thibitisha huyo Mungu yupo tuone
Kwani kila kisichothibitishika kama kipo hakipo?
Kama umeshindwa kuthibitisha kama kipo sasa kwanini useme hakipo wakati umeshindwa kuthibitisha uwepo wake?

Mimi sijasema kwamba mungu yupo au hayupo bali wewe ndiye uliyesema mungu hayupo.

Wewe ndo ulitakiwa ku"thibitisha kwamba mungu hayupo...?
 
Mkuu mwanzo wa habari yako nimeupenda sana kwasababu unaakisi uhalisia wa changamoto zinazojitokeza huku mitaani. Ila tangu ulipoingiza dhana ya "malaika" hapo nimeanza kupata mashaka dhidi ya mkasa wako kua ni finction.
Nikiwa kama mwalimu wa Kiingereza nimeona niseme neno
Hata mimi nina mashaka hii story itakuwa ni finction kwasababu story ambazo ni fiction zinaonekana tu jinsi zilivyo
 
RC ni dini ya ajabu Sana, kupokea michango wanapenda sana lakini pata tatizo ndio utajua kuwa wanafiki wakubwa, Kuna shemeji yangu wa kike alijichinja akafariki na walikuwa hawafunga ndoa aisee waligoma kumzika kwa misa kabisa wakati jamaa aliombwa kanisani kutaja mchango wake alitoa zaidi ya laki tano, shenzi kabisa
Mkuu mchango unaotoa Kanisani si kigezo tosha cha lukufanya uzikwe kwa misa.Usitumie pesa km fimbo ya kulazimisha mambo wakati taratibu haziruhusu.
 
Kwani pombe ni dhambi kwa wakatoliki?! Toka lini ikawa ni dhambi ?! Mbona ma padre wanakunywa tu ?! Embu nielewesheni I’m confused here[emoji854]
Inatakiwa nikupe dozi ya maana ili uelewe.
 
Kwani kila kisichothibitishika kama kipo hakipo?
Utajuaje kwamba hiki unachoambiwa kua kipo ni kweli kipo ila tu kimekosa uthibitisho kuonesha kipo?

Kama umeshindwa kuthibitisha kama kipo sasa kwanini useme hakipo wakati umeshindwa kuthibitisha uwepo wake?
Hapo juu nimekuoneshea sababu ya hao malaika na mungu kua hawapo kwasababu ni finction idea na ndio maana hawathibitishiki kihalisia.

Ni sawa na mimi nikuambie katikati ya jua kuna chupa ya plastic ya chai ambayo ina hang bila kuungua, utahitaji kwenda kwenye jua kuthibitisha madai yangu kua chupa hiyo haipo?

Mimi sijasema kwamba mungu yupo au hayupo bali wewe ndiye uliyesema mungu hayupo.
kwaiyo wewe binafsi hukubaliani kwamba mungu yupo?

Unaweza kuthibitisha yupo?

Wewe ndo ulitakiwa ku"thibitisha kwamba mungu hayupo...?
Kimantiki mzigo wa kuthibitisha upo mabegani kwa yule ambaye anasema kitu fulani kipo

Unataka kuniambia wewe utakubali kila kitu utachoambiwa kwamba kipo as long as hakutakua na uthibitisho wa kuonesha kua kitu hicho hakipo?
 
Nikiwa kama mwalimu wa Kiingereza nimeona niseme neno
Hata mimi nina mashaka hii story itakuwa ni finction kwasababu story ambazo ni fiction zinaonekana tu jinsi zilivyo
Post Namba 53 nahisi kutakua kuna makosa mengine pale naomba uipitie tena.

