Si kwa ajili ya ubaguzi, bali namshauri Rais Samia aepuke kufanya maamuzi makubwa ya muda mrefu yanayohusu upande wa Tanzania bara peke yake

Sasa kama watanganyika wamelala unategemea afanye nini zaidi ya kuuza kila kitu.
Inashangaza, inasikitisha, inaudhi na inakasirisha. Watanganyika tumekuwa kama kondoo, tumebaki tu tunaswagwa tukipelekwa machinjoni. Kwa hakika tusimlaumu mtu hapa, tujilaumu tu sisi wenyewe kwa kuruhusu hali hii. Wajukuu wetu watakaposoma jinsi tulivyoruhusu hali hii hakika watatulaani.
 
Hili nalo tutalitizama.
 
🚮🚮
 
Siyo Watanganyika ni CCM na Wabunge wa CCM pamoja na VIongozi wa Serikali wasioijali mama Tanganyika.
Ninavyojua ni baadhi tu ya Watanganyika ambao wanaulazimusha muungano kwa sababu wanafaidika nao. HIcho kikundi cha wasaliti ndani ya Tanganyika kinajiita CCM. Nje ya muungano hakuna CCM na ndio maana juhudi kubwa zinafanyika kuhakikisha hawaachii madaraka hata iweje!
Nakuhakikishia kama kuna kitu kinawatia hofu Wazanzibar ni kuvunjika Muungano.
Kelele za Wazanzibar ni sawa na chura kwani muungano ndio kwa sasa unawasetiri kupitia CCM. Watanganyika ndani ya CCM ni wachoyo, wabinafsi na walafi wakijifikiria tu wao na hawana habari na ndugu zao huku bara shida wananzopata. Kwao mradi mikono yao huenda kinywani.
Usiwasikilize akina '' wa Oman koko'
Muungano ukivunjika, wengi wa Wazanzibar hawatakuwa na pa kwenda. Wanauhitaji muungano kama wanavyohitaji hewa ya oxygen. Hao wapiga kelele ni wanafiki wakubwa.
Wana uwezo wa kuvunja muungano, hawana hawana uthubutu au ubavu wala pumzi
Huo uthubutu wautoe wapi? Nje ya muungano Wazanzibari ni kama samaki nje ya maji. Wengi wataishia ulowezi nje ama ndani ya Tanganyika.
 
Nnachokiona mimi ni kuwa Tanzania bara inajiundia migogoro ya Utaifa huko siku za usoni.

Kuepusha ni lazima kuwe na serikali kama ilivyo kwenye makubaliano ya awali.

Serikali ya Tanganyika iwepo kwa maslahi ya Tanhganyika, Serikali ya Zanzibar iwepo kwa maslahi ya Zanzibar. Serikali ya tanzania iwepo kwa maslahi ya Muunhgano tu na yaliyomo kwenye muungano tu.

La sivyo irudishwe serikali iliyokuwa inatawala kabla ya ujio wa wajerumani, tuwe na Zenjbar tu. Yaani Bara la watu wenye pua pana. Inasawa wengine wanatafasiri kuwa ni "bara la mtu mweusi". Serikali moja tu ya Zenjbar.
 
Kwanini hutaki kukubali ukweli kwamba watanganyika ndio wanafosi muungano?
Unajua wale kule zenji walianzisha hata harakati za uamsho kudai Zanzibar yao na waliishia wapi?
Acha masihara kwenye mambo makubwa bwashee

..sasa hivi Maraisi wote wanatoka Zanzibar. Kama wako serious huu ndio muda muafaka wa kuvunja muungano.

..ningekuelewa kama ungesema CCM ndio wanang'ang'ania muungano. Na humo wako Watanganyika na Wazanzibari.
 
Kumbe unaelewa bali unajitoa akili kimakusudi?

Mambo ya muungano yanajulikana, na japo Tanzania bara haina serikali yake, mambo yaliyofanywa kuwa ya Zanzibar yanafanya mambo yale yale yakiwa kwenye muungano yasiwe tena ya muungano bali ya Tanzania bara.

