Si sawa kumpeleka mtu Mahakamani Kwasababu ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Si sawa kumpeleka mtu Mahakamani Kwasababu ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Nashauri Mahakama zote kabla ya kutatua matatizo kama haya waanze na swala kwa walengwa kuwa je mlikubaliana na mkafanya kwa hiari yenu? Majibu yao ndiyo yawaongoze katika kutatua haya maswala badala ya kuwahukumu kwa lazima kumbe wao wamekubaliana
Haya bhana.Ngoja nikuache.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Basi vile vile si sawa kumkamata mtu anayetembea uchi, au anayeua mwanaye, Mtoto ni wake, maisha ni yake mahakama inawahusu nini!
 
Basi vile vile si sawa kumkamata mtu anayetembea uchi, au anayeua mwanaye, Mtoto ni wake, maisha ni yake mahakama inawahusu nini!
Mapenzi yanahusiana na faragha, nadhani serikali ingesema ni marufuku kufanya mapenzi hadharani badala ya kusema ni marufuku kufanya mapenzi kwasababu huwa yanafanywa kwa faragha kwahiyo hakutakuwa na namna ya kuwazuia hawa watu kwasababu hutawaona wakifanya
 
Kwani mwanasheria hawezi kuwa shoga?
Daktari anapotibu wagonjwa yeye anakuwa ni mgonjwa mojawapo sio? Watanzania wangu mnatabia ya kubaka maneno na kumwekelea mtu maneno ya mdomoni
 
Si sawa kumpeleka mtu Mahakamani Kwasababu ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja kwasababu ni starehe ya mtu binafsi na maisha yake mwenyewe. Mtu amezaliwa mwenyewe na atakufa mwenyewe kwa wakati wake hivyo basi starehe zake binafsi aachiwe mwenyewe kwasababu hajalazimisha watu washiriki nae starehe hizo bali ni makubaliano yao wenyewe.

Itakuwa sahihi kumpeleka mtu huyu mahakamani endapo anafanya vitendo hivi kwa kurubuni, kulazimisha, kushinikiza, kubaka wenzie washiriki nae pasipo maridhiano yao. Endapo watu anaoshiriki nao wamekubaliana naye basi haina haja ya kuwapeleka mahakamani kwasababu ni swala la maridhiano.

Mahakama inapokea haraka na kufanyia kazi malalamiko yote yaliyowasilishwa na mhusika mwenyewe akilalama jinsi alivyofanyiwa ubaya pengine kabakwa, karubuniwa, kalawitiwa, kanajisiwa nakadhalika. Endapo mtu anakwenda mahakamani kuishtaki watu wanaofanya starehe zao binafsi angali wao wanafurahia basi ni sawa na kupoteza muda kwasababu maswala ya watu binafsi yanamuhusu nini kwenye maisha yake.

Kama mtu ni mcha Mungu basi aishi kwenye maisha yake aliyoyachagua maswala ya kuwafuatilia walevi au wasiomcha Mungu sio kazi yake ni sawa na kuingilia maisha ya watu ni vyema kila mtu akaishi maisha yake aliyochagua pasipo kukerana kwasababu kila mtu kazaliwa mwenyewe na atakufa mwenyewe.
Mr Bwabwa
 
Hili la kusuka halina mashiko, binadamu huwezi kuwazuia wenzio kufanya yao. Wao wanadhani kwa kufanya hivyo watazuia ushoga jambo ambalo sio kweli kwasababu hata wasiosuka baadhi yao ni mashoga pia
So binadamu akitaka kuua tumwache kisa anafanya jambo lake??!!
Afu Zenji wanakomaa na kulinda maadili
 
Mauzi ya kishoga shoga yapigwe marufuku ni kama yana promote hii upindezone
 
Mapenzi yanahusiana na faragha, nadhani serikali ingesema ni marufuku kufanya mapenzi hadharani badala ya kusema ni marufuku kufanya mapenzi kwasababu huwa yanafanywa kwa faragha kwahiyo hakutakuwa na namna ya kuwazuia hawa watu kwasababu hutawaona wakifanya
Kwani bangi inavutwa hadharani? Wauaji wanaua hadharani? Maawa ya kulevya yanatumiwa hadharani?
 
Back
Top Bottom