Fanya upesi kabla wenzako hawajakuwahi Maana kuna wimbi kubwa la walimu waliokosa ajira serikalini now wana fokasi kufundisha kwenye social networks
 
Mkuu mwanzo wa habari yako nimeupenda sana kwasababu unaakisi uhalisia wa changamoto zinazojitokeza huku mitaani. Ila tangu ulipoingiza dhana ya "malaika" hapo nimeanza kupata mashaka dhidi ya mkasa wako kua ni finction.
Na mimi nilikua na same comment.
Angebadili badala ya kusema malaika, angesema hivi
"Alikufa maji akiwa katika jitihada za kumuokoa binti aliekua akizama au akiwa ktk hatari ya kuliwa na Mamba ........"
Hapo ingeleta uhalisia wa yeye kutenda mema
 
Nikiwa kama mwalimu wa Kiingereza nimeona niseme neno
Hata mimi nina mashaka hii story itakuwa ni finction kwasababu story ambazo ni fiction zinaonekana tu jinsi zilivyo
Mkuu kuna typing error na human error (misspelled) ...nadhan alitaka kuandika fiction
 
Hakuna dhambi ya ulevi kwa Wa catholic (Roman) story ya kubumba hii...bye the way ina mafunzo...thanx
 
Post Namba 53 nahisi kutakua kuna makosa mengine pale naomba uipitie tena.

Fanya upesi kabla wenzako hawajakuwahi Maana kuna wimbi kubwa la walimu waliokosa ajira serikalini now wana fokasi kufundisha kwenye social networks
Nimeshawawahi
 
Wasalaam,

Nilipokuwa kidato cha tatu, mwanafunzi mwenzetu alijiua kwa kunywa vidonge 16 vya chloroquine.

Binti huyo aliyekuwa akiitwa Rebeka, alikuwa mzuri wa sura, umbo, na tabia na kwa kweli hakuna hata mtu mmoja aliyewaza kuwa mrembo huyo angeweza Kujitoa roho kikatili hivyo. Kifo chake kilizua mtafaruku mkubwa mno katika familia, lakini kubwa zaidi ni kuwa kanisa lake lilimsusa. Rebeka alikuwa Mkatoliki (RC) na kwa taratibu za kanisa hilo mtu akijiua anakuwa ameikana imani, hivyo hawezi kuzikwa Kikristo.

Ndugu zake walizunguka makanisa kadhaa kutafuta Padre wa kumzika, lakini wote walikataa. Padre mmoja mzee kwa jina la Werawera alipoambiwa tu habari za msiba huo mara moja akakubali kuongoza mazishi bila kipingamizi.

Ajabu baadhi ya waumini wakageuka kumlaumu Padre huyo kwa kukiuka taratibu za kanisa. Wakati wa ibada ya mazishi, ndipo padre huyo akatueleza sababu zilizomsukuma kuja kumzika binti huyo aliyejiua. Akasema “Mama mmoja alikuwa na mume mlevi sana. Kila siku mwanaume huyo alienda kilabuni kunywa pombe na kurudi nyumbani usiku. Kwa vile mama huyo alikuwa Mcha Mungu, hakuweza kumkimbia mumewe; bali kila siku alimuombea kwa Mungu ili abadilike na kuwa mcha Mungu kama yeye.

Lakini siku moja mumewe alipokuwa akivuka daraja kuelekea kilabuni aliteleza na kudumbukia mtoni, akafa maji. Kifo hicho kilimuumiza sana yule mama Kila siku alimlilia Mungu kwa kutosikia maombi yake, na kumuacha mumewe kufa akiwa mlevi, jambo linalothibitisha kuwa amekwenda jehanam.

Lakini siku moja wakati huyo mama amekaa peke yake akisononeka, mpita njia mmoja akamwambia, mama bado unasonononeka kwa ajili ya mumeo? Yule mama akasema ndiyo, na sisononeki kwa sababu amekufa, bali kwa sababu amekwenda jehanam, maana amekufa akiwa mlevi. Yule mtu akamwambia “Mama jiombee nafsi yako wewe, mumeo amemaliza safari yake na yuko peponi” Mama akasema HAIWEZEKANI alikuwa mlevi sana, na alikufa akienda Kutafuta pombe. Yule mtu akamwambia “ mama, alipokuwa akianguka mtoni, katikati ya daraja na maji ALITUBU dhambi zake” halafu yule mtu akatoweka. Kumbe alikuwa ni malaika mjumbe wa Mungu.

