jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Umenena ukweli kabisa..kwasasa nchi hii vijana wengi hasa graduates wameona njia ya kutafuta chance ya maisha ni kukimbilia siasa.Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa Tanzania tuna siasa mbovu ambazo kimsingi zimechangia kuua ndoto za vijana wengi wenye fani na taaluma mbalimbali ambazo wamezihangaikia tangu wakiwa wadogo mpaka wanakuwa watu wazima.
Siasa kwetu sio taaluma bali ni ajira ambayo walafi wa madaraka ( power hungry people ) wanaipigania kwe njia zote mbaya na nzuri. Kwa mazingira haya tunapata viongozi ambao hawana sifa wala uzalendo kwa taifa lao.
Vijana wasomi wamegeuka kichekesho ( laughing stock ) kwani wengi wamejikuta unemployed sio kwa sababu hawana uwezo ila maitaji nimadogo kuliko idadi yao.
Political leaders wetu wengi ni materialistic kwani hawajali lolote kuhusu kutengeza sera bora ya elimu na uchumi ili kuwasaidia vijana waweze kujijengea uwezo wa kujiajiri na kupata mtaji kwa urahisi.
Watanzania tunajuana maisha yetu vijana hasa watoto wa wakulima ni ngumu sana kwao kujiajiri bila kuwa na mazingira wezeshi.
Hili ni timed bomb personally naliona kwenye taifa langu, maana decision makers wetu wengi ni greenhorn na wanachoweza kikubwa ni lick miguu ya mkubwa badala ya kusimamia taaluma zao.
Roho inaniuma basi tu
Wengi choka mbaya hawana future zaidi ya kuwa chawa na walamba miguu ya viongozi..ili anagalau wafikiriwe kwenye teuzi au vipesa vidogo vidogo wakitumika kueneza propaganda mbovu kwa jamii.
Kimsingi njaa ikihamia kichwani ni tatizo kubwa sana..hii nchi imepoteza maono chama cha kijani sasa sio chama cha wanachi bali limekuwa genge la walaghai.
#MaendeleoHayanaChama