TensorFlow
JF-Expert Member
- Feb 11, 2020
- 993
- 1,286
- Thread starter
- #81
Hakuna hela hapo mkuu, hujatoa hela ya Boss, mafuta, posho na pesa ya kiwi
Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyohiyo watagawana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna hela hapo mkuu, hujatoa hela ya Boss, mafuta, posho na pesa ya kiwi
Sent using Jamii Forums mobile app
1.) Kwa mfano wa Corona ulioutolea, vifo nchini Tanzania vimeongezeka kisa Corona? Ndio sawa na wewe ulivyosema foleni imepungua kwa factor moja tu ya daladala vituoni, ndio uje useme vifo Tz vimeongezeka kwa factor moja tu ya Corona, ilihali unajua factor ni nyingi mno!1. Wewe huelewi nini? Vituo vingi (tena karibu vyote) vina capacity ya daladala moja au mbili, zikija daladala kumi kila moja inataka kusimama na kuchukua abiria zingine zitalazimika kupark au kusimama barabarani (kumbuka wakati huo tayari zina abiria na wengine wamesimama). Tena tabia za madereva wa daladala ni kumblock wa nyuma yake ili asichukue abiria. Matatizo hayo hayatakwepo kwa sababu daladala ikiondoka kituo cha kwanza itakuwa ina abiria waliojaa gari na hivyo hakuna sababu ya kusimama ovyo njiani. Swali lako linafanana na hili "Hivi tunahangaika n corona, kwani corona tu ndio ugonjwa hatari au tatizo?". Kuwepo kwa sababu zingine zinazosababisha foleni kama vile barabara finyu, mbovu, nk., sio sababu ya kuzuia kuchukua hatua fulani inayoonyesha kupunguza foleni.
2. Hapana
Uzi wangu hauongelei foleni tu. Unaongelea afya, utu, ustaarabu, iwapo mikakati sahihi ya kubebwa abiria itazingatiwa. Jambo jingine, leseni zote za daladala zinataka abiria wote wawe wamekaa kwenye siti -- ni sheria. Sasa kwa nini isifuatwe?
Sasa wewe inabidi watu wengine wakusaidie.1.) Kwa mfano wa Corona ulioutolea, vifo nchini Tanzania vimeongezeka kisa Corona? Ndio sawa na wewe ulivyosema foleni imepungua kwa factor moja tu ya daladala vituoni, ndio uje useme vifo Tz vimeongezeka kwa factor moja tu ya Corona, ilihali unajua factor ni nyingi mno!
Nauli kuangaliwa upya sawa. Wanafunzi walipe nauli. Katika hali ya kawaida daladala hukubali wanafunzi mmoja, wawili, labda mwisho watatu.Nauli ya daladala mara ya mwisho ilipandishwa mwaka ____ wakati ambapo bei ya mafuta kwa lita ilikuwa shilingi _____. Toka mwaka huo, nauli imebaki vilevile, japo mafuta yamepanda bei. Hasara inafidiwa kwa abiria kurundikana. Kurudisha utaratibu wa levo siti kunaweza kusababisha kulazimika kuangalia upya nauli husika.
Starehe Gharama.
Na, je, shule zikifunguliwa, wanafunzi nao watakaa kwenye levo-siti? Starehe Gharama!
Nauli kuangaliwa upya sawa. Wanafunzi walipe nauli. Katika hali ya kawaida daladala hukubali wanafunzi mmoja, wawili, labda mwisho watatu.
Sasa hili ni jibu au pendekezo? Maana lile ni swali linalotegemea jibu na sio pendekezo, huna jibu piga kimya na acha hoja yangu iende zake bila kikwazo.Sasa wewe inabidi watu wengine wakusaidie.
Ndio maana nimesema usaidiwe na wengine ili hoja yako iendelee mbele.Sasa hili ni jibu au pendekezo? Maana lile ni swali linalotegemea jibu na sio pendekezo, huna jibu piga kimya na acha hoja yangu iende zake bila kikwazo.
Hoja zako zina mantiki sana. Mimi huwa nashangaa hili la wanafunzi kulipa nauli sijui nusu! Mfano, mimi sio tajiri lakini sioni sababu ya mtoto wangu kulipa nusu nauli ya daladala, atalipa hela kamili.Nanukuu posti yangu kwenye uzi wa:
Wenye magari binafsi watoe lift kwa watoto wa shule vituoni ili mbarikiwe - JamiiForums
*UFUMBUZI WA KUDUMU WA TATIZO LA USAFIRI KWA WANAFUNZI*
Ufumbuzi wa masuala ya usafiri wa watoto shuleni usio na kelele wala mikwaruzo ni huu hapa:
1. Kila shule ya umma ichorewe ramani ya nyumba zinazoizunguka (catchment). Mikusanyiko ya mashule ambayo mtoto anaweza kuenda kwa kutembea itaunganishwa na kufanywa kanda (zone ) (matumizi ya GIS hapa ndio pake 😎). Ni shurti kila mtoto aliyeko kwenye kanda fulani asome shule ya umma iliyoko kanda hiyo au akakae bweni. Mtoto yoyote akiamua kusoma shule ya binafsi ruksa kusoma popote. Lakini asisumbue watu kuhusu usafiri.
