Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 3,189
- 6,140
Pamoja na matumizi ya mabavu katika kuhakikisha CCM inasalia madarakani, Nchi hii haijawahi kushuhudia uchaguzi uliosuswa na kuleta unyonge katika mioyo ya watanzania kama uchaguzi huu wa mwaka 2025.
Wakati ule CHADEMA ilipokuwa na kasi mno na hata matukio ya vurugu yalikuwepo sana tu na yalirushwa katika vyombo vya habari kama ITV na katika magazeti mbalimbali, tukiwakumbuka waandishi mashuhuri kama kina Sam mahela na wengineo wakireport LIVE kutoka maeneo yenye matukio.
Pamoja na yote hayo viongozi walipatikana na kwa kiasi fulani walikubalika na hata katika siku za chaguzi haijawahi kutokea biashara zikafungwa au watu wakajifungia ndani na mitaa kubaki empty. Yaani ni kama nchi ilikuwa msibani.
Nyakati hizo si tu katika chaguzi bali hata katika sherehe za kuapishwa kulikuwa na Nuru na amani miongoni mwa wengi.
Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa tofauti kushuhudiwa kupita chaguzi zote zilizowahi kufanyika Tanzania, Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba pamoja na cama kikuu cha upinzani ambacho kwa miaka mingi ndicho kimekuwa kikileta hekaheka lakini CHADEMA haijashiriki kabisa uchaguzi huu na ndiyo uchaguzi uliokuwa na umwagaji damu mkubwa pengine kuliko chaguzi zote tulizoshuhudia.