Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Napenda tu kuwakumbusha watawala wa Tanzania kuwa mambo yanaposhinda si vibaya kutaka msaada wa kiakili kutoka nchi zilizofanya vizuri.
Nasema hivi kwa maana naona gap kubwa ya uongozi mzuri katika Wizara na sekta nyingi Tanzania. Ukichunguza vizuri utaona mapungufu hayo kwa kweli yanatokana na kutojua, ujinga na 'lack of exposure' (Sijui utaiitaje hii) ushamba?
Si haramu kuwaajiri watu kutoka nje wakaziba pengo hilo angalau kwa muda hadi hapo tutakapokuwa na weledi sisi wenyewe, badala ya kujifunza kutokana na makosa....hili huchukua muda mrefu na husabisha hasara kubwa.
Ni wazi kabisa katika elimu, fedha, ustawi wa jamii, mipango miji, biashara, ardhi, benki.....Tanzania inahitajia akili kubwa. Katika Wizara na sekta chini ya Wizara hizo mambo ni ovyo ovyo.
Nitakumbusha tu, hata nchi zilizoendelea sana kama Marekani huazima 'akili kubwa' katika sekta zake. Ukienda NASA huko kumejaa kila aina ya watu kutoka India, Misri, Urusi nk.
Sekta ya Afya Uingereza, NHS, ukiwafukuza madokta kutoka India, Sudan, Nigeria.....hii leo, sekta nzima itaanguka! Mfano wa karibu ni Rwanda.
Nani walioendeleza Rwanda hadi kuwa na satalaiti yake yenyewe (jambo ambalo viongozi tulio nao hata hawajui umuhimu wake!) na mipango miji mizuri ya kuvutia? Ni wataalamu ambao Rwanda iliwakusanya kutoka nchi mbali mbali kutoka Uganda, Kenya, DRC na hata Tanzania.
Vyuo vikuu vya Rwanda hata vinadiriki kuwaajiri Wazungu kuwa wakuu wa chuo. Sisi tumeshikilia uzalendo njaa, hata uraia pacha hatuutaki! Pum..fu kabisa.
Hebu waajirini Wanyarwanda wale wale walioweka plan za miji yao, muone. Hebu mwajiri Waziri wa elimu wa Botswana aliyestaafu uone elimu inakuwaje Tanzania?
Hebu mwajiri Waziiri wa zamani wa fedha wa Kenya aliyeufanya uchumi wa Kenya kuondoka kwenye GDP ya USD 80b mwaka 2015 wakati huo ukifukuzana na wa Tanzania GDP USD 65 b, hadi leo ambapo uchumi wa Kenya umeushinda hata ule wa Ethiopia kwa ku click GDP USD 120 b, katika kipindi cha miaka 10 tu!, Wakati ule wa Tanzania uko hapo hapo!
Tanzania haitaukaribia tena uchumi wa Kenya, kama tuna Mawaziri hawa wa akili za tozo!
Ajabu ya Tanzania: twakubali kuajiri 'akili kubwa kutoka nje' katika jambo moja tu: mpira! Ila mambo ya maana...uzalendo wetu watuzuia!
Haya si mambo ya aibu wala kukosa uzalendo: ni ujanja, kwa kusoma kwa yule aliyekuzidi!