Siasa Michezoni (Simba vs Al Ahly): Azam TV wanapaswa kuonywa, kuadhibiwa au kufungiwa!

Kwa kifupi sana kwa sheria za soka za FIFA na CAF lile lilikuwa ni kosa, na kama litashikiwa bango huenda Azam TV na mamlaka za soka hapa Tanzania zikajikuta matatani.


Ndiyo sisi hao
 
Nchi za ulaya zilionyesha mabango kuisapoti Ukraine, hapo hukuliona hilo wala kushangazwa kama unavyoshangaa leo hii.

Kuhusu Udini kwa Azam hapo hata mimi naunga hoja, JAMAA NI WADINI WA KUFU MTU Pia wamejaa ukanda kupita maelezo NADHANI HATA FEISAL ANGEKUWA NI JOHN WA SINGIDA ASINGERUBUNIWA.
 
Huu ni upuuzi,

Vita ya ukraine watu kibao walitoa yao ya moyoni wazi wazi.
Mie sioni kosa hapo.
 
Wewe mleta mada ndie una shida
Unafikiri jana matangazo ya mpira yalikuwa yana controliwa na azam.
Jana shughuli yote A to Z ilisimamiwa na CAF.
 
Ireland na wa scottish wazi tu wana support Palestine na sababu kubwa hata wao wana history ya kukaliwa kimabavu na kunyanyaswa wanajuwa machungu yake ndio maana kwenye mechi ya Celtic bendera za Palestine kibao shida hawa huku wenye makanisa kama mabanda ya kuku na bendera za Israel bila kujuwa maana yake. Mungu ni wa wote hakuna aliyempendelea na kama yuko huyo Mungu anapendelea basi natamka hakuna Mungu.
 
Wewe mleta mada ndie nyumbu.
Unafikiri jana matangazo ya mpira yalikuwa yana controliwa na azam.
Jana shughuli yote A to Z ilisimamiwa na CAF.
Kabisa production team yote ya nje wazungu wa CAF basi watu chuki tu za kidini. Uzuri uchumi mkubwa Tanzania unashikwa na hao hao wanaowachukia 😛
 
Binadamu bwana jambo lile alilifanya mzungu wakati Ukraine wanapigwa wanavamiwa lilionekana sawa ila leo kwakuwa wamefanya warabu imekuwa ugaidi.
 
Sasa hapa Azam ana kosa gani? Uchonganishi tu. Kama ni watu wenyewe wachache wameamua kuandika hivyo tatizo liko wapi? Wakiandika ‘Mama anaupiga mwingi’, ungeona sawa. Huo ndio uhuru wa mawazo bwana wewe.
 
Kama siyo bango la ''mama anaupiga mwingi'' hamna neno. Hilo linatetea haki tofauti na la Samia amabalo linaunga mkono ukandamizaji.
 
Kwani waandaaji wa hiyo African super league wamemaindi ?
 
Wewe ni mjinga.

Kila kitu kina mahali pake na taratibu zako. Sheria za soka haziruhusu soka kutumika kwenye mambo yasiyohusiana na soka.

Waandamane huko barabarani, siyo kwenye soka.
Uefa wakiona hii comment yako watakucheka sana.
 
Tatizo nini hapo? Washabiki au Azam?
 
Mkuu Al Ahly katika mechi ya marudiano na Simba wamesema wazi mapato yote watakayoyapata watayatoa kwa Wapalestina vipi kwa kauli yao hiyo na kitendo wanachotaka kukifanya wataondoshwa kabisa mashindanoni?
 
FIFA huwa hawataki mambo ya siasa michezoni. Hujawahi kusikia hilo mkuu?
Al Ahly licha ya kuwaunga mkono Wapalestina waziwazi wamesema hata mapato watakayoyapata katika mechi ya marudiano na Simba yooote watayapeleka kwa Wapalestina kwa hiyo Fifa itawafungia kabisa au itakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…