- Kwa Tz kama hakuna unasaba na kiongozi maarufu ndani ya CCM, hata uwe na akili kama Aristotle, Plato, Isaac Newton, Steve Job n.k, utaishia kutumika kama toilet paper.
- Kuajiri mgeni atataka weledi ili hali viongozi wanaotaka janjaanja, wizi n.k
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili la kwanza kwa kweli sijakufahamu kama unaunga mkono hoja yangu au una hoja mbadala.Ni sawasawa kabisa pande zote zinaweza kuhatarisha usalama wetu lakini ilivyo katika ada sekta kubwa na nyeti zote hupewa raia wa nchi. Haitojalisha kama ni Muhindi, Mzungu au Mswahili madamu ni raia wetu anayo haki ya kukabidhiwa nafasi na si kwa raia wa kigeni.
Hii haiondoi dhana ya kwamba bado raia wa Tanzania wenyewe wanao uwezo wa kupeleka mustakabali wa nchi wao wenyewe pasi na msaada wa kiutawala kutoka nchi au raia wa nchi nyingine.
Pia tu nikukumbushe tu yakuwa mimi na wewe hatujuani ninapoleta hoja yangu kisha ukamalizia kuwa ndio shida ya Mtanzania ambae hajatoka, una uhakika gani mawazo haya yangu yanaakisi ukweli wako kuwa mimi au sisi Watanzania wenye mawazo kama yangu hatujapata exposure ya maisha ama elimu nje ya nchi? Tafadhali tujadili hoja.
Mimi nadhani mawaziri wasingekuwa wanatokana na ubunge,mawaziri waajiriwe na serikali,yaani nafasi zitangazwe na vigezo husika viwekwe watu waliosoma wagombee hizo nafasi.
Pasipo hivyo hakuna kitakachofanyika kwasababu kila kitu kimekaa kisiasa!.
Unakuta Rais anateua waziri let say wa kilimo wakati yeye hakusomea kilimo kasomea Engineering,hii siyo sawa na ndiyo maana unaona tunapiga makitaimu kila leo,hizi nafasi za wakuu wa mikoa ni kuziondoa na wabaki Ras na Das na nafasi zao pia wagombee.
Bila hivyo tutazunguka palepale.
Kabisa.Watu wenye uwezo wapo wengi tu hapa nchini.
Ila watawala wameshatengeneza circle yao ambayo kama haumo humo kamwe huwezi pata nafasi hata uwe na akili kama Isack Newton.
Hua wanasema wakwetu huyo. Kama wewe sio wakwao. Sahau.
Ndio maana mtu anaiba hapa wanamwamishia kule.
Mawaziri wapo bize kutupia pongezi kwa Mh. Raisi, kulumbana na vijana online, kijejeli hoja, n.k.Extremely good read, thanks. However, examples given therein are of Kenyan officials, who are more serious than ours. Simon Nyachae was working 14 hours a day! Show me one Tanzanian minister working six hours a day and I will show you a camel with four humps!
Wewe jamaa ungekuwa kwetu ningekuzawadia Ng'ombe watano. Ni kweli kinachotutesa ni kukosa Exposure. Na tunaamini zaidi ufaulu wa darasani tena uwe umesoma chuo kama UDSM yaani wewe unaonekana ni KAMUSI INAYOTEMBEA.Waziri anatoka kijijini anaingia chuo KiKUU akimaliza kwa Kua Alipata Ufaulu mkubwa anapelekwa serikalini anagombea ubunge na anakua waziri
Hakuna exposure at all , waziri kama huyo ni Mzigo Hawezi kuleta ubunifu na akili za Darasani sio akili za Maisha
Nitumie Mkuu husinyime Riziki ya Ng'ombe nitalipia usafiri 😄😄😄Wewe jamaa ungekuwa kwetu ningekuzawadia Ng'ombe watano. Ni kweli kinachotutesa ni kukosa Exposure. Na tunaamini zaidi ufaulu wa darasani tena uwe umesoma chuo kama UDSM yaani wewe unaonekana ni KAMUSI INAYOTEMBEA.
KUNA MAMBO NCHI HII YANAUMIZA SANA. HUWA NATAMANI MUNGU AINGILIE KATI.
MUDA MWINGINE NATAFAKARI LILE WAZO KUWA SISI WAAFIRIKA MAISHA HAYA YA MIJINI/ CIVILIZATION HAYAKUWA YETU ILA TUMELAZIMISHWA TU NA WALIOTUTAWALA. JAMANI MTU MWEUSI ANA MENGI YANAYOMTOFAUTISHA NA MTU MWEUPE KITABIA NA KIFIKRA. NJOONI HATA USA MTAONA HAWA NDUGU ZETU WAKINYAMWEZI NI WATU NI HOVYOO SANA TU.
