Siasa kwa wengine ni Biashara, wengine ni Wito, wengine ni fursa ya kujipatia umaarufu

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo! Mimi sijambo

Unapoingia kwenye siasa usiingie kichwa kichwa kama panya kwenye shimo ambalo hakulichimba.

Asilimia kubwa ya watu siasa kwao ni fursa ya kibiashara na kiuchumi. Wao siasa wameingia kwa sababu ya Maslahi Yao ya kiuchumi.
Hivyo chochote anachokifanya ndani ya siasa kitazingatia mambo ya uchumi. Kujipatia kipato. Hill Kundi ndio kubwa zaidi.

Wachache Sana siasa kwao ni Wito. Yaani wanawiwa au kuwashwa rohoni kama utume vile. Kuwa viongozi ili waisaidie Jamii Yao. Kundi Hili ni wachache Sana. Sana yaani.
Na watu wa Aina hii hawapatikani wakati wote.

Kundi LA mwisho ni wale wapenda sifa, umaarufu, kuzungumzwa, na mambo ya namna hii.
Kundi Hili sio wengi pia. Hawa wapo radhi hata kufa maskini Lakini ilimradi Kamera zinawafuata, magazeti yanawataja Taja, kutembea na ving'ora. Yaani hiyo ndio furaha na mafanikio Yao.

Kiongozi gani yupo kundi gani? Je wewe kama ungekuwa mwanasiasa ungekuwa kundi lipi?

Mjadala Mezani.
 
dada ShesRise_1 kwa taarifa na kumbukumbu
 
Back
Top Bottom