Siamini nilichokishuhudia: daladala level seat, hakuna foleni, hakuna kelele, abiria hawasukumani, makonda hawatukani, unafika haraka unakoenda

pesa ya mafuta bei gani ? pesa ya boss bei gani ? posho ya dereva ? posho ya konda ? mshahara wa dereva ??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weee unafurahia wakati hesabu ya boss inasumbuana sumatra kodi iko pale pale kinachouma ni kwa nini mwendo kasi wao wajazwe kiasi na daladala wao levo siti
 
Weee unafurahia wakati hesabu ya boss inasumbuana sumatra kodi iko pale pale kinachouma ni kwa nini mwendo kasi wao wajazwe kiasi na daladala wao levo siti

Mzee hata mabasi ya kwenda mikoani kulikuwa na hoja hizihizi, abiria walikuwa wanasimama mpaka wanabanana ilifika mida tukaelewana.
 
Hebu tuongee kama watu wazima wenye akili timamu, foleni inapunguaje barabarani kwa watu kukaa level seat? Sio kwamba kuna factor nyingine imehusika?
Yaani mimi mwenyewe nimeshangaa sana hilo swala na kuwashangaa wachangiaji wanavyotiririka bila kuwaza kwa kina kuwa foleni imepungua kutokana watu wengi kutokumove sana from one place to another na sio kwasababu daladala zimepakia level seat.
Kama idadi ya abiria ni ile ile basi level seat itapelekea kuwa na foleni zaidi Barabarani mfano gar moja ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 50 sasa hivi hao abiria 50 itabidi wabebwe na daladala 2 so utaona kuna ongezeko la gari moja la zaida hapo.
Na ikiwa wamiliki wa daladala wataamua kupaki magari yao kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa kutokana na kupakia level seat hii itapelekea kuwa na msongamano wa abiria vituoni. refer vituo vya mwendokasi kimara na kwingineko
 
Wewe una mawazo kuwa magari yataongezeka barabarani na hivyo kusababisha foleni. Shida sio wingi wa magari, tatizo ni matatizo, mfano haya yanayosababishwa na daladala na madereva wengine wazembe, na miundombinu mibovu. Hapahapa Dar kama kila gari likiendeshwa kwa kuzingatia sheria na taratibu kuna sehemu unaweza kusimama katikati ya barabara kwa muda mrefu na usione gari, ndio utatambua kuwa kumbe Dar hakuna magari ukilinganisha na majiji mengine duniani ambako hakuna foleni lakini magari ni mamilioni.
 
1) Kuna maofisi wamafunga hivyo abiria wamepungua kiasi. Corona ikiisha abiria wakarudi itakuaje?

2) Abiria wanaopandia vituo vya njiani itakuaje nao kwa sasa?
 
Na yale mabomba ya kushika juu kwa waliokuwa wanasimama yaondolewe. Makonda waliyapenda sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swala la traffic kuongoza magari wakati mataa yapo linakera mno na mara nyingine huwa chanzo cha foleni kwani hawajui kubalance kabisa ...
 
Hakuna hela hapo mkuu, hujatoa hela ya Boss, mafuta, posho na pesa ya kiwi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We buyu kweli kabisa
 
Pita njia ya mbagala , temeke, buza , keko huko utakuta watu wanatembea kwa mguu je hicho ndio unakitaka? Ivi wale abiria wa mwendokasi wa kimara wanaogombania mwendokasi unahisi now wanafanyaje shuguri zao?


Sent from my iPhone using JamiiForums
Kimara wanapanga foleni mkuu, tena leo foleni inaweza kufika nje[emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1) Kuna maofisi wamafunga hivyo abiria wamepungua kiasi. Corona ikiisha abiria wakarudi itakuaje?

2) Abiria wanaopandia vituo vya njiani itakuaje nao kwa sasa?
Hivyo vya njiani abiria wanashuka na wengine wanapanda. Tembea au fanya namna yoyote nenda kituoni penye gari, vituo haviko mbali na makazi. Nilichoeleza ni kwamba huu utaratibu unapunguza foleni na kuleta ustaarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…