Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 2,912
- 12,904
Salamu JamiiForums
Juzi wakati timu yangu pendwa ya Arsenal na Aston villa zikitoka Sare ya bao 2 Kwa 2 nikaona bora nihame sehemu ile na kwenda sehemu nyingine nikazugezuge na habari za siasa .
Haswa ukizingatia chama cha
Demokrasia na maendeleo kimechukua headlines nyingi Kwa kipindi hiki.
Nilitafuta kiti nikakaa huku nikimuona jamaa fulani aliyevalia nguo za CDM akiwa kafura kakasirika mno,akaniuliza natumia kinywaji gani,nikajibu ni maji tu inatosha kwani pombe nilishaacha.
So alionekana kama anataka kuniuliza swali lakini kabla hajauliza kuna jamaa akawa anatokea Chooni huku akimwambia jamaa kuwa TUNDU ANTIPAS LISSU hana nguvu wala ushawishi wa kupata kura mbele ya mwamba wa kaskazini FREEMAN AIKAEL MBOWE .
Yule jamaa aliyenilipia maji ambaye nilitambua ni timu LISSU akawa kachachamaa anataka kupigana tena anatetemeka kabisa.
Waiter wa mule ndani akanishauri niondoke akidai yule jamaa ana mapenzi na LISSU yaani anamkubali ile mbaya. Hivyo yeyote anayepingana naye huwa hamcheleweshi.
Niliinuka huku nikijifanya naongea na simu huku nikicheka peke yangu ni jinsi gani tunagombana wakati juzi Kati Mbowe na Lissu walikuwa meza moja wakicheka na kufurahi.
Haya ukiangalia na kusikiliza namna mnyalukolo mwenzangu Yeriko Nyerere anavyompiga spana Lissu ni ngumu kuamini kama Leo wamekutana na kupiga stori pamoja.
Je, sisi wananchi wa kawaida huwa tunakwama wapi?
Pichani ni Yeriko Nyerere na Mgombea Uenyekiti bara Hon.Tundu lissu.