Padre akasema mara nyingine tunajipa nafasi ya Mungu na kupora haki ya kuhukumu ambayo ni Kazi ya Mungu tu. Si ajabu tunawazika kwa heshima wale walio machukizo kwa Mungu kwa sababu walifanikiwa kutuhadaa, na tunawadhihaki wale ambao mwenyezi Mungu amewapokea kwa sababu mioyo yao haikuwa na hila, au Walijaliwa KUTUBU kabla mauti haijawachukua. Ni Mungu tu ajuae KWA HIYO Kabla hujasema maneno mabaya kwa mtu aliyekufa, jiulize kama kweli una macho yanayoweza kuona SIRINI kama Mungu.

Inafaa sana KUMKEMEA VIKALI mtu yeyote anayetenda uovu wakati AKIWA HAI ili aziache njia zake mbaya. Lakini akishakufa hawezi kusikia wala kujirekebisha Hivyo hakuna haja ya kumtukana. Matusi kwa marehemu hayamuumizi yeye, bali wana familia yake ambao kimsingi hawana hatia yoyote. Mkaidi achapwe viboko akiwa hai, kwani maiti haijali hata ukali wa moto.

Kujiua sio suluhisho la kutatua matatizo yako.

UWE NA AMANI
1. Kinachozikwa ni mwili sio roho. Mwanadamu ni mavumbi tu na huko atarejea bila kujali ni mdhambi au mwenye haki. Rejea Biblia Takatifu:

Mhubiri 2
15 Nikasema moyoni mwangu, Kama limpatavyo mpumbavu, ndivyo litakavyonipata mimi nami; basi, kwa nini nikawa na hekima zaidi? Nikasema moyoni mwangu ya kuwa hayo nayo ni ubatili.

16 Maana hakuna kumbukumbu la milele la mwenye hekima, wala la mpumbavu; kwa sababu siku zijazo wote pia watakuwa wamekwisha kusahauliwa. Na mwenye hekima, jinsi gani anavyokufa sawasawa na mpumbavu!

2. Utaratibu wa ibada ya Mazishi ni wa kidunia wala hauna uhusiano na mbingu. Tunausindikiza "mwili" kaburini lakini mwenye huo mwili huwa hayupo hapo. Kwa hiyo basi, hadhi ya huo mwili ni sawa tu, haijalishi kama amekufa kwa ukimwi, au ajali, au usingizini nk.

Sasa Mungu anashughulika na roho. Hata kama tungefanya ibada mara mia kuombea marehemu, Mungu anashughulika na roho. Hizi habari za KUNYIMWA HUDUMA YA MAZISHI kwa sababu eti hukuhudhuria ibada mara kwa mara, au umejinyonga, ni hofu za kidunia kabisa, wala hazina uhusiano na Mungu. Ni mbinu mojawapo ya kuwalazimisha watu wawe na mafungamano na dini.

3. Kuhusu kujinyonga, hili ni dhambi mbele za Mungu. Why? Kitendo cha kuwazia kuutoa uhai tayari ni dhambi ya kuua na shetani ameshakata roho. Hebu tuichambue dhambi hii:

>> ni dalili dhahiri za kutokuwa na imani kwa Mungu. Kwamba Mungu anasamehe, au ana uwezo wa kubadili majira mabaya kuwa mazuri.

Waebrania 11
6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Habari za Danieli ana wengine wengi kwenye Biblia zimelenga kutupatia ujasiri katika Mungu kwamba tukiamini tu, atatujibu.

>> ni kuliharibu hekalu la Mungu.

1 Wakorintho 3
16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.

Hii miili yetu sio mali yetu bali ni yake Yeye aliyetuumba. Kujaribu kubadili matumizi yake kwa namna yoyote ile ni kuhujumu mpango wa aliyeiumba.

4. Kuhusu kutubu. Mungu ni mwingi wa rehema, mtu akitubu kww kumaanisha atamsamehe dhambi zake zote. Sasa mtu aliyokusudia kujinyonga tayari amekwisha tenda dhambi hiyo:

Mathayo 5
21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.

