Course Coordinator
JF-Expert Member
- Jul 27, 2019
- 1,742
- 3,224
- Thread starter
- #41
Hakuna maandikoTuwekee maandiko.
Petro alijinyonga ila mbona hakusemwa kama alitengwa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna maandikoTuwekee maandiko.
Mkuu wewe una uhakika gani kwamba hicho kitu kwamba hakipo?Kama kitu kipo na ukawa na uhakika basi hutakua na sababu ya kuamini kua kipo kwasababu ushajua kwa uhakika na unaweza kuthibitisha pasi na shaka uwepo wa hicho kitu
Kwaiyo kutuambia kitu flani kipo eti kwasababu imani yako imekushawishi uamini hivyo, hiyo haitoi mwanya kufikia hitimisho juu ya madai yako kua ni kweli.
Una vithibitisho vyovyote vvyenye uhakika na visivyo na shaka ambavyo vinasema kitu hicho hakipo? (mungu)Kwasababu ni jambo ambalo huwezi kulithibitisha kwa uhakika. Na kama huwezi kulithibitisha bila kuacha shaka tutakubsliana vipi kua kitu hicho ni kweli kipo na sio kwamba ni invention uliyoitengeneza kichwani mwako tu
Hayupo kwasababu ni dhana tu ya kufikirika ambayo haithibitishiki kihalisia nje ya masimulizi yakeMkuu wewe una uhakika gani kwamba hicho kitu kwamba hakipo?
Una vithibitisho vyovyote vvyenye uhakika na visivyo na shaka ambavyo vinasema kitu hicho hakipo? (mungu)
Mama mmoja alikuwa na mume mlevi sana. Kila siku mwanaume huyo alienda kilabuni kunywa pombe na kurudi nyumbani usiku. Kwa vile mama huyo alikuwa Mcha Mungu, hakuweza kumkimbia mumewe; bali kila siku alimuombea kwa Mungu ili abadilike na kuwa mcha Mungu kama yeye
Hakuna aliyefariki.Kuna msiba kwani? Nani amefariki ?
Hayupo kwasababu ni dhana tu ya kufikirika ambayo haithibitishiki kihalisia nje ya masimulizi yake
Kwani kila kisichothibitishika kama kipo hakipo?Kama unapingana na hoja yangu basi thibitisha huyo Mungu yupo tuone
Nikiwa kama mwalimu wa Kiingereza nimeona niseme nenoMkuu mwanzo wa habari yako nimeupenda sana kwasababu unaakisi uhalisia wa changamoto zinazojitokeza huku mitaani. Ila tangu ulipoingiza dhana ya "malaika" hapo nimeanza kupata mashaka dhidi ya mkasa wako kua ni finction.
Mkuu mchango unaotoa Kanisani si kigezo tosha cha lukufanya uzikwe kwa misa.Usitumie pesa km fimbo ya kulazimisha mambo wakati taratibu haziruhusu.RC ni dini ya ajabu Sana, kupokea michango wanapenda sana lakini pata tatizo ndio utajua kuwa wanafiki wakubwa, Kuna shemeji yangu wa kike alijichinja akafariki na walikuwa hawafunga ndoa aisee waligoma kumzika kwa misa kabisa wakati jamaa aliombwa kanisani kutaja mchango wake alitoa zaidi ya laki tano, shenzi kabisa
Inategemea mkuu.Kujinyonga ni tendo linalofuta matendo yote ya Kikristu aliyoyaishi mhusika for eternity.
Sio wana hisi,tunaamini hivyo.Njoo RC uone utamu.Amina hao wanaojiita Rc wanahc pepo ni yao peke yao na kuhic wakikusalia unaenda mbinguni
Inatakiwa nikupe dozi ya maana ili uelewe.Kwani pombe ni dhambi kwa wakatoliki?! Toka lini ikawa ni dhambi ?! Mbona ma padre wanakunywa tu ?! Embu nielewesheni I’m confused here[emoji854]
Utajuaje kwamba hiki unachoambiwa kua kipo ni kweli kipo ila tu kimekosa uthibitisho kuonesha kipo?Kwani kila kisichothibitishika kama kipo hakipo?
