Siasa: Kama hii katuni ya chatu na mbwa imechorwa na Masood Kipanya basi anapaswa kupewa tuzo ya kutuchanganya

Siasa: Kama hii katuni ya chatu na mbwa imechorwa na Masood Kipanya basi anapaswa kupewa tuzo ya kutuchanganya

Tafsiri

Chadema wamejisalimisha kwa CCM na sasa CCM inawapeleka Chadema inapo taka mbaya zaidi CCM inawarudisha nyuma chadema inawezekana wakafa kabisa kwa sababu CCM wameingia ndani na wameshaharibu mifumo Yao yote. Kuanzia upuaji hadi mmeng'enyo wa Chakula ina maana mpaka Leo Chadema hawana moyo maini wala figo. WAMEKWISHA. SALUTE KWA KIPANYA.

Nmejaribu kutafsiri[emoji23][emoji23]
Kwanini huyo wa kijani asife,mbona utumbo wake umesha haribiwa,hata kutembea kwake anatumia miguu ya aliyemmeza
 
Kwa haraka haraka mbwa na chatu kila mmoja anataka kwenda njia yake kimbem

Kwanini huyo wa kijani asife,mbona utumbo wake umesha haribiwa,hata kutembea kwake anatumia miguu ya aliyemmeza
CCM (Chatu)wameimeza CDM( mbwa) ila Chatu hana uwezo tena wa kutambaa,mbwa ndiye anayempeleka japo haoni uelekeo😂😂. Mwisho wa game Chatu ameshatobolewa tumbo atakufa tu na akioza mbwa anatoka na kusonga mbele😂😂
 
View attachment 2544444

1. Yaani hapo kuna mbwa na chatu.
2. Chatu amemmeza mbwa.
3. Miguu ya mbwa imetoboa tumbo la chatu.
4. Mbwa anatembea huku amemezwa.
5. Najaribu kulitazama jicho la chatu nimebaki nimeduwa sielewi kwanini liko hivo.

..katuni inaonyesha " WIN-WIN " situation.🤣

..Mbwa ameshinda, na Chatu ameshinda.
 
View attachment 2544444

1. Yaani hapo kuna mbwa na chatu.
2. Chatu amemmeza mbwa.
3. Miguu ya mbwa imetoboa tumbo la chatu.
4. Mbwa anatembea huku amemezwa.
5. Najaribu kulitazama jicho la chatu nimebaki nimeduwa sielewi kwanini liko hivo.

Kwa mawazo yangu. Chatu ni CCM Alafu Mbwa ni CHADEMA.

Hii katuni mwanzo ilionesha mbwa kamezwa na chatu na alibaki miguu tu ( CCM iliwameza CHADEMA kwa wakati uliopita)

Wakati huu inaonesha mbwa kutoa miguu na anatembea ila kichwa ni cha chatu (CCM imewapa unafuu CHADEMA ila kwenye uelekeo Bado hawapo pamoja)
 
Tafsiri

Chadema wamejisalimisha kwa CCM na sasa CCM inawapeleka Chadema inapo taka mbaya zaidi CCM inawarudisha nyuma chadema inawezekana wakafa kabisa kwa sababu CCM wameingia ndani na wameshaharibu mifumo Yao yote. Kuanzia upuaji hadi mmeng'enyo wa Chakula ina maana mpaka Leo Chadema hawana moyo maini wala figo. WAMEKWISHA. SALUTE KWA KIPANYA.

Nmejaribu kutafsiri[emoji23][emoji23]
Kumbe eeh Hongera
 
Kuna Taasisi Fulani imeimeza Taasisi nyingine kupitia maridhiano,ila baada ya muda Taasisi iliomezwa inafufuka na kuanza kuipeleka njia tofauti na anaconda alivyozoea. Anakonda ametoa jicho! Teh teh!
 
Tafsiri isiyo rasmi.

Joka(ccm) amemmeza mbwa(makamanda)ili amtumie kukimbia na kufika anapopataka,japo umbwa kagezia miguu nyuma,akiwa na maana ana ajenda zake,ila haoni wala,itabidi atumie macho ya joka na kukosa kabisa maamuzi ya wapi aelekee.

