Siamini nilichokishuhudia: daladala level seat, hakuna foleni, hakuna kelele, abiria hawasukumani, makonda hawatukani, unafika haraka unakoenda

1.) Kwa mfano wa Corona ulioutolea, vifo nchini Tanzania vimeongezeka kisa Corona? Ndio sawa na wewe ulivyosema foleni imepungua kwa factor moja tu ya daladala vituoni, ndio uje useme vifo Tz vimeongezeka kwa factor moja tu ya Corona, ilihali unajua factor ni nyingi mno!
 
Nauli ya daladala mara ya mwisho ilipandishwa mwaka ____ wakati ambapo bei ya mafuta kwa lita ilikuwa shilingi _____. Toka mwaka huo, nauli imebaki vilevile, japo mafuta yamepanda bei. Hasara inafidiwa kwa abiria kurundikana. Kurudisha utaratibu wa levo siti kunaweza kusababisha kulazimika kuangalia upya nauli husika.

Starehe Gharama.

Na, je, shule zikifunguliwa, wanafunzi nao watakaa kwenye levo-siti? Starehe Gharama!
 
Sasa wewe inabidi watu wengine wakusaidie.
 
Nauli kuangaliwa upya sawa. Wanafunzi walipe nauli. Katika hali ya kawaida daladala hukubali wanafunzi mmoja, wawili, labda mwisho watatu.
 
Nauli kuangaliwa upya sawa. Wanafunzi walipe nauli. Katika hali ya kawaida daladala hukubali wanafunzi mmoja, wawili, labda mwisho watatu.

Nanukuu posti yangu kwenye uzi wa:
Wenye magari binafsi watoe lift kwa watoto wa shule vituoni ili mbarikiwe - JamiiForums

*UFUMBUZI WA KUDUMU WA TATIZO LA USAFIRI KWA WANAFUNZI*

Ufumbuzi wa masuala ya usafiri wa watoto shuleni usio na kelele wala mikwaruzo ni huu hapa:

1. Kila shule ya umma ichorewe ramani ya nyumba zinazoizunguka (catchment). Mikusanyiko ya mashule ambayo mtoto anaweza kuenda kwa kutembea itaunganishwa na kufanywa kanda (zone ) (matumizi ya GIS hapa ndio pake 😎). Ni shurti kila mtoto aliyeko kwenye kanda fulani asome shule ya umma iliyoko kanda hiyo au akakae bweni. Mtoto yoyote akiamua kusoma shule ya binafsi ruksa kusoma popote. Lakini asisumbue watu kuhusu usafiri.

2. Wanafunzi wote watakaopanda mabasi walipe nauli sawa na ya mtu mzima. (yunifomu alizovaa, viatu, madaftari, penseli, kalamu ya wino, viepe vya lanchi ya mchana 😉 , vyote hivyo hulipa kamili siyo nusu bei. Kwa nini kwenye madaladala tu ndio iwe nusu nauli?)

3. Mwanafunzi ambaye atalazimika kupanda basi kwenda shule ya umma, na hana uwezo wa kujilipia nauli kamili, apewe ruzuku kupitia kwa Afisa Elimu wilaya, ambaye atathibitisha kuwepo kwa sababu za msingi kwa nini mwanafunzi huyo hakai bweni au hasomi shule ya karibu.

Easy-peasy-lemmon-squeazy

REJEA:
Starehe Gharama

https://www.asymptotejournal.com/blog/2019/08/06/translation-tuesday-comfort-is-expensive-by-mlenge-mgendi
 
Sasa hili ni jibu au pendekezo? Maana lile ni swali linalotegemea jibu na sio pendekezo, huna jibu piga kimya na acha hoja yangu iende zake bila kikwazo.
Ndio maana nimesema usaidiwe na wengine ili hoja yako iendelee mbele.
 
Hoja zako zina mantiki sana. Mimi huwa nashangaa hili la wanafunzi kulipa nauli sijui nusu! Mfano, mimi sio tajiri lakini sioni sababu ya mtoto wangu kulipa nusu nauli ya daladala, atalipa hela kamili.
 
Level seat kwa daladala za Temeke Mbezi mbona zimegoma?!

Unaongelea za daladala zipi mkuu mie nipo hapa Mbezi shamba yaani ni vurugu tupu watu wanagombana ili kuwahi seat na bado waliokosa seat wanan'gan'gania kuingia tu kwa kubanana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dada unaenda wapi..naenda Temeke..
Hamna siti shuka...

Dada unaenda wapi...naenda Ubungo..panda kaa pale..

makonda wanabalance hesabu wanajua akikushusha ubungo akapakia wa tabata,tabata akapakia wa Temeke siti moja itakaliwa na watu watatu kidogo hesabu itabalance
 
Hesabu yako ina assume gari linatumia maji badala ya mafuta. Weka Trip moja inatumia mafuta kiasi gani? Weka gharama ya vipuli na service kisha igawanye kwa siku.
 
Corona ikiisha tupate faida zifuatazo
1. Daladala Seat Level
2.. Kupanda Daladala au Usafiri wote wa Umma Kwa Foleni/mlolongo na bila mpiga Debe.3
3. Kila anayekohoa/Mafua/chafya/miayo avae Mask au azibe mdomo/pia Kwa handkachifu(leso). Hii ni popote kwenye Public. Ikiwezekana owe Sheria na Faini Kwa atakayeshindwa. Tumechoka kuambukizwa Magonjwa.
4. Kila anawe mikono kabla na baada ya Kazi Ofisini.
 
Kinachoniuma ni sisi 'wezi wadogo wadogo by professional' tutakula wapi, maana si kwa ustaarabu huu wa Leo kwenye daladala walaqhi'..!!
Sio nyie tu, kuna wale wazee wa kubambia ndani ya daradara nao wanateseka
 
Hivi Kama Mwendokasi inajazia Kimara mnaopandia vituo vya katikati inakuaje
 
Naunga mkono hoja, huu utaratibu uwe endelevu.
Kiukweli jana na leo nimeenjoy sana.
 
Haya mambo watu wanafanya masiara...jioni nilipanda coaster moja kinondoni akazidisha abiria wakati wengine wako level..tumefika magomeni wajomba wamamdaka na afande kaenda nae kituoni...watu watii maelekezo jamani yaani mpaka unaniuliza hivi kweli hali ilivo kwa wenzetu wengine wanachukulia simple tu...jamii yetu ni kweli tunapuuzia namna hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…