Hapo juu nimekuoneshea sababu ya hao malaika na mungu kua hawapo kwasababu ni finction idea na ndio maana hawathibitishiki kihalisia.Kama umeshindwa kuthibitisha kama kipo sasa kwanini useme hakipo wakati umeshindwa kuthibitisha uwepo wake?
kwaiyo wewe binafsi hukubaliani kwamba mungu yupo?Mimi sijasema kwamba mungu yupo au hayupo bali wewe ndiye uliyesema mungu hayupo.
Kimantiki mzigo wa kuthibitisha upo mabegani kwa yule ambaye anasema kitu fulani kipoWewe ndo ulitakiwa ku"thibitisha kwamba mungu hayupo...?
Post Namba 53 nahisi kutakua kuna makosa mengine pale naomba uipitie tena.Nikiwa kama mwalimu wa Kiingereza nimeona niseme neno
Hata mimi nina mashaka hii story itakuwa ni finction kwasababu story ambazo ni fiction zinaonekana tu jinsi zilivyo
Na mimi nilikua na same comment.Mkuu mwanzo wa habari yako nimeupenda sana kwasababu unaakisi uhalisia wa changamoto zinazojitokeza huku mitaani. Ila tangu ulipoingiza dhana ya "malaika" hapo nimeanza kupata mashaka dhidi ya mkasa wako kua ni finction.
Mkuu kuna typing error na human error (misspelled) ...nadhan alitaka kuandika fictionNikiwa kama mwalimu wa Kiingereza nimeona niseme neno
Hata mimi nina mashaka hii story itakuwa ni finction kwasababu story ambazo ni fiction zinaonekana tu jinsi zilivyo
Najua mkuu,namzingua tuMkuu kuna typing error na human error (misspelled) ...nadhan alitaka kuandika fiction
NimeshawawahiPost Namba 53 nahisi kutakua kuna makosa mengine pale naomba uipitie tena.
Fanya upesi kabla wenzako hawajakuwahi Maana kuna wimbi kubwa la walimu waliokosa ajira serikalini now wana fokasi kufundisha kwenye social networks
1. Kinachozikwa ni mwili sio roho. Mwanadamu ni mavumbi tu na huko atarejea bila kujali ni mdhambi au mwenye haki. Rejea Biblia Takatifu:Wasalaam,
Nilipokuwa kidato cha tatu, mwanafunzi mwenzetu alijiua kwa kunywa vidonge 16 vya chloroquine.
Binti huyo aliyekuwa akiitwa Rebeka, alikuwa mzuri wa sura, umbo, na tabia na kwa kweli hakuna hata mtu mmoja aliyewaza kuwa mrembo huyo angeweza Kujitoa roho kikatili hivyo. Kifo chake kilizua mtafaruku mkubwa mno katika familia, lakini kubwa zaidi ni kuwa kanisa lake lilimsusa. Rebeka alikuwa Mkatoliki (RC) na kwa taratibu za kanisa hilo mtu akijiua anakuwa ameikana imani, hivyo hawezi kuzikwa Kikristo.
Ndugu zake walizunguka makanisa kadhaa kutafuta Padre wa kumzika, lakini wote walikataa. Padre mmoja mzee kwa jina la Werawera alipoambiwa tu habari za msiba huo mara moja akakubali kuongoza mazishi bila kipingamizi.
Ajabu baadhi ya waumini wakageuka kumlaumu Padre huyo kwa kukiuka taratibu za kanisa. Wakati wa ibada ya mazishi, ndipo padre huyo akatueleza sababu zilizomsukuma kuja kumzika binti huyo aliyejiua. Akasema “Mama mmoja alikuwa na mume mlevi sana. Kila siku mwanaume huyo alienda kilabuni kunywa pombe na kurudi nyumbani usiku. Kwa vile mama huyo alikuwa Mcha Mungu, hakuweza kumkimbia mumewe; bali kila siku alimuombea kwa Mungu ili abadilike na kuwa mcha Mungu kama yeye.