22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.

Kumbe kule kuwa tu na wazo la kujiua NI DHAMBI YA KUJIUA. Hizi ndizo amri za ufalme wa Mungu. Hazihukumu kitendo bali nia ya kutenda. Hazihukumu mwili bali mawazo yaliyo rohoni. Sasa kama mtu yuko hewani wakati ameamua kujirusha ghorofani, ndipo akabadili mawazo kabla ya kufika chini, hilo Mungu ndiye ajuaye. Kwamba mtu anapata wazo la kuzini, hashtuki kama ni dhambi, anatongoza mke wa jirani yake, haoni dhambi, wanapanga tarehe na saa ya kuzini, bado tu haoni, siku ikifika anazunguka mji mzima kutafuta gesti ya mafichoni, hajajua tu kama dhambi inamtafuna, anaingia na mke wa mtu kwa kujificha ili asionekane chumbani, bado tu!! Halafu wakati akiwa katikati ya tendo la ngono ndipo fahamu zinamrudia, ghafla anagundua kuwa anatenda dhambi, anafanya toba.

Sasa Yesu Kristo alileta sheria za ufalme, sheria ambazo zilikuja kuthibitisha kuwa torati asili yake ni rohoni. Mwana wa ufalme wa Mungu HAWEZI KUFIKIA KUTENDA HAYO. Dhambi itabinywa mapema tu, kabla ya kufika kwenye tendo na maungamo yatafanyika. Huo ndio ufalme aliohubiri Kristo.
 
Utajuaje kwamba hiki unachoambiwa kua kipo ni kweli kipo ila tu kimekosa uthibitisho kuonesha kipo?
Kimekosa uthibitisho kuwa kipo sasa unapingaje hakipo wakati wewe ndiye uliyeshindwa kuthibitisha uwepo wake?

Labda kipo sababu kimekosa uthibitisho wake na sio kwamba hakipo kisa wewe umekosa uthibitisho.
Hapo juu nimekuoneshea sababu ya hao malaika na mungu kua hawapo kwasababu ni finction idea na ndio maana hawathibitishiki kihalisia.
Utasemaje ni fiction wakati umeshindwa kuthibitisha kama kipo na umeshindwa kuthibitisha kama hakipo.

Kushindwa kuthibitisha uwepo wa kitu haimaanishi kwamba kitu hicho hakipo sababu mwenye tatizo ni wewe uliyeshindwa kuthibitisha kama kipo na ukichangia pia umeshindwa kuthibitisha kutokuwepo kwa hicho kitu.
Ni sawa na mimi nikuambie katikati ya jua kuna chupa ya plastic ya chai ambayo ina hang bila kuungua, utahitaji kwenda kwenye jua kuthibitisha madai yangu kua chupa hiyo haipo?
Nitakuuliza wewe umejuaje?
kwaiyo wewe binafsi hukubaliani kwamba mungu yupo?

Unaweza kuthibitisha yupo?
Kwanini nithibitishe kwamba mungu yupo wakati hakuna sehemu niliandika kwamba mungu yupo au hayupo?
Kimantiki mzigo wa kuthibitisha upo mabegani kwa yule ambaye anasema kitu fulani kipo
Sasa mimi hakuna sehemu ambayo nimesema kwamba mungu yupo au hayupo ila wewe ndio umesema hayupo tena kwa sababu yako ndogo kwamba umeshindwa kuthibitisha uwepo wake.

Inabidi uthibitishe kutokuwepo kwake na sio kisa umeshindwa kuthibitisha basi unakuja na simple conclusion kwamba hayupo.

Sasa thibitisha kwamba mungu hayupo.
Unataka kuniambia wewe utakubali kila kitu utachoambiwa kwamba kipo as long as hakutakua na uthibitisho wa kuonesha kua kitu hicho hakipo?
Kwanini nikatae na kwanini nikubali kitu ambacho hakina uthibitisho?
 
Back
Top Bottom