Mr Why
JF-Expert Member
- Nov 27, 2019
- 2,235
- 4,252
Si sawa kumpeleka mtu Mahakamani Kwasababu ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja kwasababu ni starehe ya mtu binafsi na maisha yake mwenyewe. Mtu amezaliwa mwenyewe na atakufa mwenyewe kwa wakati wake hivyo basi starehe zake binafsi aachiwe mwenyewe kwasababu hajalazimisha watu washiriki nae starehe hizo bali ni makubaliano yao wenyewe.
Itakuwa sahihi kumpeleka mtu huyu mahakamani endapo anafanya vitendo hivi kwa kurubuni, kulazimisha, kushinikiza, kubaka wenzie washiriki nae pasipo maridhiano yao. Endapo watu anaoshiriki nao wamekubaliana naye basi haina haja ya kuwapeleka mahakamani kwasababu ni swala la maridhiano.
Mahakama inapokea haraka na kufanyia kazi malalamiko yote yaliyowasilishwa na mhusika mwenyewe akilalama jinsi alivyofanyiwa ubaya pengine kabakwa, karubuniwa, kalawitiwa, kanajisiwa nakadhalika. Endapo mtu anakwenda mahakamani kuishtaki watu wanaofanya starehe zao binafsi angali wao wanafurahia basi ni sawa na kupoteza muda kwasababu maswala ya watu binafsi yanamuhusu nini kwenye maisha yake.
Kama mtu ni mcha Mungu basi aishi kwenye maisha yake aliyoyachagua maswala ya kuwafuatilia walevi au wasiomcha Mungu sio kazi yake ni sawa na kuingilia maisha ya watu ni vyema kila mtu akaishi maisha yake aliyochagua pasipo kukerana kwasababu kila mtu kazaliwa mwenyewe na atakufa mwenyewe.