Kwa mfano, huwezi kusema mafuta yaliyoko Zanzibar ni suala la Zanzibar, na mafuta yaliyoko bara ni ya muungano. Ukishafanya mafuta yaliyoko visiwani ni ya Zanzibar, inference ni kwamba mafuta yaliyoko bara hayapaswi tena kuonwa kama ni mafuta ya muungano.

Kumbuka kwamba, kimsingi, iwe imeandikwa kwenye katiba au la, mteule wa kugombea uraisi wa Tanzania siku zote atatoka bara, na mgombea mwenza kutoka Zanzibar. Yote haya ni kutambua kwamba siku hizi raisi wa Tanzania kimsingi ni raisi wa Tanzania bara kwa sababu Zanzibar inajitegema kiserikali. Kuna kama 2% ya mambo atakayofanya kama raisi yataihusu Zanzibar, na sana sana ni mambo ya nchi za nje.

Katika mpangilio huu, hawakuona mbali na walisahau kusema raisi akifa makamu wa raisi hapaswi kuwa raisi kwa sababu siku zote makamu wa raisi wa kupigiwa kura atakuwa ni kutoka Zanzibar, na raisi wa Tanzania ndio atakuwa raisi wa Tanzania bara, bila serikali ya Tanzania bara kuwapo rasmi. Raisi akifa na makamu wa Raisi toka Zanzibar akawa raisi basi awe acting president kwa maximum mwaka mmoja tu ili ndani ya muda huo uchaguzi mpya wa raisi ufanyike kisha arudie kuwa makamu wa raisi.

Theoretically, ukitaka kusawazisha hali iliyopo, ya Samia kuwa raisi wa Tanzania kutoka Zanzibar, inabidi mtu kutoka bara aende akawe raisi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar. Tumpeleke Mwigulu akawe raisi kule, mweupe kama wao.

Ndio maana nikasema, kwa kuwa Samia anatoka Zanzibar kutokana na jambo lisilotazamiwa, ni busara kwamba asifanye maamuzi kuhusu mambo makubwa ya bara yenye long term lock-in effect, na kusubiri hadi raisi kutoka bara akiwa madarakani ndio afanye hayo maamuzi.
 

..mafuta yaliyoko TANGANYIKA.
 
..sasa hivi Maraisi wote wanatoka Zanzibar. Kama wako serious huu ndio muda muafaka wa kuvunja muungano.
Haswaa! na sijui kwanini wamekaa kimya. Wazanzibar wana 'double face' au kaunafiki
Mara zote wanasema Rais ni wa Tanganyika, jhawawezi kutoka

Kuanzia Nyerere hadi JP Magufuli hakujawahi kuwa na Marais kutoka upande mmoja.

KwasasaMarais wote ni Wazanzibar! tulitegemea lile shinikizo lizidi kinyume chake ACT ndio wasemaji wa SSH Zanzibar na CCM ndio wamekumbatia Muungano huko.

Mwaka 2010 Karume alisaini mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar bila kushirikisha Tanganyika au JMT.

Rais Mwinyi aitishe Baraza la Wawakilishi watoe hoja ya kujadili muungano iwe S3 au kujitoa
Rais SSH ana uwezo wa kutoka hoja kupitia mchakato wa Katiba kama livyofanya J Kikwete awasaidie
Wabunge wa Zanzibar wapeleke hoja kwa kutumia 2/3 ya Wazanzibar wakiungwa mkono na SSH na Mwinyi
Ikishindikana, Wabunge, Mawaziri na watumishi wa Zanzibar waondoke Bara, muungano utakuwa umekwisha

Kwanini isiwe Watanganyika? Jibu ni lile lile hawana chombo cha kusimamia masilahi yao kama ambavyo hawana chombo cha kusimamia rasilimali zao.
..ningekuelewa kama ungesema CCM ndio wanang'ang'ania muungano. Na humo wako Watanganyika na Wazanzibari.
Ni CCM , Mag3 anasema ni kakundi kadogo kanafaidika! Wananchi wa kawaida hawataki huu muundo.
Na sasa Watanganyika ndio kabisa wanajiuliza wanahitaji nini hadi kulaumiwa ? Wana nini cha kupoteza!
 

..serikali zinazopaswa kurudishwa ni zile zilizokuwepo 1964 kabla ya muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…