2. Wanafunzi wote watakaopanda mabasi walipe nauli sawa na ya mtu mzima. (yunifomu alizovaa, viatu, madaftari, penseli, kalamu ya wino, viepe vya lanchi ya mchana 😉 , vyote hivyo hulipa kamili siyo nusu bei. Kwa nini kwenye madaladala tu ndio iwe nusu nauli?)
3. Mwanafunzi ambaye atalazimika kupanda basi kwenda shule ya umma, na hana uwezo wa kujilipia nauli kamili, apewe ruzuku kupitia kwa Afisa Elimu wilaya, ambaye atathibitisha kuwepo kwa sababu za msingi kwa nini mwanafunzi huyo hakai bweni au hasomi shule ya karibu.
Easy-peasy-lemmon-squeazy
REJEA: Starehe Gharama
https://www.asymptotejournal.com/blog/2019/08/06/translation-tuesday-comfort-is-expensive-by-mlenge-mgendi
Mbona mama yako ndio alikuwa ananipa lifti mkuuyule mdada aliyekuwaga anakupa lift ukamtaka akakuchana umu mliishia wapi?
Sent using Jamii Forums mobile app
Dada unaenda wapi..naenda Temeke..Level seat kwa daladala za Temeke Mbezi mbona zimegoma?!
Unaongelea za daladala zipi mkuu mie nipo hapa Mbezi shamba yaani ni vurugu tupu watu wanagombana ili kuwahi seat na bado waliokosa seat wanan'gan'gania kuingia tu kwa kubanana
Sent using Jamii Forums mobile app
Hesabu yako ina assume gari linatumia maji badala ya mafuta. Weka Trip moja inatumia mafuta kiasi gani? Weka gharama ya vipuli na service kisha igawanye kwa siku.Hata hivyo watapata tu hela tena bila shida. Assume daladala itaenda mjini safari tano kwa siku. Kwa hiyo kwenda na kurudi ni trip 10. Kila daladala inabeba abiria 31. Kama kila abiria atatoa TZS 400, maana yake kwa siku konda atakusanya 10 x 31 x 400 = TZS 124,000. Hapo hatuhesabii anayepanda na kushuka njiani na mwingine kupanda.
Pia magari yatakuwa kwenye hali nzuri kwa sababu hawatayaoverload, hivyo kupungua kwa gharama ya service.
Corona ikiisha tupate faida zifuatazoHata kama corona ikiisha halafu mtu akatangaza kuwa sasa daladala zinaruhusiwa kujaza watu kama magunia kama ilivyokuwa mwanzo nitamshangaa sana. Kila mtu kukaa kwenye seat yake ni tija kwa afya ya msafiri, kiakili, kimwili na kisaikolojia. Kwa mara ya kwanza leo nimepanda daladala na kwenda ninakoenda na kurudi bila kichwa kuvurugika kwa sababu ya kelele, matusi, foleni na bughdha mbalimbali za daladala na makonda wao.
Kwa maoni yangu, huu ni utaratibu ambao waziri au mamlaka zinazohusika zilitakiwa kuchukua hatua tangu siku nyingi na kuusimamia. Ndio leo nagundua kuwa foleni na misongamano vituoni na barabarani kisababishi kikubwa kilikuwa ni daladala kujaza watu kama zitakavyo -- makonda wana msemo wao gari haijai. Ukiacha COVID-19, ndani ya daladala iliyobeba watu waliojaa kama magunia ni chanzo kingine cha kuambukizana magonjwa kwa njia ya hewa na kugusana/kubanana. Adha ya kubanana huku kukiwa na joto kama tanuru kwa daladala hasa za Dar ni chanjo cha stress na frustrations kwa watu wengi.
Daladala ikishapakia watu wakajaa kwenye seats tu haisimami popote isipokuwa kama inashusha. Daladala zilikuwa zinasimama vituoni au barabarani hata kama zimejaa kwa lengo la kuendelea kubeba abiria, hili ndilo tatizo lililokuwa linasababisha barabara zipitike kwa shida. Maoni yangu ni kuwa huu utaratibu uendelee, na watu vituoni waanze kupanda kwa foleni, yaani aliyefika wa kwanza mpaka wa mwisho.
Nimeweza kufika nilikokuwa naenda haraka sana kuliko kawaida, na kutambua kumbe nilipokuwa naenda ni pafupi mno.
Pamoja na haya "matrafiki" waache tabia zao za kuongoza magari badala ya taa, hawa ndio tatizo jingine kubwa. Hivi inakuwaje trafiki anajigeuza roboti na kuanza kuongoza magari kwa mikono? Taa za kazi gani? Nilishaambiwa mapolisi hawa wa barabarani huvuta magari ya upande fulani ili kumuwahisha mtu fulani ambaye ana uhusiano naye kwa namna moja au nyingine - kiongozi, hawara, mke/mme/rafiki/etc., ni mambo ya ajabu sana! Taa zipo na zinatosha kuongoza magari, labda kama zimezima.
Abiria kukaa level seat lisiwe tu zoezi la muda kwa sababu ya COVID-19, bali liwe ni zoezi endelevu kwa sababu ni zoezi la kistaarabu, linalojali afya na utu wa abiria.
Sio nyie tu, kuna wale wazee wa kubambia ndani ya daradara nao wanatesekaKinachoniuma ni sisi 'wezi wadogo wadogo by professional' tutakula wapi, maana si kwa ustaarabu huu wa Leo kwenye daladala walaqhi'..!!
Lakini wanaruhusu wanafunzi kusimama. Bara ni ngumu shule na maofisi vikifunguluwa.