Si vibaya kuajiri akili kubwa kutoka nje!

  • Kwa Tz kama hakuna unasaba na kiongozi maarufu ndani ya CCM, hata uwe na akili kama Aristotle, Plato, Isaac Newton, Steve Job n.k, utaishia kutumika kama toilet paper.
  • Kuajiri mgeni atataka weledi ili hali viongozi wanaotaka janjaanja, wizi n.k
 
Hili la kwanza kwa kweli sijakufahamu kama unaunga mkono hoja yangu au una hoja mbadala.
Hili la pili la kutoka nje, naomba samahani. Pengine ni kweli ulitoka nje ya nchi. Ila suala si kutoka nje pekee. Ni kutoka nje na kuangalia kwa tafakari. Wengi huenda nje lakini hawaoni tofauti yeyote na Bongo zaidi ya uzuri wa barabara na madem! Ulipotoa hoja kuwa wageni wasiajiriwe kwa vile watavujisha siri za nchi....!?
 
Mimi nadhani mawaziri wasingekuwa wanatokana na ubunge,mawaziri waajiriwe na serikali,yaani nafasi zitangazwe na vigezo husika viwekwe watu waliosoma wagombee hizo nafasi.
Pasipo hivyo hakuna kitakachofanyika kwasababu kila kitu kimekaa kisiasa!.

Unakuta Rais anateua waziri let say wa kilimo wakati yeye hakusomea kilimo kasomea Engineering,hii siyo sawa na ndiyo maana unaona tunapiga makitaimu kila leo,hizi nafasi za wakuu wa mikoa ni kuziondoa na wabaki Ras na Das na nafasi zao pia wagombee.

Bila hivyo tutazunguka palepale.
 

Gwajima kwenye Afya alifanya nini? Kama sio bangi tu
 
Kabisa.
 
Extremely good read, thanks. However, examples given therein are of Kenyan officials, who are more serious than ours. Simon Nyachae was working 14 hours a day! Show me one Tanzanian minister working six hours a day and I will show you a camel with four humps!
 
Mifano hai ni mingi mno.
  • Kwenye orodha ya matajiri 10 bora, je Watanzania ni % ngapi? (Tafakari)
  • Hata makanisa yanaakisi ukweli. Makanisa yenye mchanganyiko wa uongozi ni tofauti na yenye 'wanavijiji' Tu.
  • Waandamizi serikalini ni akina Nape, January, .....; kule Bugeni kuna Msukuma, Babu Tale, ..... Nimemkumbuka yule aliyemshukuru Magufuli kwa kumtoa jalalani (UDSM). Serious! Eti tunataka maendeleo
  • Hata haya makampuni makubwa ya kibiashara yangekuwa yanaendeshwa na wabongo, wangekwisha fungasha virago.
 
Mawaziri wapo bize kutupia pongezi kwa Mh. Raisi, kulumbana na vijana online, kijejeli hoja, n.k.
Hakuna kiongozi aliye tayari kwa mjadala hu n
 
Tatizo siyo watu, tatizo mfumo mbovu. Hapo fedha hata akiwekwa mshindi wa tuzo ya Nobel kwenye mambo ya uchumi hawezi kufanya la maana.
 
Tatizo siyo watu, tatizo mfumo mbovu. Hapo fedha hata akiwekwa mshindi wa tuzo ya Nobel kwenye mambo ya uchumi hawezi kufanya la maana.
Nakubali. Ila uwozo ni maradufu ikiwa mfumo ni yai viza na Waziri naye ni kichwa-hewa!
 
Wewe jamaa ungekuwa kwetu ningekuzawadia Ng'ombe watano. Ni kweli kinachotutesa ni kukosa Exposure. Na tunaamini zaidi ufaulu wa darasani tena uwe umesoma chuo kama UDSM yaani wewe unaonekana ni KAMUSI INAYOTEMBEA.

KUNA MAMBO NCHI HII YANAUMIZA SANA. HUWA NATAMANI MUNGU AINGILIE KATI.

MUDA MWINGINE NATAFAKARI LILE WAZO KUWA SISI WAAFIRIKA MAISHA HAYA YA MIJINI/ CIVILIZATION HAYAKUWA YETU ILA TUMELAZIMISHWA TU NA WALIOTUTAWALA. JAMANI MTU MWEUSI ANA MENGI YANAYOMTOFAUTISHA NA MTU MWEUPE KITABIA NA KIFIKRA. NJOONI HATA USA MTAONA HAWA NDUGU ZETU WAKINYAMWEZI NI WATU NI HOVYOO SANA TU.
 
Nitumie Mkuu husinyime Riziki ya Ng'ombe nitalipia usafiri πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Niliwah kuongea hili,tatizo letu hatuna viongozi wenye maono,nadhani kuna shida kwenye mifumo yetu ya elimu,tunazalisha kizazi ambacho hakiwezi kujiongoza...Wenzetu kina Nyerere walipata Elimu ya mzungu,tazama uwezo wao ulikuwaje.
 
Watu wenye uwezo wako wengi. Hilo Nakubaliana na wewe. Ila wengi hao hawana exposure ya kutosha kutupeleka tunakotaka. Siamini kama mtu aliyesomea na kufanya kazi maisha yake yote Tanzania ana same skills na knowledge kuliko aliyewahi kutoka nje ya nchi.

Huyu Mwigulu kama kweli ni ni first class na ni presidental material kama anavyodai angepata chance ya kukaa na kufanya kazi nje naamini angeweza kufanya bora kuliko sasa..... Probably hata Mahera.

Tatizo kubwa la Watanzania ni mindset.
 
Mpeni wizara ya fedha ruth Zaipuna yule CEO wa NMB mpeni uhuru afanye yake naamini baada ya miaka miwili wizara ya fedha itaongoza kwa ubunifu
 
Bandiko mujarabu hili.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Wakenya Hawa Hawa wanaokufa kwa njaa ndo wanauchumi mkubwa?
 
Wakenya Hawa Hawa wanaokufa kwa njaa ndo wanauchumi mkubwa?
Soma ndugu yangu usisikize ya kuambiwa. Angalau ukisikia la kuambiwa, changanya na zako! Kenya iko mbali sana na tukicheza hatuifikii tena, ingawaje tuna mali zaidi na mahindi kuliko wao, ndiyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…