Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uwa nikiiangali serikali yetu,kiukwel nina akili kubwa kuliko wengi wao... ukweli usiopingika asilimia kubwa ya Watanzania bado ni wajinga au uwezo wa kufikiri ni mdogo ila wanatembelea bahati na uwezo wa waliowatanguliaNapenda tu kuwakumbusha watawala wa Tanzania kuwa mambo yanaposhinda si vibaya kutaka msaada wa kiakili kutoka nchi zilizofanya vizuri.
Nasema hivi kwa maana naona gap kubwa ya uongozi mzuri katika Wizara na sekta nyingi Tanzania. Ukichunguza vizuri utaona mapungufu hayo kwa kweli yanatokana na kutojua, ujinga na 'lack of exposure' (Sijui utaiitaje hii) ushamba?
Si haramu kuwaajiri watu kutoka nje wakaziba pengo hilo angalau kwa muda hadi hapo tutakapokuwa na weledi sisi wenyewe, badala ya kujifunza kutokana na makosa....hili huchukua muda mrefu na husabisha hasara kubwa.
Ni wazi kabisa katika elimu, fedha, ustawi wa jamii, mipango miji, biashara, ardhi, benki.....Tanzania inahitajia akili kubwa. Katika Wizara na sekta chini ya Wizara hizo mambo ni ovyo ovyo.
Nitakumbusha tu, hata nchi zilizoendelea sana kama Marekani huazima 'akili kubwa' katika sekta zake. Ukienda NASA huko kumejaa kila aina ya watu kutoka India, Misri, Urusi nk.
Sekta ya Afya Uingereza, NHS, ukiwafukuza madokta kutoka India, Sudan, Nigeria.....hii leo, sekta nzima itaanguka! Mfano wa karibu ni Rwanda.
Nani walioendeleza Rwanda hadi kuwa na satalaiti yake yenyewe (jambo ambalo viongozi tulio nao hata hawajui umuhimu wake!) na mipango miji mizuri ya kuvutia? Ni wataalamu ambao Rwanda iliwakusanya kutoka nchi mbali mbali kutoka Uganda, Kenya, DRC na hata Tanzania.
Vyuo vikuu vya Rwanda hata vinadiriki kuwaajiri Wazungu kuwa wakuu wa chuo. Sisi tumeshikilia uzalendo njaa, hata uraia pacha hatuutaki! Pum..fu kabisa.
Hebu waajirini Wanyarwanda wale wale walioweka plan za miji yao, muone. Hebu mwajiri Waziri wa elimu wa Botswana aliyestaafu uone elimu inakuwaje Tanzania?
Hebu mwajiri Waziiri wa zamani wa fedha wa Kenya aliyeufanya uchumi wa Kenya kuondoka kwenye GDP ya USD 80b mwaka 2015 wakati huo ukifukuzana na wa Tanzania GDP USD 65 b, hadi leo ambapo uchumi wa Kenya umeushinda hata ule wa Ethiopia kwa ku click GDP USD 120 b, katika kipindi cha miaka 10 tu!, Wakati ule wa Tanzania uko hapo hapo!
Tanzania haitaukaribia tena uchumi wa Kenya, kama tuna Mawaziri hawa wa akili za tozo!
Ajabu ya Tanzania: twakubali kuajiri 'akili kubwa kutoka nje' katika jambo moja tu: mpira! Ila mambo ya maana...uzalendo wetu watuzuia!
Haya si mambo ya aibu wala kukosa uzalendo: ni ujanja, kwa kusoma kwa yule aliyekupita!
Si lazima 'critical mass'. Ni zile sehemu muhimu kwa uchumi na maendeleo. Tena kwa muda mfupi mpaka wenyewe tuchukue. Vietnam ilifanya hivyo na sasa uchumi wa Vietnam ni mara tatu ya wa Tanzania at USD 261 billion, wakati ule wa Tanzania ni USD 61 Billion!Nakubali sana hoja hii. Lakini kuleta 'akili kubwa' pia kwaweza kuchangia mabadiliko katika sekta nyingine, hata uongozi. Kinachotakikana ni 'critical mass' ya hizo 'akili kubwa' ndipo wananchi waone kuna haja ya kubadilisha.
Hapo umesema. Air Tanzaia inataka CEO aliyefanya kazi hiyo akaleta ufanisi katika shirika ambalo lilikuwa linakufa. Kwa lugha ya Kiingereza mtu mwenye track record. Alas! Tanzania sharti kuu ni uwe mkereketwa wa CCM!Kuna maeneo mengine kuajiri toka soko la ajira la kimataifa si kukosa uzalendo. Mbona Kuna wakati Emirates( airline) waliajiri Muingreza kama CEO. Nissan ya Japan ilikuwa na CEO Mlebanon. Makocha wa soka n.k. Air Tz kmf. ikipata CEO mahiri huenda ikapona.
Sio waliotoa siri za nchi hii. Sema waliouza utu wa nchi hii ni watanzania wenyewe. Matanzania karibu yote ninayoyaona mtaani na yaliyomo serikalini na kwenye siasa ni matanzania mepesi sana kununulika. Wawe wasomi wasiwe wasomi yaani ni taabu tupu.Haya ndiyo niyasemayo ndugu. Ukiwa Tanzania bila kutoka ndio unakuwa na dhana hizi. Nani kakuambia kuwa mtu akiwa raia hawezi kuhatarisha usalama wa taifa? On the contrary, wengi waliotoa siri za nchi si wengine bali raia wenyewe.
Kwa hiyo hiyo broadband wanaoewa bure? Mbona nyie watu mna mawazo so mediocre? Tanzania iko kwenye top 10 big economies in GDP terms in Africa ikiwa ni pamoja na Nigeria, SA, Egypt, Algeria, Morocco, Kenya, Ethiopia, Ghana na Angola. Sasa hawa Rwanda mnataka watufundishe nini sisi? Labda Udikteta, wizi w madini ya DRC na kuua wapinzani
Hizo ni data za 2020 kurudi nyuma halafu zimeishia namba 8 tu. Tafuta za 2022 halafu uende hadi 10 au 11, Tanzania huwezi kuikosa
Sawa.Hizo ni data za 2020 kurudi nyuma halafu zimeishia namba 8 tu. Tafuta za 2022 halafu uende hadi 10 au 11, Tanzania huwezi kuikosa
Na karibia yote jamaa kasema uongo, eti GDP ya Kenya inaizidi ya Ethiopia,Hatuna cha kujifunza Rwanda bali tuna mengi ya kuwafunza kwa sasa na tuliwafunza sana toka Kagame aingie mwaka 1994 baada ya kumuua Habyarimana. Rwanda inayotawaliwa kimabavu huku kiongozi wake akiua wakosoaji kimya kimya popote walipo na kuwekeza kwenye PR ya akina Tony Blair haina cha kutufunza
Ni upuuuzi kufananisha hivyo "vimafanikio vya Rwanda" na nchi ya Tanzania. At most linganisha Rwanda na mkoa wa Mwanza.
Usitumalizie Bando kwa hoja kama hizi
Ndio maana wakiteuana tunaona kama vile wametoka mbinguni wanaleta miujiza wakati wapo miaka yote walewale recycling washibe upya wakishapungukiwa kiuchumi!Nakuunga mkono, ni hatari sana kuwapa watu wasio na exposure madaraka.