Lakini siku moja mumewe alipokuwa akivuka daraja kuelekea kilabuni aliteleza na kudumbukia mtoni, akafa maji. Kifo hicho kilimuumiza sana yule mama Kila siku alimlilia Mungu kwa kutosikia maombi yake, na kumuacha mumewe kufa akiwa mlevi, jambo linalothibitisha kuwa amekwenda jehanam.
Lakini siku moja wakati huyo mama amekaa peke yake akisononeka, mpita njia mmoja akamwambia, mama bado unasonononeka kwa ajili ya mumeo? Yule mama akasema ndiyo, na sisononeki kwa sababu amekufa, bali kwa sababu amekwenda jehanam, maana amekufa akiwa mlevi. Yule mtu akamwambia “Mama jiombee nafsi yako wewe, mumeo amemaliza safari yake na yuko peponi” Mama akasema HAIWEZEKANI alikuwa mlevi sana, na alikufa akienda Kutafuta pombe. Yule mtu akamwambia “ mama, alipokuwa akianguka mtoni, katikati ya daraja na maji ALITUBU dhambi zake” halafu yule mtu akatoweka. Kumbe alikuwa ni malaika mjumbe wa Mungu.
Padre akasema mara nyingine tunajipa nafasi ya Mungu na kupora haki ya kuhukumu ambayo ni Kazi ya Mungu tu. Si ajabu tunawazika kwa heshima wale walio machukizo kwa Mungu kwa sababu walifanikiwa kutuhadaa, na tunawadhihaki wale ambao mwenyezi Mungu amewapokea kwa sababu mioyo yao haikuwa na hila, au Walijaliwa KUTUBU kabla mauti haijawachukua. Ni Mungu tu ajuae KWA HIYO Kabla hujasema maneno mabaya kwa mtu aliyekufa, jiulize kama kweli una macho yanayoweza kuona SIRINI kama Mungu.
Inafaa sana KUMKEMEA VIKALI mtu yeyote anayetenda uovu wakati AKIWA HAI ili aziache njia zake mbaya. Lakini akishakufa hawezi kusikia wala kujirekebisha Hivyo hakuna haja ya kumtukana. Matusi kwa marehemu hayamuumizi yeye, bali wana familia yake ambao kimsingi hawana hatia yoyote. Mkaidi achapwe viboko akiwa hai, kwani maiti haijali hata ukali wa moto.
Kujiua sio suluhisho la kutatua matatizo yako.
UWE NA AMANI
Kimekosa uthibitisho kuwa kipo sasa unapingaje hakipo wakati wewe ndiye uliyeshindwa kuthibitisha uwepo wake?Utajuaje kwamba hiki unachoambiwa kua kipo ni kweli kipo ila tu kimekosa uthibitisho kuonesha kipo?
Utasemaje ni fiction wakati umeshindwa kuthibitisha kama kipo na umeshindwa kuthibitisha kama hakipo.Hapo juu nimekuoneshea sababu ya hao malaika na mungu kua hawapo kwasababu ni finction idea na ndio maana hawathibitishiki kihalisia.
Nitakuuliza wewe umejuaje?Ni sawa na mimi nikuambie katikati ya jua kuna chupa ya plastic ya chai ambayo ina hang bila kuungua, utahitaji kwenda kwenye jua kuthibitisha madai yangu kua chupa hiyo haipo?
Kwanini nithibitishe kwamba mungu yupo wakati hakuna sehemu niliandika kwamba mungu yupo au hayupo?kwaiyo wewe binafsi hukubaliani kwamba mungu yupo?
Unaweza kuthibitisha yupo?
Sasa mimi hakuna sehemu ambayo nimesema kwamba mungu yupo au hayupo ila wewe ndio umesema hayupo tena kwa sababu yako ndogo kwamba umeshindwa kuthibitisha uwepo wake.Kimantiki mzigo wa kuthibitisha upo mabegani kwa yule ambaye anasema kitu fulani kipo
Kwanini nikatae na kwanini nikubali kitu ambacho hakina uthibitisho?Unataka kuniambia wewe utakubali kila kitu utachoambiwa kwamba kipo as long as hakutakua na uthibitisho wa kuonesha kua kitu hicho hakipo?