TheForgotten Genious
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 2,087
- 3,156
Kuna dhana imezoeleka na wazazi ambao vijana wao wamefikia umri wa kujitegemea kuwaruhu ama kuwataka waondoke nyumbani ili hali hawana chochote na inawezekana hata kazi hana inayoeleweka.
Hii hali ina athari nyingi sana kwa vijana wa jinsia zote ila kwa wakike ndio zaidi. Kijana kuhitimu chuo haimaanishi kwamba sasa anaweza kumudu kila kitu,bado anakuwa na changamoto za kutqfuta kibarua ili aweze kujikimu.
Kwa upande wangu mimi nitafanya hivi ,wanangu kutoka nyumbani itakuwa ni option,na anapotoka nilazoma nijue kwa uyakinifu anaenda wapi na kwanini? Akinipa hoja yakinifu na nikazikunali basi nitagharamia kila kitu,kodi ya nyumba miezi 6, pesa yakujikimu miezi 6( hata kama anamshahara) kama amepata kazi,!,nitam unulia kila kitu ambacho ni hitaji muhimu kwa kuanza maisha ikiwemo kitanda, na godoro na mengineyo.
Kama ameamua kufanya biashara basi nitampatia mtaji,na nitaifuatilia mpaka pale jitakapo ona imesimama,na katika kipindi hicho chote nitampatia mahitaji muhimu mpaka pale biashara itakapo shinda kipindi cha mpito.
Unamruhusu mtoto aondoke halafu mkononi hana kitu wala hana kitu cha maana, matokeo yake kama ni wa kike anashawishika kujiuza.
Hakikisha mtoto kasimama na unauhakika kasimama kikamilifu ndio umuache.