Si vibaya kuajiri akili kubwa kutoka nje!

Wananchi tungekuwa na mamlaka ni bora tununue management ya kutuongoza toka nje ya nchi na sio hawa ccm, kwao uongozi ni ajira. Tunanunua menejiment toka nje ukiperform chini ya kiwango tunakupiga chini. Kama tunaweza ajiri makocha toka nje, kwann tusiajiri Rais na timu yake toka nje watuongoze?
 
Tanzania akili ni zile zile yaani watu wale wale walioko kweny mfumo miaka kibao hii imetokana na kufanya siasa kabla ya maendeleo...Better kuwa na utawala wa kifalme kimkakati kutopoteza nguvu za kupoteza pesa kweny kuomba kura instead watu wanabase kweny kutengeza taifa kwa ujumla na wenyewe uwezo ndo wawe kipaumbele , leo wapo watu Wana uwezo lakini kutokana na siasa hawawezi kuingia kweny mfumo na kusaidia taifa mwingine anataka mpaka awe raisi nchi ndo aweze kulisaidia
 
Ubaya wa Mwanza uko wapi? Au unalinganisha kale kapicha ka mtaa mmoja wa Kigali wenye maghorofa na barabara ukadhani Rwanda yote iko vile?
Rwanda especially kigali iko very articulated in terms of residents and infrastructure networks , city sewage system na mavitu kibao tuwape credit hina tatizo kubishana .

Mwanza iko poa pia ila kwa kweli vile vinyumba kwa juu vinatia aibu ila naona mbali sana coz vinatolewa mpango uko mezani .

Mwanza kwangu ni jiji zuri sana sema pale centre harufu ya dagaa inatia njaa yaani unaona utamu utamu sana kule kunatamanisha kula kila mda.
 
Haya ndiyo niyasemayo ndugu. Ukiwa Tanzania bila kutoka ndio unakuwa na dhana hizi. Nani kakuambia kuwa mtu akiwa raia hawezi kuhatarisha usalama wa taifa? On the contrary, wengi waliotoa siri za nchi si wengine bali raia wenyewe.
Ni sawasawa kabisa pande zote zinaweza kuhatarisha usalama wetu lakini ilivyo katika ada sekta kubwa na nyeti zote hupewa raia wa nchi. Haitojalisha kama ni Muhindi, Mzungu au Mswahili madamu ni raia wetu anayo haki ya kukabidhiwa nafasi na si kwa raia wa kigeni.
Hii haiondoi dhana ya kwamba bado raia wa Tanzania wenyewe wanao uwezo wa kupeleka mustakabali wa nchi wao wenyewe pasi na msaada wa kiutawala kutoka nchi au raia wa nchi nyingine.

Pia tu nikukumbushe tu yakuwa mimi na wewe hatujuani ninapoleta hoja yangu kisha ukamalizia kuwa ndio shida ya Mtanzania ambae hajatoka, una uhakika gani mawazo haya yangu yanaakisi ukweli wako kuwa mimi au sisi Watanzania wenye mawazo kama yangu hatujapata exposure ya maisha ama elimu nje ya nchi? Tafadhali tujadili hoja.
 
Mshua hii makitu umeongea ukweli tupu.
Nakubaliana sana na wewe hapa.
 
Hujafika rwanda sikulaum ...ila rwanda ipo very organized licha ya kuwa na milima mingi. Kingine ni usafi wenzetu wamejitahidi sana kutunza mazingira.
Unachukua rais amezaliwa na kukulla kwenye mazingira ya uchafu, unategemea nini?
 
The best post this year. Maofisini kumejaa upumbavu, mtu analipwa mamilioni ya walipakodi bado anafanya kazi anavyojisiikia. Issue ndogo serikalini it takes months to be resolved. Idiots
 
Wewe ni mfuasi wa chadema.
 
Mawaziri hawa wa akili za tozo hahhahahahahahaha Mwigulu kijembe hicho
 
Kukosa exposure kwa baadhi ya viongozi ni janga kwa taifa ebu angalia waziri Kama Nape hana exposure yeyote alafu mtu Kama huyu alete mageuzi kwenye sekta ya mawasiliano na habari kweli?

Watu wenye uwezo siku zote huwa na self confidence hivyo kushindwa kuwa chawa ili kupata teuzi lakini mtu asiye na uwezo lazima awe chawa na kwa kuwa viongozi wetu wanapenda sifa na kuambiwa kile wanacho penda kusikia basi huzungukwa na watu wenye uwezo mdogo matokeo yake ndo aya kiongozi kuwa myopic Kama watu wake.