Watu wenye uwezo wako wengi. Hilo Nakubaliana na wewe. Ila wengi hao hawana exposure ya kutosha kutupeleka tunakotaka. Siamini kama mtu aliyesomea na kufanya kazi maisha yake yote Tanzania ana same skills na knowledge kuliko aliyewahi kutoka nje ya nchi.Watu wenye uwezo wapo wengi tu hapa nchini.
Ila watawala wameshatengeneza circle yao ambayo kama haumo humo kamwe huwezi pata nafasi hata uwe na akili kama Isack Newton.
Hua wanasema wakwetu huyo. Kama wewe sio wakwao. Sahau.
Ndio maana mtu anaiba hapa wanamwamishia kule.
🤣 🤣🤣Nitumie Mkuu husinyime Riziki ya Ng'ombe nitalipia usafiri 😄😄😄
Bandiko mujarabu hili.Napenda tu kuwakumbusha watawala wa Tanzania kuwa mambo yanaposhinda si vibaya kutaka msaada wa kiakili kutoka nchi zilizofanya vizuri.
Nasema hivi kwa maana naona gap kubwa ya uongozi mzuri katika Wizara na sekta nyingi Tanzania. Ukichunguza vizuri utaona mapungufu hayo kwa kweli yanatokana na kutojua, ujinga na 'lack of exposure' (Sijui utaiitaje hii) ushamba?
Si haramu kuwaajiri watu kutoka nje wakaziba pengo hilo angalau kwa muda hadi hapo tutakapokuwa na weledi sisi wenyewe, badala ya kujifunza kutokana na makosa....hili huchukua muda mrefu na husabisha hasara kubwa.
Ni wazi kabisa katika elimu, fedha, ustawi wa jamii, mipango miji, biashara, ardhi, benki.....Tanzania inahitajia akili kubwa. Katika Wizara na sekta chini ya Wizara hizo mambo ni ovyo ovyo.
Nitakumbusha tu, hata nchi zilizoendelea sana kama Marekani huazima 'akili kubwa' katika sekta zake. Ukienda NASA huko kumejaa kila aina ya watu kutoka India, Misri, Urusi nk.
Sekta ya Afya Uingereza, NHS, ukiwafukuza madokta kutoka India, Sudan, Nigeria.....hii leo, sekta nzima itaanguka! Mfano wa karibu ni Rwanda.
Nani walioendeleza Rwanda hadi kuwa na satalaiti yake yenyewe (jambo ambalo viongozi tulio nao hata hawajui umuhimu wake!) na mipango miji mizuri ya kuvutia? Ni wataalamu ambao Rwanda iliwakusanya kutoka nchi mbali mbali kutoka Uganda, Kenya, DRC na hata Tanzania.
Vyuo vikuu vya Rwanda hata vinadiriki kuwaajiri Wazungu kuwa wakuu wa chuo. Sisi tumeshikilia uzalendo njaa, hata uraia pacha hatuutaki! Pum..fu kabisa.
Hebu waajirini Wanyarwanda wale wale walioweka plan za miji yao, muone. Hebu mwajiri Waziri wa elimu wa Botswana aliyestaafu uone elimu inakuwaje Tanzania?
Hebu mwajiri Waziiri wa zamani wa fedha wa Kenya aliyeufanya uchumi wa Kenya kuondoka kwenye GDP ya USD 80b mwaka 2015 wakati huo ukifukuzana na wa Tanzania GDP USD 65 b, hadi leo ambapo uchumi wa Kenya umeushinda hata ule wa Ethiopia kwa ku click GDP USD 120 b, katika kipindi cha miaka 10 tu!, Wakati ule wa Tanzania uko hapo hapo!
Tanzania haitaukaribia tena uchumi wa Kenya, kama tuna Mawaziri hawa wa akili za tozo!
Ajabu ya Tanzania: twakubali kuajiri 'akili kubwa kutoka nje' katika jambo moja tu: mpira! Ila mambo ya maana...uzalendo wetu watuzuia!
Haya si mambo ya aibu wala kukosa uzalendo: ni ujanja, kwa kusoma kwa yule aliyekupita!
Wakenya Hawa Hawa wanaokufa kwa njaa ndo wanauchumi mkubwa?Napenda tu kuwakumbusha watawala wa Tanzania kuwa mambo yanaposhinda si vibaya kutaka msaada wa kiakili kutoka nchi zilizofanya vizuri.

Soma ndugu yangu usisikize ya kuambiwa. Angalau ukisikia la kuambiwa, changanya na zako! Kenya iko mbali sana na tukicheza hatuifikii tena, ingawaje tuna mali zaidi na mahindi kuliko wao, ndiyo!Wakenya Hawa Hawa wanaokufa kwa njaa ndo wanauchumi mkubwa?