Thats why tunaona watu wameanza kuimba mapambio ya kusifu na kuabudu.
 
CCM (CHATU), MIGUU YA MBWA (MIHIMILI YA DOLA + WANANCHI)... CCM(CHATU) imemeza mihimili yote ya dola pamoja na wananchi wake wote.. Huo uelekeo wa chatu na miguu ya mbwa kuwa tofauti - Hii inaamanisha DIRA ya Taifa na Dira ya chama tawala kwasasa ni tofauti kichwa cha CHATU(Rais) kinaonekana kuingalia miguu ya mbwa kana kwamba imemzidi nguvu ya uelekeo wake na sasa anatafakari namna ya kuishinda hiyo nguvu japo ni kama kashachelewa maana MBWA HAJAFA na sasa anapata wasiwasi kuwa tayari kashakosea na yeye yupo kwenye hatari ya kufa(kupoteza nguvu aliyo nayo madarakani).
Hujafuatilia toka mwanzo. Mbwa wa rangi ya Kaki ni CHADEMA
 
Kiuhalisia hapo angeongezewa na mfugaji wa chatu na mbwa (mwananchi) anaangaika kuwatafutia mifugo hii chakula wao wanaendeleza sarakasi episode moja baada ya nyingine huku wakiendelea kunyonya jasho la mfugaji (inabidi awachinjilie mbali wote na kuwala kitoweo)
 
Tafsiri

Chadema wamejisalimisha kwa CCM na sasa CCM inawapeleka Chadema inapo taka mbaya zaidi CCM inawarudisha nyuma chadema inawezekana wakafa kabisa kwa sababu CCM wameingia ndani na wameshaharibu mifumo Yao yote. Kuanzia upuaji hadi mmeng'enyo wa Chakula ina maana mpaka Leo Chadema hawana moyo maini wala figo. WAMEKWISHA. SALUTE KWA KIPANYA.

Nmejaribu kutafsiri[emoji23][emoji23]
sukuma gang bhana.
 
Hapo Mbwa ( Chadema) kajinyenyekeza mpaka kaingia ndani kabisa ya Nyoka ( CCM). Chadema wamo ndani ya tumbo la Nyoka lakini bado hawajakufa, ndiyo maana miguu ya Mbwa imesimama imara.
Kwa kifupi ngoma droo. CCM wakiharibu nje, Chadema wataharibu ndani. Yaani watamtafuna Nyoka mpaka atakwisha na kutoka nje ya tumbo. Ni kama Chadema ndiyo wameshkilia mpini.
 
View attachment 2544444

1. Yaani hapo kuna mbwa na chatu.
2. Chatu amemmeza mbwa.
3. Miguu ya mbwa imetoboa tumbo la chatu.
4. Mbwa anatembea huku amemezwa.
5. Najaribu kulitazama jicho la chatu nimebaki nimeduwa sielewi kwanini liko hivo.
Halafu huu naona ni mwendelezo wa zile katuni zingine mbwa alikuwa anaombwa amezwe alipokubali ikawa swadakta sasa leo tena katoboa tumbo na anamkontro chatu.
CCM VS CHADEMA.

wapo pamoja ila mielekeo tofauti.
CHADEMA {mbwa} amekubali kuwa na CCM {chatu wa kijani} ila sasa misimamo tofauti, ndiyo maana miguu imeelekea uelekeo mwingine kabisa.
 
View attachment 2544444

1. Yaani hapo kuna mbwa na chatu.
2. Chatu amemmeza mbwa.
3. Miguu ya mbwa imetoboa tumbo la chatu.
4. Mbwa anatembea huku amemezwa.
5. Najaribu kulitazama jicho la chatu nimebaki nimeduwa sielewi kwanini liko hivo.
Mbwa kamezwa na chatu katobolewa tumbo. Maana yake wote watakufa maana tumbo likitoboka huponi na kichwa cha mbwa kimo ndani hawezi kupumua.

Yaani CCM na CDM wote wako ICU
 
Back
Top Bottom