Mbona ni ukweli ulio wazi baadhi ya nchi au mashiriki fulani uko duniani hununua uongozi kwenye baadhi ya maeneo mfano shirika la Qatar airways limenunua uongozi toka British Kama sija kosea na linafanya vizuri hii pia kuna mdau kaigusia Rwanda naona walitambua hili mapema wakanunua uongozi,

Hongera mleta uzi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wewe ndiyo mpumbavu ila siyo Mimi kama unadhani ku assemble magari ni big deal. Hapo ni transfer pricing tu inafanyika. Tz tulifanya assembling pale Nyumbu kwa kuwanda cha TPDF na pale TAMCO Kibaha kwa magari ya Scania.

Bado nasema ni kujidogosha kujioima na Rwanda. Kama wewe ni mhutu au mtusi endelea kutoa povu
 
Kwa hiyo hiyo broadband wanaoewa bure? Mbona nyie watu mna mawazo so mediocre? Tanzania iko kwenye top 10 big economies in GDP terms in Africa ikiwa ni pamoja na Nigeria, SA, Egypt, Algeria, Morocco, Kenya, Ethiopia, Ghana na Angola. Sasa hawa Rwanda mnataka watufundishe nini sisi? Labda Udikteta, wizi w madini ya DRC na kuua wapinzani
 
Hujafika rwanda sikulaum ...ila rwanda ipo very organized licha ya kuwa na milima mingi. Kingine ni usafi wenzetu wamejitahidi sana kutunza mazingira.
Kwani usafi nani kakumbia Tanzania hakuna majiji masafi? Umefika Moshi wewe au Iringa?
 
Kama waziri wa fedha asiyejua kutetea mfumo wa kutumia bank kufanya malipo, kuweka akina n.k kwa kuondoa tozo.
Jingine la latra kutojua umuhimu wa mfumo wa Uber au Bolt katika usafiri wa mijini ni usalama wa Abiria pia wa dereva
 
Vyuo vikuu vya Rwanda hata vinadiriki kuwaajiri Wazungu kuwa wakuu wa chuo.

 
 
Tatizo la hii nchi sio ukosefu wa watu,tatizo letu ni mfumo mbovu unaotulazimisha wote wananchi na viongozi kua kwenye kapu moja la ujinga.Bila kubadilisha huo mfumo hata watakaotoka nje hawataweza kufanya mageuzi yoyote.Siku tutakayopata akili yakujijua kua wote tumekwama kwenye kapu moja tukabadilisha huo mfumo ndio siku tutakayoweza kupiga hatua.Kwasasa usitegemee jambo lolote jipya linalotokana na big brain kwasababu viongozi wote wanawaza namna yakumsifia rais badala yakuwaza kuboresha mazingira yao ya kazi ili kuleta manufaa kwa nchi.
 
Hilo pia linaunga mkono hoja yangu. Ni ujinga, ushamba na uhaba wa uzoefu ndio ulikopelekea janga hilo. Kuajiri akili kubwa si mzungu tu, kama watu wanavyodhania. Anaweza kuwa Mkongomani, Mganda, Mkenya.....kama Rwanda ilivyofanya. Wazungu huajiri Waafrika tele! Weee waenda kuchuku mijizungu tu kutoka Afrika Kusini wategemea nini? Si hata makocha wazungu hushindwa na ligi ya Bongo?
Halafu jambo moja ambalo ni special kwa Tanzania: kwa vile kuna deficit kubwa ya elimu, kila aliyesoma kidogo anaona YEYE tu ndiye anayehodhi ujuzi wote, na aghalabu hataki ushauri wa yeyote. Tumeliona hili kwa Nyerere, Mkapa .....
Pengine ilivyotokea ni kuwa hayati Mkapa aliamka siku moja akaamuru Wasauzi hao waajiriwe Tanesco bila hata kushauri, maana yeye anajua zaidi! After all, hayati alikuwa business nyingi huko Sauzi!
 
Nakubali sana hoja hii. Lakini kuleta 'akili kubwa' pia kwaweza kuchangia mabadiliko katika sekta nyingine, hata uongozi. Kinachotakikana ni 'critical mass' ya hizo 'akili kubwa' ndipo wananchi waone kuna haja ya kubadilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…