Si kwa ajili ya ubaguzi, bali namshauri Rais Samia aepuke kufanya maamuzi makubwa ya muda mrefu yanayohusu upande wa Tanzania bara peke yake

..serikali zinazopaswa kurudishwa ni zile zilizokuwepo 1964 kabla ya muungano.
Serikali iliyotuwekea misingi mibovu mpaka tukawa masikini wa mwisho duniani?

"Kazi ya Mungu haina makosa".
 
..sasa hivi Maraisi wote wanatoka Zanzibar. Kama wako serious huu ndio muda muafaka wa kuvunja muungano.

..ningekuelewa kama ungesema CCM ndio wanang'ang'ania muungano. Na humo wako Watanganyika na Wazanzibari.
Najua umeshaelewa, ila kukubali mbele ya watoto ndio shida, halafu sasa hivi wamebadilishana mtanganyika anatawala zenji na mzenji anatawala bara

Ccm wapo makini sana, haiwezi kutokea hata mara moja marais wote wakatoka upande mmoja wala dini moja, wala makamu na rais wakafanane, katu haitatokea tena
*
Kama ulikua hufahamu, Huseni ni mbara tena mtanganyika original
 
inakwaza kuona nchi yenye raia zaidi ya 58m inashindanishwa waajiriwa/wateuliwa na kawilaya kenye watu hata 2m hawafiki, kazanzibar. Tanganyika ipo mioyoni mwa wengi na kuna siku itafufuka kwa nguvu kubwa sana, na wale walioibeza watatafuta kwa kwenda.
 
Unapoteza muda wako bure kushauri wapumbavuu
 

..Watanganyika wengi huwa hawana habari na muungano mpaka pale Wazanzibari wanapoanza kulalamika.

..Vilevile Watanganyika hawana muamko wa siasa kulinganisha na Wazanzibari kwa hiyo sio rahisi kuanza kuudadisi muungano.

..Watanganyika wanaopinga muungano ni wale wanaofuatilia historia na siasa kwa ukaribu, na tena wako ktk vyama vya upinzani.

..Kwa upande mwingine, muungano unalindwa na kutetewa na genge la Watanganyika na Wazanzibari walioko ndani ya CCM.

..Wazanzibari walioko CCM wanategemea majeshi ya muungano kutwaa madaraka ya Zanzibar. Hivyo wanatetea muungano kwasababu unawasaidia kubaki madarakani.

..Watanganyika walioko CCM hawataki muungano uguswe, kwasababu hauwezi kuguswa bila kugusa na mengine kama Tume ya Uchaguzi, mamlaka ya Raisi, etc etc. Mabadiliko yoyote ktk muungano yanatishia madaraka yao.

..Huo ndio mtizamo wangu kuhusu kinachoendelea ktk muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 
Una hoja Mkuu.
 
Huyu mama kazungukwa na watu ambao sio wazuri na wanamdanganya na kwa bahati mbaya mno ni watu ambao anawaamini.
 
Labda Watoto wa Waasisi ni special 😂😂

Ulale Unono 😃

Mtoto akirithi kazi za wazazi wake kuna ubaya? Tena huyo anakuwa mzuri zaidi.

Tazama wahindi na Waarabu wanavyotesa watoto zao kwa kazi za kurithi
kwa wazazi wao.

Unataka mtu katoka maporini huko mjini kaja kwa kusoma tu akihitimu anapewa shirika la umma la usafirishaji?

Matokeo; DMT chali, UDA chali, KAMATA chali. hatujakoma, sasa BRT chali.

Tunaisubiri na ATC na SGR, kama hatua za haraka hazitachukuliwa, na zenyewe chali.

Januari alitakiwa aishie jeshini na kwenye chama tu, kama baba'ke.

Nape, mwisho kabisa ukuu wa mkoa tu.
 
Akina Maharagwe ni WA hapa hapa town kama Pedeshee Amos Makala na Mongela 😂
 

..Je, Mama Abduli naye alitakiwa aishie kwenye ualimu, kwasababu ilikuwa kazi ya Mzee wake?
 
Linatekelezeka kwa kuirudisha nchi ya Tanganyika.
Kwanini iwe dhambi kuirudisha hiyo nchi?
Mkuu ni lazima wakubaliane na Nchi ya Zanzibar. Kwenye makubaliano ni budi kuwe na time mbili, moja ya Nchi ya Zanzibar na ingine ya Nchi gani (Tanganyika)? maana Tanganyika sio nchi, watu gani wataiwakilisha wenye hadhi ya Nchi.
 
Mkuu umenena vyema kabisa, kifo cha Hayati Rais Magufuli kimetoa somo kubwa sana juu ya mapungufu yaliyomo ndani ya KATIBA yetu. Kuna utata wingi kwenye Katiba iliyopo. Rasimu ya Katiba ya Mzee Warioba ilikuwa ndio Katiba sahihi na iliyo endana na wakati tulio nao, ila Bunge chini ya maelekezo ya wajumbe wachache ndani na nje ya Bunge waliifuta Rasimu hiyo na kutoa maelekezo ya aina ya Katiba waitakayo na kuliagiza BUNGE kutengua RASIMU hiyo kwa manufaa yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…