GE2025 Siasa ni chaguo lakini Kila chaguo linamfichua mtu alivyo ndani yake

GE2025 Siasa ni chaguo lakini Kila chaguo linamfichua mtu alivyo ndani yake

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

MTAZANIA

Member
Joined
May 28, 2025
Posts
28
Reaction score
47
Ndugu zangu, tuseme ukweli usiofunikwa na siasa za kupaka sukari!"

Wafuasi wa CHADEMA wamegawanyika katika njia tatu — na kila njia ina hadithi yake.

Waliokimbilia CHAUMA
Hawa ni wanasiasa waliochukua uamuzi si kwa tafakari ya kina, bali kwa msukumo wa kundi. Ni kama mtu anayeongozwa na kelele za umati kuliko sauti ya dhamira yake. Ni kama inzi – hata ukimpa ice cream, bado atarudi kukaa kwenye mavi. Walivutwa na hisia za muda, si maono ya mbali.

Waliokimbilia CCM
Hapa tunazungumzia wale waliokosa subira ya kisiasa. Wale ambao tamaa ya madaraka imewapofusha kuona kwamba uongozi wa kweli ni safari ndefu yenye maumivu na kujitolea. Walihisi njia fupi ipo CCM, na wakakimbilia humo kama mtu anayekimbilia kivuli cha miti wakati bado hajapanda mti wake mwenyewe. Ni uroho wa mamlaka, si ujenzi wa taifa. Kama nitaoata nafasi ya kuonana na mchugaji ningemwambia hili bila kupepesa macho

Waliokimbilia ACT Wazalendo
Hawa wanabeba hadithi tofauti. Walisoma alama za nyakati, wakaona upepo mkali wa kisiasa ndani ya CHADEMA, na wakaamua kusaka anga jipya. Hawa si wafuasi tu, ni wabeba hoja, ni watu wenye maono. Ni wale ambao kesho tunaweza kuwaona wakibeba kijiti cha uongozi wa taifa, kwa sababu waliona mbali na wakaamua kusimama upande wa imani zao.

"Hii ndiyo siasa — na siasa ni chaguo. Lakini kila chaguo linamfichua mtu alivyo ndani."
 
Back
Top Bottom